CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME CHAPIGA HODI BUNGENI"Sasa chataka kianze kutambuliwa rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME CHAPIGA HODI BUNGENI"Sasa chataka kianze kutambuliwa rasmi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cement, Jun 17, 2012.

 1. cement

  cement JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Ndugu zangu mmelalamika sana ooh mara yule mama wa Tgnt kila siku analalamika tu peke yake sasa mkae mikao ya kula kitu hicho kinakuja kwa wale ambao.......

  1.Wanaolala nje kwa kuhofia kupigwa makofi na wake zao haki yako inakuja
  2.Wanao lala mzungu wa nje kisa mama hujamletea zawadi kazi hiyo inakuja
  3.wanao pika kwa lazima na kufua haya twendeeeeeeeeee
  4.Na mengineyooooooooooo


  OFISI YA SPIKA WA BUNGE LA[/FONT]

  [FONT=&quot]JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA[/FONT]
  [FONT=&quot]S.L.P 941,[/FONT]
  [FONT=&quot]DODOMA.[/FONT]


  [FONT=&quot]Mh. Spika,[/FONT]


  [FONT=&quot]YAH: CKHWT KUOMBA KUWA WAGENI WAKO [/FONT]
  [FONT=&quot]KATIKA KIKAO KIJACHO CHA BUNGE LA JAMHURI YA [/FONT]
  [FONT=&quot]MUUNGANO WA TANZANIA[/FONT][FONT=&quot].[/FONT]

  [FONT=&quot]Rejea kichwa cha somo tajwa hapo juu,[/FONT]


  [FONT=&quot]Kwa heshima na taadhima Uongozi wa juu wa chama cha kutetea Haki za Wanaume Tanzania [ CKHWT ] umekaa na kutafakari kwa kina sana na kuona kuna umuhimu mkubwa wa kukuomba kuwa wageni wako katika kikao kijacho cha Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. [/FONT]


  [FONT=&quot]Lengo kubwa la Chama hiki ni kuomba kutambuliwa na mhimili huu muhimu katika nchi yetu kwa vile tumeona kuwa, pamoja na viongozi waasisi wa Taifa hili kufanya mambo mengi mazuri, waasisi wa chama hiki wamegundua mapungufu makubwa kuhusu haki sawa kwa wote. [/FONT]


  [FONT=&quot]Hivyo chama hiki kinaomba kuwakumbusha viongozi wetu sasa kuwa baadhi ya mambo muhimu waliyoyaweka walisahau kukumbuka “siku ya mwanaume” nchini ili Tanzania nayo sasa iweze kuonekana inamtendea haki mwanaume kwa kutomtenga katika mambo mazito ya kitaifa na kimataifa, ili kuungana na nchi nyingine Duniani kuiadhimisha siku hiyo kama ilivyo kwa Siku ya Wanawake Duniani, Siku ya Mtoto Duniani n.k. siku ambazo huadhimishwa na walengwa ili kuweza kuwa na matamko mbalimbali na kauli mbiu zinazoimarisha na kujenga umoja wa Watanzania bila kuathiri haki za Binadamu upande wowote.[/FONT]


  [FONT=&quot]Mh.Spika,[/FONT][FONT=&quot] chombo hiki kitakuwa ni chombo huru ambacho moja ya malengo yake makubwa ni kutetea Haki sawa kwa wote tofauti na ilivyo sasa ambapo zipo taasisi zinazotetea upande mmoja, jambo linaloonyesha kubaguliwa kijinsia kwa Mwanamme wa Tanzania kwa vile hana sauti ndani na nje ya mipaka ya nchi. [/FONT]


  [FONT=&quot]Mh. Spika,[/FONT][FONT=&quot] kupitia chombo hiki muhimu kwa Mwanamme wa Tanzania tunaliomba Bunge lako tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukitambua rasmi chama hiki na kwamba tunaomba sana kwa waheshimiwa wabunge wote, Serikali, waheshimiwa mabalozi wa nchi mbalimbali, taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, wafanya biashara mashuhuri akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya IPP Dr Regnald Mengi na wadau mbalimbali nchini mtuunge mkono kwa kutupa misaada mbalimbali ikiwemo majengo,fedha na vyombo mbalimbali vya usafiri ili kukiimarisha chama hiki kusaidia kuenea kwa kasi nchi nzima angalau chama hiki kiweze kuanza shughuli zake katika ngazi za Wilaya Mkoa na Taifa. [/FONT]


  [FONT=&quot]Pia tunaomba wasomi hususan vyuo vikuu nchini watusaidie kutoa michango ya maandishi itakayosaidia kuboresha katiba ya chama hiki ambayo itakuwa ni katiba Baba wa Mwanaume wa Tanzania.[/FONT]


  [FONT=&quot]Mh. Spika,[/FONT][FONT=&quot] sisi kama wadau na watetezi wa haki za binadamu ilikuwa inatupa wakati mgumu na mkanganyiko mkubwa sana hasa wakati wa kutetea Haki za Binadamu kwa vile kuna baadhi ya taasisi ndani na nje ya nchi ambazo tayari zinatetea upande mmoja na kuuacha upande wa Baba ukiwa hauna mtetezi na msimamizi wa kuhakikisha kwamba endapo mwanamme wa Tanzania hajatendewa Haki, mtetezi wa upande huo anasimamia haki ikiwemo kupewa msaada wa kisheria katika vyombo vya utoaji haki. [/FONT]


  [FONT=&quot]Mh. Spika,[/FONT][FONT=&quot] kwa namna ya kipekee tunapenda kukipongeza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kwa Ripoti yake iliyotolewa kwa waandishi wa habari na wao kuitoa kwa umma ili kuona unyanyasaji anaofanyiwa Baba licha ya kutolewa kwa matukio mbalimbali na vyombo vinavyotetea upande mmoja huku vikiacha kutoa hali halisi bila upendeleo.[/FONT]


  [FONT=&quot]Baba wa Tanzania anatambulishwa kitaifa na kimataifa kuwa ni hodari kwa ukandamizaji akitumia mfumo dume huku kukiwa hakuna chombo kinachojibu tuhuma hizi kutimiza Demokrasia ya kweli kwa wote bila kuathiri Haki za Binadamu ndani na nje ya nchi.[/FONT]


  [FONT=&quot]Mh. Spika,[/FONT][FONT=&quot] tunaomba sasa tuishie hapa ili kulipa bunge hili nafasi ya kujadili na kutoa maelekezo kwa wadau mbali mbali ili chombo hiki kiweze kuwa huru kufanya shughuli zake kwa kuwa tayari tuko katika mchakato wa kukamilisha taratibu za usajiri na kuandaa sherehe za uzinduzi utakaofanyika Mkoani Mwanza kwa kumuomba Mh waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo.[/FONT]


  [FONT=&quot]Asante kwa kukubali ombi letu.[/FONT]


  [FONT=&quot]Antony J. Sollo[/FONT]


  [FONT=&quot]………………………………………[/FONT]
  [FONT=&quot]Katibu Mkuu wa CKHWT Taifa[/FONT]
  [FONT=&quot]Nakala: [/FONT]
  [FONT=&quot]Vyombo vyote vya Habari[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wangeeleza hiyo ripoti ya LHRC imesema ni wanaume wangapi wananyanyaswa au kupigwa na wake zao, na wao wana mikakati gani kuhakikisha hilo linapungua kama si kutoweka kabisa....
  Wangeeleza sheria ambazo zinakandamiza haki za wanaume, ushawishi watakaoufanya ili bunge letu tukufu liweze kuzipitia na kuzibadilisha au kuziboresha.........

  Vinginevyo nitawaona kama waganga njaa tu..........
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,213
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Duuuh heheee! Kazi ipo!
   
 4. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Afadhali kiwepo kutetea haki za wanaume. Jamani kuta za nyumba zimeficha mengi sana, wanaume wananyanyaswa sana ila wanakufa kikondoo maana hawana pa kusemea. wanakosa unyumba, wanapigwa nk. na hakuna mtetezi, heri sasa kuna wa kuwatetea. Naunga mkono chama hiki
   
 5. cement

  cement JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Watu tunanyanyasika sana nyumba zinaficha mengi!!ahahahaaaaa
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,080
  Likes Received: 7,306
  Trophy Points: 280
  Wengine huu ni mwezi wa saba "hatujaona ndani",
  Bora hikin chama kije kitutetee.
   
 7. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi kabisa,kitatusaidia wengi
   
 8. cement

  cement JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Coz wanaume ni wasiri kutoa siri za ndani ss tutakuwa tunapishana kwenye ofisi za hiki chama!
   
 9. K

  KISWAHILI Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinatetea wanaume wa wapi?kinamtetea mwanaume kwa nani?
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Hiki chama cha kijinga, mwanaume huwa hatetewi, anajitetea. Wanavunja miiko ya uanaume. Tatizo vijana wa leo mnakula chips mayai halafu mnajiita wanaume. Ujinga mtupu.
   
 11. cement

  cement JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Majumba na fence vinaficha mengi!
   
 12. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kula 100%,hapo umenena mkuu.
   
 13. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nimepita hapa!
   
 14. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,136
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Wala sishangai! Kuna Wanaume we waone tu mjini, wakishafika nyumbani huwa wanatumwa chunvi dukani na wake zao.
   
 15. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni dalili tosha kuwa mfumo wa utawala haujali haki za watawaliwa. Hapa ndio nafasi ya Muumba inapoonekana dhahiri, bila mfumo wa aliyetuumba bila shaka maisha haya yatagubikwa na mashaka kila uchao. Baadae kutaanzishwa chama cha kutetea haki za watembea kwa miguu, waendesha magari (cha waendesha baiskeli kipo), mashoga nk nk nk

  Nina mashaka kidogo iwapo watu hawa wanaodai haki kama wameshatimiza wajibu wao ndipo wakadai haki zao, mara nyingi unapodai haki ukumbuke pia wajibu wako.

  Nawasilisha
   
Loading...