Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuunda Serikali za Mitaa zisizo na ofisi

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,177
Leo tar 13/11/2019 kulikua na vikao kati ya wanachama wa Chama tajwa katika kata mbali mbali za wilaya ya mbarali na ujumbe toka mkoani Mbeya.

Ujumbe ulikuwa unasisitiza kuwa licha ya jimbo la mbarali kutokukumbwa na kadhia ya kuenguliwa wagombea wanatakiwa kususia. Ujumbe huo umesisitiza kuwa huo ndio msimamo wa chama kitaifa.

Suala la mkutano sio habari lakini habari yenyewe ni juu ya muundo wa serikali.
Viongozi hao wamesema kuwa wagombea wanaosusia ndio viongozi wa wanachama wao. Yaani hao ndio watatangaza michango, mikutano ya vijiji na kususia michango, mikutano na kutowatambua viongozi watakaopita bila kupingwa kwenye vijiji vyao.

Yaani kwa lugha nyingine ni kuwa itakuwa ni serikali isiyo na ofisi. Na kutokana na madiwani wa baadhi ya kata husika kutoka chama hicho wamepewa kazi ya kusimamia kidete msimamo huo na kuwakingia kifua wanachama wakikutwa na masahibu pindi wakigomea michango.

Hivi ndio msimamo wa kitaifa au ni huku Mbeya tu?
 
Mooooo.
97596_special_cars_jpg95b1b2c9aaf3c0b02ff5ee1f4748e78b.jpeg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom