Chama cha Kijamii (CCK) wapanga kufanya mkutano mkuu Ikulu

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
4,582
Points
2,000

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
4,582 2,000


Dar es Salaam. Chama cha Kijamii (CCK) kinajiandaa kufanya mkutano wake mkuu mapema mwakani katika ofisi ya Rais, Ikulu ya Dar es Salaam. Mpango huo umetangazwa na mwenyekiti wa chama hicho, Constantine Akitanda ikiwa ni siku chache baada ya Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kuvialika vyama vya upinzani kufanya mikutano yake Ikulu kama chama hicho kinavyofanya baadhi ya mikutano yake.

Kauli ya Rais Magufuli ilikuja huku kukiwa na malalamiko ya baadhi ya vyama vya siasa ikiwemo Chadema vikisema CCM imekiuka Sheria ya Vyama vya Siasa inayokataza vyama vya siasa kutumia rasilimali za Serikali kwa manufaa yake.

Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Rais Magufuli alisema: “Nawakaribisha sana hapa Ikulu hapa ni kwenu. Bila ninyi mimi nisingekuwa hapa. Kwahiyo sioni aibu kuwakaribisha wana CCM, lakini pia hapa ni kwa Watanzania wote, na ndio maana kuna wageni kutoka nje wamefika hapa Ikulu, wanamuziki niliwakaribisha Ikulu, wakati wa futari tulifanyia hapa hapa.

“Kwahiyo sioni ajabu ninyi kuwakaribisha hapa. Halafu kuona watu wajiulize kwanini mikutano wanafanyia Ikulu,” alisema Rais Magufuli. Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili leo Jumanne, Mwenyekiti wa CCK, Akitanda amesema wameipokea kauli hiyo ya Rais na wataitekeleza kwa kufanya mkutano wao mkuu mapema mwakani.

Amesema awali walipanga kufanyia kikao cha Kamati Kuu Ikulu, lakini wameona wasogeze mbele ili wafanye mkutano mkuu Februari mwakani. Tunataka kutumia ukumbi wa Ikulu kama alivyoelekeza Rais, maana ni ukumbi wa wananchi wote,” amesema Akitanda.

Aliongeza: “Tulitaka tuombe ukumbi wa Ikulu kwa ajili kikao cha Kamati Kuu wiki ijayo, lakini tukaona kikao hicho kitakuwa na wajumbe wachache tu yaani 30, sasa tunajipanga kufanya mkutano mkuu utakaokuwa na wajumbe 500 maana ule ukumbi ni mkubwa sana. Ameongeza pia sababu za kusogeza mbele mkutano wao ni barua waliyopokea kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ikiwataka wauandae mkutano huo kwa miezi minne.

“Chama kimepokea barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo inatuelekeza kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu ndani ya miezi minne, nadhani kuanzia mwezi huu itakuwa Februari mwakani,” amesema Akitanda. “Katiba yetu inasema Mkutano Mkuu utakuwa na wajumbe 500, lakini hata wakiwepo nusu yake wanaweza kufanya uamuzi. Tunaamini kabisa Rais atatukubalia kufanyia mkutano Ikulu, akikataa basi tutajua kwamba hatufai, lakini hatutarajii kukataliwa,” ameongeza.

Amesema kabla ya mkutano huo, kutakuwa na vikao vya utangulizi vitatu ambavyo ni pamoja na kamati ya utendaji, sekretarieti na mwisho Kamati Kuu ambayo itapendekeza tarehe ya Mkutano Mkuu.
 

kivava

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Messages
5,794
Points
2,000

kivava

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2013
5,794 2,000
Wanatafuta njia kuhalalisha maccm kutumia gharama za serikali
Muda utasikia Mrema Cheyo,Shibuda na Lipumba nao wamefanya vikao Ikulu
Komedi ya kijinga sana
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
12,056
Points
2,000

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
12,056 2,000
CCJ to CCK naona mzimu umefufuka. Marehemu Sitta kafariki bila kutufumbulia hili fumbo,anyway kuna Mwakyembe,Mpendabure ooh sorry Mpendazoe na Bashite watuweke.sawa
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Messages
8,255
Points
2,000

ushuzi.1

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2015
8,255 2,000
Wanatafuta njia kuhalalisha maccm kutumia gharama za serikali
Muda utasikia Mrema Cheyo,Shibuda na Lipumba nao wamefanya vikao Ikulu
Komedi ya kijinga sana
Hivyo vizee vitatu Cheyo, Mrema na Dovutwa si vipinzani tena vimekuwa vidalali vya Siasa kama Lipumba anavyokula pesa za magufuli na CCM kiulaini huku akilindwa na walinzi wanaolipwa mishahara na walipa kodi.
 

Forum statistics

Threads 1,364,841
Members 521,025
Posts 33,330,163
Top