Chama cha Polepole ni uzalendo, kisasi au tamaa?

Leo wigo wa siasa nchini utaandika ukurasa mwingine kwa ujio wa chama kipya.

Ni chama kilichoasisiwa na Ndugu Humphrey Polepole, ambaye si siku nyingi alikuwa mwanachama wa CCM, na kwa kweli si tu mwanachama alikuwa kiongozi wa juu kiasi cha kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Kama hiyo haitoshi alifaulu kuwaonyesha vijana kwamba yeye ni mzalendo wa kweli kwa Taifa na mwanachama mwaminifu, ambaye anaziishi vyema KANUNI au ahadi za mwana CCM, mojawapo ikiwa ni kusema kweli daima na fitna ni mwiko na nyingine inasema cheo ni dhamana sitatumia cheo changu kwa maslahi binafsi.

Wakati akiwa kiongozi wa chama alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha uzalendo kwa Taifa na uaaminifu kwa chama, hilo lilimpa heshima ya kuwa mmoja wa vijana wazalendo na viongozi wa kutarajiwa wa baadae.

Lakini baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya uongozi katika chama ghafla kile chama alichokuwa akijinasibu kukitumikia kwa moyo wote, ndani ya wiki chache kikawa ndiyo mada yake ya kukosoa asubuhi na jioni, wenye akili walijua nini kitakuja kutokea.

Muda umejibu, anakwenda kuasisi chama akiwa na wafuasi wake, hiki si la kuhoji kwa sababu ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba yetu, lakini hoja hapa ni sababu na dhamira ya kuanzishwa kwa chama hicho kipya.

Tunaweza kumuamini kwa kwa kiasi ndugu yetu huyu? uzalendo wake aliotusadikisha ulikuwa ni uzalendo wa kweli kwa Taifa au ulikuwa ni utiifu kwa mtu aliyelinda maslahi yake?

Kama uzalendo wake na uaaminifu wake kwa chama ingekuwa hauna nasaba na maslahi binafsi, tusingetegemea mabadiliko haya ghafla ya kiitikadi kutoka kwa mtu wa aina yake.

Chama hiki kipya kinaelezwa kufadhiliwa kuanzishwa kwake na uendeshaji wake kwa kiasi kikubwa na wafadhili kutoka nje. Je, mabeberu ambao alikuwa akiupinga mpaka hapo majuzi, ghafla wamekuwa washirika muhimu wa chama hiki kipya?

Kama kinafadhiliwa na watu wa nje, nini agenda yao, hatma ya rasilimali za Taifa ni nini kama agenda ya chama hiki ikifanikiwa?!

Ni kweli Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alitabiri kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM, lakini hii haina maana kila mwana CCM akitoka nje ya chama hicho na na kuanzisha chama unakuwa upinzani wa kweli, hoja hapa ni kwa kiasi gani upinzani umejengwa juu ya dhamira safi na njema kwa maslahi mapana ya taifa.

Kuanzisha chama kwa kusukumwa na kisasi, tamaa na maslahi binafsi, haijalishi umetoka wapi au ulikuwa nani kabla, hakitafanikiwa, mifano ni mingi na karibu kila uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka 1995, kulikuwa na mazingira ya namna hii, na hata hili si jipya, ni muendelezo tamaa binafsi za kutaka madaraka kwa gharama yoyote.
Kesha ingia hamsini za CCM, chama tawala.
Sasa ndio atajua kuwa hajui!
 
Ni kweli Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alitabiri kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM, lakini hii haina maana kila mwana CCM akitoka nje ya chama hicho na na kuanzisha chama unakuwa upinzani wa kweli, hoja hapa ni kwa kiasi gani upinzani umejengwa juu ya dhamira safi na njema kwa maslahi mapana y

Kuna upinzani uliotokea ndani ya CDM, by the way kule ACT wazalendo nafasi zimejaa mpake kianzishwe chama kingine

Huyu dogo atatafunwa na usaliti wake kwa Mzee Warioba
 
Mtu aliefanikiwa baada ya kutoka kwenye chama chake ni Zitto kabwe tu
Pole pole hana watu,hana nguvu amechoka,hicho chama kitakua kama DP tu
 
Kama ni kweli polepole anaanzisha chama chake.

Basi Tanzania kunahatar ya kuanzishwa vyama vingi vya kikanda vyenye mafungamano na ukabila.

Kama ni sukuma hangi ndio limeamua hivyo na kule kuna chaga gangi.badi watu wa usalama,walingalie hili kwa ukalibu sana.
Lasivyo ukabila na ukanda unakuja kwa staili ya vyama.
Point 👏🏾👏🏾
 
Hahaaaa!!!!hamtoacha kuweweseka mpk mwisho wa maisha yenu
Umetumwa au, subili akitangaze ndo uje na mbwembwe zako hapa.

Na kama ameanzisha chama basi ni sawa kama hatavunja sheria kama wale wa ufipa.

Tunataka chama mbadala chenye siasa safi ambacho kitaweza kusaidiana na chama cha mapinduzi na sio matapeli wa ufipa.
 
Leo wigo wa siasa nchini utaandika ukurasa mwingine kwa ujio wa chama kipya.

Ni chama kilichoasisiwa na Ndugu Humphrey Polepole, ambaye si siku nyingi alikuwa mwanachama wa CCM, na kwa kweli si tu mwanachama alikuwa kiongozi wa juu kiasi cha kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Kama hiyo haitoshi alifaulu kuwaonyesha vijana kwamba yeye ni mzalendo wa kweli kwa Taifa na mwanachama mwaminifu, ambaye anaziishi vyema KANUNI au ahadi za mwana CCM, mojawapo ikiwa ni kusema kweli daima na fitna ni mwiko na nyingine inasema cheo ni dhamana sitatumia cheo changu kwa maslahi binafsi.

Wakati akiwa kiongozi wa chama alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha uzalendo kwa Taifa na uaaminifu kwa chama, hilo lilimpa heshima ya kuwa mmoja wa vijana wazalendo na viongozi wa kutarajiwa wa baadae.

Lakini baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya uongozi katika chama ghafla kile chama alichokuwa akijinasibu kukitumikia kwa moyo wote, ndani ya wiki chache kikawa ndiyo mada yake ya kukosoa asubuhi na jioni, wenye akili walijua nini kitakuja kutokea.

Muda umejibu, anakwenda kuasisi chama akiwa na wafuasi wake, hiki si la kuhoji kwa sababu ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba yetu, lakini hoja hapa ni sababu na dhamira ya kuanzishwa kwa chama hicho kipya.

Tunaweza kumuamini kwa kwa kiasi ndugu yetu huyu? uzalendo wake aliotusadikisha ulikuwa ni uzalendo wa kweli kwa Taifa au ulikuwa ni utiifu kwa mtu aliyelinda maslahi yake?

Kama uzalendo wake na uaaminifu wake kwa chama ingekuwa hauna nasaba na maslahi binafsi, tusingetegemea mabadiliko haya ghafla ya kiitikadi kutoka kwa mtu wa aina yake.

Chama hiki kipya kinaelezwa kufadhiliwa kuanzishwa kwake na uendeshaji wake kwa kiasi kikubwa na wafadhili kutoka nje. Je, mabeberu ambao alikuwa akiupinga mpaka hapo majuzi, ghafla wamekuwa washirika muhimu wa chama hiki kipya?

Kama kinafadhiliwa na watu wa nje, nini agenda yao, hatma ya rasilimali za Taifa ni nini kama agenda ya chama hiki ikifanikiwa?!

Ni kweli Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alitabiri kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM, lakini hii haina maana kila mwana CCM akitoka nje ya chama hicho na na kuanzisha chama unakuwa upinzani wa kweli, hoja hapa ni kwa kiasi gani upinzani umejengwa juu ya dhamira safi na njema kwa maslahi mapana ya taifa.

Kuanzisha chama kwa kusukumwa na kisasi, tamaa na maslahi binafsi, haijalishi umetoka wapi au ulikuwa nani kabla, hakitafanikiwa, mifano ni mingi na karibu kila uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka 1995, kulikuwa na mazingira ya namna hii, na hata hili si jipya, ni muendelezo tamaa binafsi za kutaka madaraka kwa gharama yoyote.
 
Acha kusifia TU kama fitina ameeziishi sana na kuzosimamia, kuwakandamiza wapinzani wa chama chake Cha mwanzo na kuwahujumu, na kusimamia hujuma kwenye chafuzi🤔.
 
Chama chake ni CCM na hatoki hadi abebwe mzobe mzobe na wenye nguvu atupwe dirishani!
 
Back
Top Bottom