Chama cha LDP Japan kinawakaribisha wanawake mikutanoni lakini ‘mwiko kuzungumza’

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Siku kadhaa baada ya mkuu wa michezo ya Olimpiki nchini Japani kulazimishwa kujiuzulu kwasababu ya maneno yake ya kudhalilisha wanawake, chama chake kimeamua kualika wanawake kuhudhuria mikutano muhimu - mradi tu wasiseme neno.

Chama cha Liberal Democratic (LDP) kilipendekeza wabunge wanawake washuhudie bodi ambayo ina wanaume tu namna wanavyoendesha mkutano wao.

Hawaruhusiwi kuzungumza wakati wa mkutano - lakini wanaweza kutoa maoni yao baadaye.
Wanawake nchini Japani kwa kipindi kirefu wamekuwa wakijitenga na ushiriki wa kisiasa na kiuchumi.

Nchi hiyo imeorodheshwa kuwa ya 121 kati ya nchi 153 kulingana na kipimo cha Jukwaa la Kiuchumi Duniani mwaka 2020 cha tofauti la kijinsia Duniani.

Wanawake wawili sasa hivi ndio wanaoshiriki katika bodi ya watu 12 ya chama cha LDP ambacho kimekuwa madarakani karibu kila wakati tangu mwaka 1955.

Toshihiro Nikai, 82, katibu mkuu wa chama cha LDP, amezungumza na wanahabari Jumanne kwamba anataka kukaribisha wanawake katika mkutano huo.

Alisema anafahamu ukosoaji unaoendelea dhidi ya wanaume kutawala bodi ya chama hicho na ilikuwa muhimu kwa wanachama wa kike wa chama hicho kufuatilia mchakato wa maamuzi unavyoendeshwa, alinukuliwa na shirika la habari la Reuters

"Ni muhimu kuelewa majadiliano yanavyoendelea. Kutazama na kufuatilia," alisema.

Chombo cha habari nchini Japani kimesema wanawake watano huenda wakaruhusiwa kuketi na kufuatilia mkutano wa bodi inayofanya maamuzi lakini hawataruhusiwa kuzungumza. Wanaweza kuwasilisha maoni yao baadaye kwa Sekretarieti.

Sasa hivi wanasiasa 46 kati ya 465 nchini Japani ndio waakilishi wa wanawake - hiyo ikiwa ni takriban asilimia 10 ikilinganishwa na asilimia 25 kote duniani.

Ubaguzi wa kijinsia Japani

Maoni ya Mariko Oi, BBC News
Kama mwanamke wa Kijapani, ubaguzi wa kijinsia kwa bahati mbaya ni jambo ambalo limezoeleka kwa miaka mingi. Inawezakana ukatokea katika mikutano ya kibiashara, wakati wafanyakazi wanakunywa vivywaji vyao baada ya kazi au mikutanoni. Nyakati kama hizo, wengi wetu hucheka tu na kujifanya hatukusikii kilichotokea na kusonga mbele.

Hiyo ndio sababu matamshi ya Bwana Mori hayakunishangaza, na uamuzi wa chama tawala wa kuruhusu wanawake kwenda katika mkutano wao mradi tu wasizungumze ni mbinu ambayo tunaifahamu.

Chini ya utawala uliopita wa Shinzo Abe, serikali iliweka lengo lake la kuongeza idadi ya viongozi wanawake kufikia mwaka 2020. Na baada ya kushindwa kufikia lengo hilo, taratibu ikasongeza lengo hilo kwa mwongo mmoja.

Kwa kipindi kirefu wakosoaji wamekuwa wakisema badala ya kuongeza idadi ya wanawake basi tu, kile Japani inachohitaji ni mabadiliko kuanzia elimu hadi utamaduni wa kuajiri.

Kipi kilichotokea katika mzozo wa Olimpiki?

Yoshiro Mori, 83, alisema katika majadiliano juu ya kuongeza idadi ya wanawake katika bodi, kwamba "lazima tuhakikishe muda wao wa kuzungumza unadhibitiwa - wanakuwa na wakati mgumu kumaliza mazungumzo."

Baada ya matamshi hayo kusababisha hasira miongoni mwa wananchi, alijiuzulu kwa kile kilichodaiwa ni "matamshi yasiofaa".
Wafadhili wakubwa wa mashindano ya Olimpiki ya Tokyo walikosoa matamshi hayo ikiwemo kampuni ya Toyota.

Kundi la wabunge wanawake walivaa nguo za rangi nyeupe na kufanya maandamano dhidi ya matamshi hayo na gavana wa Tokyo Yuriko Koike akasema hatahudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa maafisa wa Olimpiki.

Baadhi ya watu 400 inasemekana walifuta mambi yao ya kujitolea katika michezo ya Olimpiki, ambayo imepangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
 
Safi sana wanaongea kuliko kawaida kuna yule boss wa Olympic alijiuzulu kwa kusema wanawake wanaongea sana kwenye mikutano ya Board? Wakati alisema ukweli.

Waingie na Barakoa na marufuku kuzivua
 
Hizi habari hazina kashiko tunataka updates Nani kudondoka na covid Duniani
 
Japan ilivyo na uchumi mkubwa vile, naona sawa tu wanawake washinde jioni wakitengeneza Sushi kwa ubora zaidi. Sababu kila kitu wanachacho, na kila kitu kina utaratibu na sheria.

Sio huku kwetu, Jiwe likitikisika tu utsikia, Leo natoa bilioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa bandari hapa Dodoma, nakuagiza katibu mkuu, Leo leo fuatilia pesa na ujenzi uanze mara moja, au sio ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom