Chama cha Mapinduzi kimeipongeza ACT Wazalendo kwa kushinda Ubunge jimbo la Konde

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
"CCM kinatoa pongezi kwa Chama Cha ACT - Wazalendo kwa kushinda katika jimbo la Konde Na hii ndiyo demokrasia kama ambayo Rais Samia mara baada ya kuingia madarakani aliahidi kwamba katika uongozi wake ataimarisha dhana nzima ya siasa safi na demokrasia ndani ya nchi yetu" SHAKA
 
Sio tu kupongeza hata kushirikiana sio mbaya, kama tunavyoona wawili hawa.

images (35).jpeg
 
Hili igizo ndilo walilopanga kulifanya baada ya yule jamaa wa CCM kutangaza kujiuzulu kwasababu za kifamilia.

Huu usanii hausaidii chochote, japo naamini umefanywa Zanzibar ambako ni nyumbani kwa mama na ACT ni washirika wao kwenye mseto.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
"CCM kinatoa pongezi kwa Chama Cha ACT - Wazalendo kwa kushinda katika jimbo la Konde Na hii ndiyo demokrasia kama ambayo Rais Samia mara baada ya kuingia madarakani aliahidi kwamba katika uongozi wake ataimarisha dhana nzima ya siasa safi na demokrasia ndani ya nchi yetu" SHAKA
Zamani Wapare walikuwa wanawatania wachaga kuwa "Mchaga akikosa cha kuiba yupo radhi kujiibia kutoka mfuko mmoja kupeleka mfuko mwingine".Nahisi kuna wakati viongozi wa kisiasa hasa wa CCM wanakuwa na tabia kama za utani huo wa wachaga na wapare.Kiangalie chama cha ACT ,tuangalie kilichotokea Konde,turudi huko Ushetu.Naam n kizungumkuti.ACT wanaamini wanajenga Chama chao na ni kweli kwa utashi wa CCM kinajengeka lakini ndani ya mioyo ya watu ndivyo ilivyo?
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾

Ccm inacheza mindgame za kizee ile mbaya. Walipora uchaguzi huyo mama akiwa rais, ACT wakatishia kuvunja ndoa wakaona isiwe tabu wakamuagiza aliyetangazwa kihuni ajiuzulu. Uchaguzi ukarudiwa na ACT wakashinda tena, ila tofauti safari hii wakatangazwa ili kulinda ndoa.

Wanachokifanya ccm ni kutaka kuwavutia Cdm washiriki ili wangalau chaguzi ziwe na wapiga kura wengi, baada ya kuona chaguzi zimepuuzwa na wananchi. Siwashauri Cdm kushiriki chaguzi chini ya tume hii ya kihuni. Uchaguzi utakapokuwa huru na haki Cdm watapata kura zetu bila tatizo lolote. Hivyo wasihofu kwa hivi vitisho vya kijinga eti chama kisiposhiriki uchaguzi kinapotea kwa wananchi. Wananchi wote waelewe tunajua kwa sasa hakuna ushindani wa kisiasa, na chaguzi zilizopo sio chaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Back
Top Bottom