Chama cha Madaktari wa Uganda Wametoa Madaktari Bingwa Kumtibu Bobi Wine

Daraja Makofia

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
695
901
Madaktari wa Uganda wamelaani vikali kuteswa kwa watuhumiwa wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama.

Kufuatia tukio la kukamatwa Mbunge Bobi Wine na kuteswa na vyombo vya usalama, Madaktari hao wameunda timu ya wataalamu wa figo na upasuaji wa aina zote ili kwenda kumfanyia matibabu ya kina mbunge huyo bure kama Rais Yoweri Museveni ataona inafaa.

Angalia video hapo chini kuona taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari.

 
Uganda nawakubali na huyu dogo atawaamsha wengi
Huku kwetu watu wanaogopa hata kivuli cha jamaa
 
'Bure kama Rais Yoweri ataona inafaa'

Huu ni mtego kwa Yoweri akiona haifai anajinunulisha wapinzani kilazima.

Bora aone inafaa jamaa atibiwe apone.

Ila siasa za Afrika ni ngumu sana kwa mpinzani anayewaza kuchukua dola.

Kuna wapinzani hapa Tz hawawazi kuchukua dola ndiyo maana hujawahi kusikia hata kama amewahi kuliona gari la polisi lililojaa askari.
 
kila binadamu chini ya jua ni kiumbe cha mwenyezi mungu,amri kuu ya mwenyezi mungu ni kupendanda,wamefanya la maana sana hao madaktari.Uasama na chuki mwenyezi mungu amevikataa kuishi mioyoni mwa binadamu.
 
Back
Top Bottom