Chama cha Jubilee chazima jaribio la Rutto kutaka kuchukua madaraka kwa nguvu, chapendekeza afurushwe toka Jubilee

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,613

MY TAKE: Dunia ya samaki Kambare hii, kila mtu hadi watoto wameota ndevu, Hakuna law and order, fujo kwa kwenda mbele.

======

Chama tawala cha Jubilee nchini Kenya kimependekeza kuondolewa kwa naibu wa rais Willima Ruto kutoka kwa wadhfa wake kama naibu kiongozi wa chama hicho.

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amemshutumu bwana Ruto kwa kuwa 'mjeuri, mwenye madharau na asiyemheshimu Rais Uhuru Kenyatta".

Je katibu mkuu wa Jubilee amesema nini
Taarifa iliosomwa hii leo imezungumzia kuhusu matusi ya hivi karibuni yaliotolewa na wandani wa naibu huyo wa rais yakimlenga mamake Uhuru {seneta mmoja tayari ameshtakia kwa kutoa matamshi ya chuki} walipokuwa wakimuunga mgombea wao katika uchaguzi wa marudio ambapo chama hicho kilikuwa kimeamua kutowakilishwa mbali na kutokuwepo kwa naibu huyo wa rais katika mkutano wa Jumatatu kuhusu corona wakati abapo rais alilegeza baadhi ya masharti ya kukabiliana na ugonja huo.

Kiti chake kilikuwa kimehifadhiwa katika mkutano huo. Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya naibu huyo wa rais kutembelea makao makuu ya chama hicho na zaidi ya wabunge 35 wanaounga mkono ugombea wake wa urais.

Chama hicho kimeshtumu kwa kujaribu kfanya mapinduzi huku rais akiwa Ufaransa . hapo Jana bwana Ruto alijibu katika mtandao wake wa twitter kwamba ameshangaa kwamba ziara yake ya makao makuu ya cham hicho cha Jubilee ilikuwa habari kuu.

Uongozi wa chama hicho hivi sasa umesema kwamba hautamruhusu kuingia katika makao hayo, ukisema kwamba hautamruhusu kuendesha kampeni zake za urais kutoka katika afisi hiyo ili kuwatishia wapinzani wake.

Je wandani wa Ruto wamejibu vipi?
Lakini wakiongea katika hafla moja mjini Nakuru, Magharibi mwa Kenya, ambayo pia ilihudhuriwa na makamu wa rais William, Ruto, Wabunge kadhaa na maseneta, wamekashifu tangazo hilo la bwana Tuju, huku wakisema kuwa, kama kaimu katibu mkuu wa chama Tuju hana mamlaka hayo na kuwa ofizi za kitaifa za chama ni za wanachama wote.

Bwana Ruto ameanza kufanya kampeni zake za kuwania urais 2022.

Rais Kenyatta amesisitiza kwamba sasa sio muda wa kufanya kampeni na badala yake kutimiza walichoahidi Wakenya.

Hapo jana katika mahojiano na chombo cha habari cha France21, rais Uhuru Kenyatta alikataa kusema iwapo atamuunga mkono William Ruto katika kiny'anga'nyiro cha urais na kusema kuwa lengo lake sasa ni kuwaleta Wakenya pamoja.

Rais Kenyatta ameungana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika mradi kwa jina BBI , ambao wanasema unalenga kumaliza hali ya kuwa msimamizi wa kila kitu kwa kila anayeunda serikali.

Mradi wa BBI una jopo linalolenga kubadilisha katiba na kufanyika kwa kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa 2022 . Bwana Ruto anapinga mradi huo.

BBC Swahili
 
Hustler nation. Hustler the 5th wapende wasipendeee.

Jayden awe makini anaweza asirudi, hili nasikitika kwa hawa jirani zetu.
 
Hahah kuna kina MK254 ambao wanamshabikia Tundu kuwa presdaa, hakuwafanyi kuwa watanzania.

Mimi ni mtanzania 100%. Bantugbro The best 007
Jirani mwenye busara hapaswi kuegemea upande mmoja katika malumbano ya jirani yako, kumbuka sisi Tanzania ndio kimbilio la majirani kwa ajili ya kuwasuluhisha, sasa huoni ukilalia upande mmoja unapoteza sifa ya kuwa jirani mwema?

Hao wakenya uliowataja, tuliwakumbusha kwamba sio jambo la busara kushabikia upande mmoja katika siasa za Tanzania, ninadhani walielewa.
 
MY TAKE: Dunia ya samaki Kambare hii, kila mtu hadi watoto wameota ndevu, Hakuna law and order, fujo kwa kwenda mbele.

======

Chama tawala cha Jubilee nchini Kenya kimependekeza kuondolewa kwa naibu wa rais Willima Ruto kutoka kwa wadhfa wake kama naibu kiongozi wa chama hicho.

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amemshutumu bwana Ruto kwa kuwa 'mjeuri, mwenye madharau na asiyemheshimu Rais Uhuru Kenyatta".

Je katibu mkuu wa Jubilee amesema nini
Taarifa iliosomwa hii leo imezungumzia kuhusu matusi ya hivi karibuni yaliotolewa na wandani wa naibu huyo wa rais yakimlenga mamake Uhuru {seneta mmoja tayari ameshtakia kwa kutoa matamshi ya chuki} walipokuwa wakimuunga mgombea wao katika uchaguzi wa marudio ambapo chama hicho kilikuwa kimeamua kutowakilishwa mbali na kutokuwepo kwa naibu huyo wa rais katika mkutano wa Jumatatu kuhusu corona wakati abapo rais alilegeza baadhi ya masharti ya kukabiliana na ugonja huo.

Kiti chake kilikuwa kimehifadhiwa katika mkutano huo. Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya naibu huyo wa rais kutembelea makao makuu ya chama hicho na zaidi ya wabunge 35 wanaounga mkono ugombea wake wa urais.

Chama hicho kimeshtumu kwa kujaribu kfanya mapinduzi huku rais akiwa Ufaransa . hapo Jana bwana Ruto alijibu katika mtandao wake wa twitter kwamba ameshangaa kwamba ziara yake ya makao makuu ya cham hicho cha Jubilee ilikuwa habari kuu.

Uongozi wa chama hicho hivi sasa umesema kwamba hautamruhusu kuingia katika makao hayo, ukisema kwamba hautamruhusu kuendesha kampeni zake za urais kutoka katika afisi hiyo ili kuwatishia wapinzani wake.

Je wandani wa Ruto wamejibu vipi?
Lakini wakiongea katika hafla moja mjini Nakuru, Magharibi mwa Kenya, ambayo pia ilihudhuriwa na makamu wa rais William, Ruto, Wabunge kadhaa na maseneta, wamekashifu tangazo hilo la bwana Tuju, huku wakisema kuwa, kama kaimu katibu mkuu wa chama Tuju hana mamlaka hayo na kuwa ofizi za kitaifa za chama ni za wanachama wote.

Bwana Ruto ameanza kufanya kampeni zake za kuwania urais 2022.

Rais Kenyatta amesisitiza kwamba sasa sio muda wa kufanya kampeni na badala yake kutimiza walichoahidi Wakenya.

Hapo jana katika mahojiano na chombo cha habari cha France21, rais Uhuru Kenyatta alikataa kusema iwapo atamuunga mkono William Ruto katika kiny'anga'nyiro cha urais na kusema kuwa lengo lake sasa ni kuwaleta Wakenya pamoja.

Rais Kenyatta ameungana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika mradi kwa jina BBI , ambao wanasema unalenga kumaliza hali ya kuwa msimamizi wa kila kitu kwa kila anayeunda serikali.

Mradi wa BBI una jopo linalolenga kubadilisha katiba na kufanyika kwa kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa 2022 . Bwana Ruto anapinga mradi huo.

BBC Swahili

Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
 
Kilimchotokea Lowassa ndicho kitamtokea Ruto.

Rais ajaye wa kenya atakuwa yule ambaye hategemewi kabisa
Rais wa Kenya ni yule atakayekubalika na kuungwa mkono na wakikuyu, Wakikuyu wanasema wao ndio waluopigana vita vya Mau mau na kuikomboa Kenya wakati kabila zingine zilikua zinawasaidia waingereza.

Kwa ujumla Kenya ni nchi ya wakikuyu, wakikukataa huwezi kuwa rais wa Kenya hata siku moja, ndio wenye "total control of economy and politics of Kenya".
 
Back
Top Bottom