Chama cha Wafamasia Wamiliki wa Maduka ya Dawa chatoa Msaada kusaidia wahanga wa Moto

Ze Heby

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,622
2,000
August 12, 2019 na Sophia Mtakasimba

2019-08-12-170-0001.jpg

Mwakilishi wa Chama cha Wafamasia Wamiliki wa Maduka ya Dawa (POPTA) Bw.Henry Bandawe, akikabidhi Dawa na Vifaa tiba kwa Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw.Deus Buma,ambavyo ni msaada kwa wahanga wa ajali ya moto.
2019-08-12-170-0002.jpg

Mwakilishi wa Chama cha Wafamasia Wamiliki wa Maduka ya Dawa (POPTA) Bw.Henry Bandawe akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari wakati akikabidhi msaada wa Dawa na vifaa tiba kwa ajili ya Majeruhi wa ajali ya Moto.
2019-08-12-170-0003.jpg

Mkuu wa Idara ya Utasishaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili bi. Batusaje John Akitoa neno la shukrani kwa POPTA baada ya kupokea msaada wa Dawa na Vifaa tiba kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto.

Na Sophia Mtakasimba
Chama cha Wafamasia wamiliki wa Maduka ya Dawa (POPTA) wametoa msaada wa dawa na vifaa tiba kwa ajili wa majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro, ambao wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza leo wakati wa makabidhiano wa vifaa hivyo, yaliyofanyika Hospitalini hapa mwakilishi wa POPTA Bw. Henry Bandawe amesema chama hicho kimeona kuwa majeruhi wanahitaji kusaidiwa hasa katika vifaa na dawa kwa ajili ya tiba.
“Hizi dawa tulizoleta ni zile ambazo sisi tumeona kwa uharaka wake zinahitajika, zinazojumisha dawa za moto (burn cream), maji yanayowekwa kwenye mishipa (infusion water)), gozi pamoja na pamba. Kwa ujumla ni zile dawa zinazotumika kutibu majeraha ya moto” alisema Bw. Bandawe.
Aliongeza kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni tano vimetolewa kwa haraka, lakini kama kuna uhitaji zaidi POPTA ipo tayari kuendelea kuchangia,ikiwa ni kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli ambaye alifika Hospitali kuwajulia hali wajeruhi hao.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Hospitali, Mfamasia Mkuu Bw. Deus Buma amewashukuru sana POPTA kwa kuunga mkono Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kuhudumia wagonjwa hao na hii inaonyesha jinsi watanzania tulivyo na umoja katika kusaidiana kwenye majanga.
Naye mkuu wa idara ya utasishaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi.Batusaje John Mwaibanje ameshukuru POPTA kwa msaada huo kwa kuwa vifaa walivyoleta ndivyo hasa vinavyotakiwa katika kuwa hudumia wagonjwa wa moto.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom