Chama cha walimu tanzania hakipo kwa manufaa ya walimu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha walimu tanzania hakipo kwa manufaa ya walimu.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mkulia, Oct 4, 2012.

 1. M

  Mkulia JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 342
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mimi ni mwalimu na pia ni mwanachama wa chama hiki cha walimu Tanzania. Kwa ujumla hiki chama (CWT) hakipo kwa ajili ya manufaa ya walimu bali kwa manufaa ya mwajiri. Nasema hivi kwasababu walimu tuna matatizo mengi sana ya kimasilahi lakini chama kinashindwa kuyasimamia. Kwa mfano mgomo uliokuwa umeitishwa na chama mwezi uliopita haukupaswa kusitiishwa hadi madai ya walimu yatekelezwe. Chama hakikupashwa kusikiliza vitisho vya serikali badala yake kingeshikilia msimamo wake uleule wa mgomo mpaka kieleweke. Angalia chama cha walimu cha kenya kilivyosimama kidete kutetea mishahara 300% ya walimu wake mpaka wamefanikiwa. Sisi Tanzania hata 1% tumeshindwa kupata. Hakika walimu tunapaswa kukitazama chama hiki upya na ikiwezekana ku-review katiba yetu ili makatibu wa chama wa wilaya, mikoa na taifa wasiwe waajiriwa wa kudumu badala yake kuwe na specific period of time ya kukaa madarakani. Makaribu wetu wote wamejisahau na wanachofanya kwa sasa ni kubuni vitega uchumi kwa manufaa yao na siyo kwa manufaa ya walimu. Hebu angalia ile MWALIMU HOUSE ina manufaa gani kwa mwalimu? Makato ya mishahara ya walimu kila mwezi yanayokwenda kwenye chama yanatunufaisha vipi mwalimu? INAUMA SANA.
   
 2. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yaaaani sana 2 mkubwa.
   
Loading...