Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 36,283
- 43,720
Skauti ni mahali sahihi zaidi kwa vijana kujifunza uzalendo, uongozi, ushirikiano, umoja na mambo mengine muhimu ya kimaisha bila kuwapa vijana ambao ni washiriki wake hali ya ujivuni wa kijeshi kama walivyo wengi wa JKT.
Ningeshauri serikali iwekeze katika kuimarisha zaidi skauti kwa sababu ina gharama ndogo sana, iko katika sehemu kubwa ya nchi na italeta ufanisi zaidi katika kuwajengea vijana uzalendo bila kuwaweka mbali na raia.
VETA ni mahali sahihi zaidi pa kujifunza stadi za kazi kuliko sehemu nyingine yoyote kwa Tanzania hii. Huko kuna wataalamu wa ufundi wa kila aina, wa ujenzi n.k mambo ambayo yanahitajika zaidi katika jamii yetu badala ya kulima matikiti na kupasua mawe kwa nyundo na mikono.
Serikali iwekeze VETA kuwajengea vijana stadi za maisha na tofauti na JKT huko haitasumbuliwa kuwapatia ajira vijana wanaopitia huko.
Serikali inaweza kuangalia mambo gani muhimu yaliyopo katika mafunzo ya JKT yanayopungia Skauti na VETA ikayaongezea kwa maboresho zaidi.