Chama cha Kisoshalisti cha Waziri mkuu, Pedro Sanchez kimeshinda katika uchaguzi mkuu wa kitaifa wa Hispania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,520
9,322
Chama cha Kisoshalisti cha Waziri mkuu, Pedro Sanchez kimeshinda katika uchaguzi mkuu wa kitaifa wa Hispania jana.

Katika uchaguzi huo wa pili katika muda wa chini ya miezi saba, chama hicho cha kinachoegemea siasa za mrengo wa kushoto kimeendelea kupata wingi wa viti katika Bunge la Kitaifa.

Huku asilimia 99.9 za kura zikiwa zimehesabiwa, chama hicho kilijinyakulia viti 120, hii ikiwa ni idadi iliyopungua viti vitatu kutoka uchaguzi uliopita wa mwezi Aprili lakini pia vikiwa pungu ya kiwango cha viti 176 vinavyohitajika ili kiweze kuunda serikali peke yake.

Uchaguzi huo umerudiwa ili kujaribu kumaliza mkwamo wa kisiasa nchini humo baada ya Sanchez, licha ya kushinda katika uchaguzi wa Aprili, kushindwa kuunda Serikali.

Takriban wapiga kura milioni 37 walipiga kura Jumapili kuchagua Nunge jipya wakiwa na matarajio kwamba chama cha Sanchez kingeshinda, lakini pia kwamba asingepata wingi wa kutosha bungeni kumwezesha kuunda serikali.
 
Back
Top Bottom