Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa kimemteua Christopher Chiza kuwa mgombea wa Buyungu

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFAView attachment 806519
IMG_20180710_160443_454.JPG
 
Hapo lengo lilikua ni kuongelea ndege, hizo porojo nyingine zilikua zinajulikana...lakini asante kwa kutukumbusha
 
thubutuuu, hao jamaa wakiwa nyimanyuma ya zito ccm itateseka sana!

Mlisema hivi hivi miaka ya 90 ambapo Mrema aliondoka CCM na hakukuwa na jipya na mkaja kusema tena mwaka 2015 ambako Lowassa aliondoka CCM halafu leo tena Wewe usiyejua Siasa na hata kuijua vyema CCM bila hata aibu / haya unadiriki kusema kuwa Nape na Bashe wakiondoka CCM na Kuungana na Zito Kabwe CCM itapata taabu. Nadhani huijui CCM vizuri na kwa kukusaidia tu ni kwamba ndani ya CCM hakuna mkubwa wala mdogo bali wote ni sawa. CCM Kwanza Mtu baadae!
 
Vijana wapo wengi hawatumiki mnatuletea Gari bovu lililopakwa rangi. Upuuzi!
 
Sasa kazi imebaki kwa tume na polisi wao kama chama wamemaliza kazi.
 
Chiza atapewa pande la kusimamia Dreamliner sasa hivi, kama si kwenye board, basi wizarani.
 
Dar es Salaam.Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemteua Christopher Chiza kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa tiketi ya chama hicho.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne Julai 10, 2018 kwa vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema Chiza ameteuliwa na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana leo chini ya mwenyekiti wake Rais John Magufuli.

Chiza ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo anagombea kwa mara nyingine baada ya kuangushwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 na marehemu Kasuku Bilago wa Chadema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Polepole, pamoja na mambo mengine kwa kauli moja Kamati Kuu imempongeza Rais Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM na kwa kasi kubwa ya upelekaji maendeleo na huduma za kijamii hasa katika maeneo ya pembezoni na mijini.

Pia wajumbe wa kamati hiyo kwa pamoja wameridhishwa na kuweka kauli kwamba jitihada hizo za kuongeza tija, ufanisi, faida, utumishi wa watu, uadilifu, vita dhidi ya rushwa na kupambana na ubadhirifu wa mali za chama na umma na uchapakazi kwenye chama na Serikali ziendelezwe maradufu.
 
Back
Top Bottom