Chama cha Walimu kuna haja ya kuwapa semina wanachama wenu kuhusu masuala ya pesa na maisha baada ya kustaafu?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Kwakweli walimu wana tatizo kuhusu suala la pesa. Wengi hawajui masuala ya pesa na uwekezaji.

Utapeli wowote wa kipesa lazima uwahusishe waalimu kwa wingi. Ila sijajua kama ni sababu ya wingi wao au wanapigika kirahisi? Vyovyote vile, kuna tatizo.

CWT andaeni semina za kuwafundisha watu wenu kuhusu masuala ya pesa na uwekezaji, hasa wale wanaokaribia kustaafu. Inauma mtu kutapeliwa hela yake ya mafao.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png

Wanapigika kirahisi. CWT inatakiwa yenyewe ijitathmini kama inafaa kuendelea kuwepo na kuendelea kutumbua hela za wanachama wake wakati hawana msaada wowote kwa walimu. Inatakiwa wajitoe kwenye hicho chama kwani siyo lazima. Provided kwamba unatoa notice ya mwezi mmoja kwa mwajiri
 
Wastaafu wanao tapeliwa ni wengi sana nimeshuhudia daktari mstaafu akitapeliwa 30mil , lakin walimu wanasikika sana kwa sababu kwanza ni wengi sana katika kundi la wanao staafu hivyo kelele ni nyingi sana.
 
Wastaafu wanao tapeliwa ni wengi sana nimeshuhudia daktari mstaafu akitapeliwa 30mil , lakin walimu wanasikika sana kwa sababu kwanza ni wengi sana katika kundi la wanao staafu hivyo kelele ni nyingi sana.
Basi kuna haja ya vyama vyote vya kitaaluma kuanza kuwaelimisha watu wao elimu ya fedha.
 
Mbona kuna walimu wajanja tu..hao wanaopigwa kifala ni wa huko Nguriati tu.
 
Ni kweli kabisa Walimu wakistaafu wengi wanaishiwa kutapeliwa au kuingia kwe biashara za ajabu ajabu ambazo mwishowe wanapoteza hela zao zote.CWT wanatakiwa kuja na mwarobaini wa hili tatizo sugu.Au wanaweza iga Chama cha kuweka na kukopa cha walimu wa Moshi Vijijini (MRTS).

Hawa wana program ya kuempower walimu wastaafu ambayo mpaka sasa wastaafu zaidi ya 200 ,wamewekeza pesa za mafao yao. Chini ya uongozi wa chama,wanapata faida nono na pia wanapatiwa mafunzo kabla ya wao kufungua biashara.
 
CWT ni majambazi pamoja na Benki Ya Walimu ,maana iwapo wangekuwa na huruma na Wanachama wao,Walimu hawakutakiwa kutaabika kiasi hiki.Je Mwalimu Bank ina faida gani kwa Walimu wa Tanzania?
 
Nahisi hili ni muhimu kwa wastaafu wote na si kwa walimu pekee.

Kuna boss mmoja namfahamu alitapeliwa 60ml baada ya kustaafu..alafu kizembe Sana😂😂
 
CWT ni majambazi pamoja na Benki Ya Walimu ,maana iwapo wangekuwa na huruma na Wanachama wao,Walimu hawakutakiwa kutaabika kiasi hiki.Je Mwalimu Bank ina faida gani kwa Walimu wa Tanzania?
Hapa napo pana tatizo. Ingeweza kuwa inachuana na NMB na CRDB kwa wingi wa waalimu. Ingeweza kutoa mikopo kwa riba nafuu zaidi.
 
walimu ni wengi,mshahara ukitoka tu wao ndiyo hujaza foleni za atm,na ndiko huko matapeli huwalia timing kutaka kuwaibia.CWT haina wataalamu wa kutoa elimu za fedha labda mtaalamu atoke nje ya kada hiyo.Halafu lini cwt imekuwa na huruma na mwalimu? madhila mangapi yanawapata walimu na haina uwezo wa kumsaidia mwanachama wake? kipo tu kisheria lakini hakina mpango na mwalimu
 
Back
Top Bottom