Chama cha mabaharia chaja juu

Hahaha hii nchi ina vituko yaani mwanataaluma mzima unajitokeza kuzungumzia hii issue
Nadhani kinachowasumbua ni kile kijulikanacho kwa Kimombo kama "Inferiority Complex ". Hii nadhani inaweza kuwaelezea kikamilifu hali zao kiuchumi etc zikoje.
 
mabaharia wa kweli hawalalamiki kimama kwa ishu ndogondogo kama hizi,kwann hata wao hujiitaga kamanda ilihali hawajawahi hata kunusa depo na afande mabeyo hajawakemea????waache ujinga,mabaharia hatupotezi muda kufatilia unlogical cases
 
Lkn vp kuhusu ile 7800 wameibariki au na yenyewe wameipinga?
 
....Madokta nao watatoa tamko karibuni... Anglizo> fani yao imeingiliwa na wanasiasa. ๐Ÿ˜‚
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Asante sana msemaji wetu sasa na sisi mabaharia tunashukuru kwa kuja mbele ya umma kutubatiza, na kuukomaza ubaharia.

Asante sana sasa na sisi kamati ndogo ya mabaharia tutakaa kutengeneza sheria zetu, na katiba yetu.
 
Asante sana msemaji wetu sasa na sisi mabaharia tunashukuru kwa kuja mbele ya umma kutubatiza, na kuukomaza ubaharia.

Asante sana sasa na sisi kamati ndogo ya mabaharia tutakaa kutengeneza sheria zetu, na katiba yetu.
 
Mnachafua dhana nzima ya mabaharia.. sisi kama mabaharia wa ukweli tunaosafiri na meli tunapinga vikali matumizi ya neno baharia kwa sababu hatuwezi kukaa kapu moja na wanaume wanao ogopa hata panya road
Sijui kama Huwa tunafikiri sawa sawa sana; Ivi ni Vitu Vidigo mno kwa ndugu zangu kuanza kuleta Complain, Mbona yako majina Mengi yanatumika na watu ambao Kiuhalisia Sio wahusika?
-Kamanda
-Ninja
-Master
-Rais (wa manzense, wasafi, wa Tanzania,etc)
-Mkuu ( mambo vipi mkuu?)
-Muheshimiwa
-Kiongozi
-Boss
-Askari ( Niaje askari wangu? wakati anayepewa hana taaluma ya Uaskari)

Yaan yako mengi ambayo yanatumika; As long as Hakuna Udhalilishaji wa Mtu husika.
Chama inabidi kijikite kuhakikisha kinaendelea kutoa Huduma Bora
Career ya Ubaharia haiwezi kupata shida kwa maneno ya watu; Kuna career zinapondwa hiyo cha Mtoto, Askari polisi, wapishi, waalimu ila bado watu ndo kwanza wanamiminika kwenye izo career.

Nadhani wao waendelee kutafsiri neno BAHARIA kama walivyozoea waachane na haya ya Mtandaoni hawataathirika kitu;
 
MWAMBIE BAHARIA WA UKWELI ASIKURUPUKE!!! hizi Zinaitwa LUGHA ZA MSIMU

Msimu ni maneno yasiyo sanifu yanayoanzishwa na kikundi cha watu wachache wenye utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi. Kwa kawaida maneno hayo huzuka na kupotea, ila yale yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha.

Chanzo

Mabadiliko ya kihistoria yanaoikumba jamii katika shughuli mbalimbali na miongoni mwa utu wa watu mbalimbali.
Kwanza ni matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii; matukio hayo yanaweza kuwa vita, njaa, ukame na kadhalika. Misimu hiyo yaweza kuwa ni ya kubeza, kusifu na kukejeli.
Ya pili ni uwepo wa matabaka, uwepo wa tofauti za kimaisha katika jamii fulani: kwa mfano, walalahoi ni maskini na magambacholi ni wenye nazo.
Ya tatu ni utani, utamaduni wa kutaniana. Jambo lingine linalosababisha kuzuka kwa misimu, msimu huu hubeba kejeli na dhihaka.
Ya nne ni maendeleo ya sayansi na teknolojia: hayo pia huwa chanzo cha misimu; vitu vipya vinavyojitokeza katika jamii vinadai uwepo wa maneno yanayozuka, kwa mfano, bajaji na digitali.

Sifa

  • 1) Huzuka na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya jamii
  • 2) Ni lugha isiyosanifiwa
  • 3) Ni lugha ya mafumbo
  • 4) Hupendwa na watu wengi kwa sababu hufurahisha
  • 5) Ni lugha inayofahamika na watu wachache
  • 6) Huwa na chumvi nyingi.

Aina za misimu

Katika misimu kuna aina tatu ambazo ni:
  • 1) Misimu ya pekee: misimu hii huelezea uhusiano wa kikundi kidogo kwenye utamaduni mmoja ambayo huweza kuwa shule moja, mtaa mmoja, ofisi moja na kadhalika.
  • 2) Misimu ya kitarafa: misimu hii huchukua eneo pana kidogo, kwa mfano kata, wilaya na hata mkoa.
  • 3) Misimu zagao: misimu hii huenea karibu nchi nzima; wakati mwingine huvuka nchi
Mimi kama baharia wa majini. Hili suala ni la msimu litatumika likiwa zuri hili neno litaingizwa kwenye maneno ya kiswahili.
 
Hawa mabaharia watakuwa na kitu "inferiority complex" kama alivyosema McCarthy pale juu; mtaani miaka nenda rudi yanatumika majina ya vyeo vya watu haijawahi tokea malalamika sembuse hii ya mabaharia

1. Kuna watu wanajiita Raisi wa Manzese n.k hujawahi sikia serikali imetoa kauli ya kukemea kwamba inadhalilisha taasisi ya Uraisi
2. Watu mtaani tukisalimiana utasikia "Niambie Shekhe au niambie Ustaadh" na wengine tunaosalimiana hvo wala sio waislam, lakini hujawahi sikia viongozi wa dini ya kiislamu wakilalamika kudhalilishwa vyeo vyao vya kidini
3. Chadema na vijana wengi mtaani wanaitana "Kamanda" lakini hujawahi sikia IGP Sirro au CDF Mabeyo au hata watangulizi wao wakikemea kuwa vyeo vya jeshi vimedhalilishwa
4. Mifano ni mingi

Hawa viongozi wa mabaharia halisi (seafarers) wangeanza kwanza kupigania stahiki na maslahi ya wanachama wao (ktk ajira zao) wangeonekana wa maana zaidi kuliko kuita press kulalamikia suala la kitoto namna hii.
 
Hakika mkuu
Sijui kama Huwa tunafikiri sawa sawa sana; Ivi ni Vitu Vidigo mno kwa ndugu zangu kuanza kuleta Complain, Mbona yako majina Mengi yanatumika na watu ambao Kiuhalisia Sio wahusika?
-Kamanda
-Ninja
-Master
-Rais (wa manzense, wasafi, wa Tanzania,etc)
-Mkuu ( mambo vipi mkuu?)
-Muheshimiwa
-Kiongozi
-Boss
-Askari ( Niaje askari wangu? wakati anayepewa hana taaluma ya Uaskari)

Yaan yako mengi ambayo yanatumika; As long as Hakuna Udhalilishaji wa Mtu husika.
Chama inabidi kijikite kuhakikisha kinaendelea kutoa Huduma Bora
Career ya Ubaharia haiwezi kupata shida kwa maneno ya watu; Kuna career zinapondwa hiyo cha Mtoto, Askari polisi, wapishi, waalimu ila bado watu ndo kwanza wanamiminika kwenye izo career.

Nadhani wao waendelee kutafsiri neno BAHARIA kama walivyozoea waachane na haya ya Mtandaoni hawataathirika kitu;
 
IMG-20190909-WA0011.jpeg
 
Back
Top Bottom