Chama cha maalbino chaendelea kumkoromea Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha maalbino chaendelea kumkoromea Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 13, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Leo asubuhi mmoja wa wajumbe wa chama cha maalbino nchini alihojiwa na TBC1 na kuendelea kushinikiza meneja wa kampeni ya Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz katika jimbo la Lindi Mjini awaombe radhi maalbino wote nchini kwa kuwadhalilisha.

  Sakata hili lilianza kutokana na kinachodaiwa Meneja huyo kudai anazo taarifa za kitaalamu zinazothibitisha ya kuwa maalbino wanapopigwa na jua huathirika kiakili na hivyo hawapaswi kuwa viongozi.

  Shutuma hii ilisadikiwa ilimlenga mualbino mmoja ambaye ni mshindani wa karibu wa Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz kupitia chama kimoja cha upinzani.

  Chama cha maalbino kilikwisha kutoa kauli ya kulaani kudhalilishwa huko lakini hadi leo si mgombea au meneja huyo ambaye amejitokeza hadharani kukiri au kukanusha tuhuma hizo za udhalilishaji wa walemavu wa ngozi.

  Tuhuma hizi ni nzito hususani tukizingatia ya kuwa wenzetu waathirika wa ngozi wamekuwa wakipatwa na suluba za kuuawa au kukatwa viungo vyao kutokana na imani za kishirikina. Sasa kuendelea kuwadhalilisha katika mazingira haya ni dhahiri ya kuwa kunawaongezea maumivu ya kunyanyapaliwa na jamii na hivyo maisha yao kuwekwa rehani na kauli ambazo ni za kiuonevu.

  katika hali ya kawaida tungelimtegema mwajiri wa kampeni meneja huyu ambaye ndiye Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz kujitokeza hadharani na kuomba msamaha au kukanusha ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki kama kumfuta kazi meneja wake ili kuonyesha anakerwa na tabia hiyo chafu dhidi ya walemavu wa ngozi.

  Uamuzi wa Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz kukaa kimya ni dhahiri ya kuwa anaunga mkono kauli za mtumishi wake na hii ni sababu tosheleza ya wapigakura kumkataa bila ya kujali ushabiki wa vyama vyao vya siasa na kumpa kura zote za ndiyo mgombea huyo wa kialbino kuonyesha mshikamano ambao wanajamii tunao na waathirika hao.
   
 2. M

  Martinez JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  huyo mtu apelekwe mahakamani, hakuna hakimu atakayemuachia. Na pia hakuna mtanzania aliyefurahishwa na kauli zake za kipumbavu, za kibaguzi, na za kishenzi. Ikumbukwe, Binadamu wote tuna haki sawa mbele ya Muumba
   
Loading...