Chama cha wafanyakazi wa serikali kimetishia kuwachukulia hatua viongozi wa serikali juu ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa watumishi wa umma nje ya sheria. Kiongozi wa chama amesema kuna matumizi mabaya ya msemo wa 'hapa kazi tu' ikiwemo kuwaweka rumande watumishi wa umma, kuzuia likizo bila kusema zitafunguliwa lini, kusimamisha kazi watumishi bila kufata sheria na kadhalika. 'Hapa kazi tu inavunja misingi ya utumishi wa umma'.
Amesema sheria zipo kwa wanaotumia mamlaka yao vibaya na hawajafika bado lakini ikifika wakati watawachukulia hatua ikiwemo kuwashitaki kwenye vyombo vya sheria. Chama kimesisitiza hakitetei watumishi wazembe lakini wawajibishwe kulingana na taratibu zilizopo.