Chama cha waalim Tanzania {CWT} igeni wenzenu wa chama cha waalimu Kenya.

Shamge

Member
Sep 4, 2011
21
0
Hongereni sana chama cha waalimu Kenya kwa kupata suluhu ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili, na poleni saaana CWT kwa kupigwa danadana na viongozi mliosimamia uchaguzi wao na kuwapa ulaji. Ndugu zanguni waalimu naowaombeni sana muweze kutumia mfano wa wenzetu wakenya kwenye kudai haki zenu, inasononesha sana na kusikitisha saana kuona kila mwaka mnatangaza mgogoro KIBOGOYO na serikali yetu bila kuona madhara ya mgogoro,
Kwa kila mtanzania hata mwenye uelewa mdogo kama wa kwangu huwa anatambua ya kwamba Serikali yetu inawasikiliza wapiga kelele hivyo pindi mnapotangaza mgomo tunaomba mgome kiukweli ila sio kelele za mbu nje ya net ambazo hazimzuii mtu kuchapa usingizi.
Nipende kutoa ushauri wangu wa dhati kwa uongozi wa Chama C ha Waalim Tanzania kuwa kama meshindwa kudai haki za waalimu wetu wa Tanzania badilisheni chama chenu ili kiwe ni chama cha siasa kwani watanzania wengi wana imani kubwa sana na waalimu so hatutowanyima kura ili muende kusaidia wenzenu, but kwa kifupi sisi watanzania tumechoshwa na kelele butu za migomo yenu toka kwa uongozi wenu usiokuwa na madhara. KUMBUKENI YA KWAMBA" NO CONFLICTS NO DEVELOPMENTS"
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom