Chama cha CUF: Buriani Maalim Seif Shariff Hamad

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
TAARIFA KWA UMMA

NI MSIBA MZITO SANA! BURIANI MAALIM SEIF

The Civic United Front CUF- Chama Cha Wananchi kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa sana Taarifa ya Kifo Cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT-WAZALENDO Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad kilichotangazwa leo Jumatano Februari 17, 2021 saa 07: 00 mchana na Dr. Husein Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar.

CUF- Chama Cha Wananchi kinamtambua Marehemu Maalim Seif Shariff Hamad kama Muassi na miogoni mwa Viongozi Wakuu wa Chama cha CUF kiliposajiliwa mwaka 1993. Maalim Seif alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa CUF na kushika wadhifa huo mwaka 1993 – 1999. Mwaka 1999 nilipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Maalim Seif alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu. Amefanya kazi ya Katibu Mkuu wa CUF mpaka Machi 2019 alipohamia ACT-WAZALENDO.

Maalim Seif alikuwa Makamu wa Kwanza wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015.

Wakati wa Mfumo wa Chama kimoja mwanzoni mwa miaka ya 1980, Maalim Seif alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Mjumbe wa Sekretariati ya CCM akiongoza Idara ya Uchumi.

Binafsi nilikutana na Maalim Seif kwa mara ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1973. Wakati huo yeye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala mimi nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Idara ya Uchumi. Tukiwa Chuo Kikuu, Maalim Seif alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Muslim Students Association of University of Dar es Salaam (MSAUD) mimi nikiwa Mweka Hazina wa Umoja huo. Pia tulishirikiana katika shughuli za kiuongozi wa wanafunzi wakati akiwa Kiongozi wa Wanafunzi wa Zanzibar na mimi nikiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Maalim Seif alikuwa mwanafunzi bora mwenye kipaji cha juu. Mwaka 1975 aliongoza katika Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala kwa kupata Shahada ya Kwanza ya daraja la juu. B.A. (Hon) First Class. Chuo Kikuu kilijaribu kumshawishi abakie kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu. Hata hivyo aliitikia wito wa kurudi Zanzibar na kufanya kazi kama Katibu na Msaidizi wa Rais Aboud Jumbe.

Maalim Seif ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kisiasa na kijamii. Alikuwa Waziri wa Elimu wa Zanzibar, Waziri Kiongozi wakati wa mabadiliko ya sera za Uchumi za Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi 1984-85, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar 2010 – 15 na 2020 mpaka alipofariki.

Kwa hakika Taifa limepoteza Mwanasiasa Mahiri ambaye itakuwa ni vigumu sana kumsahau katika Siasa za nchi hii, hususan kwa Zanzibar. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na amuepushe na Adhabu zake na amthibitishe kuwa ni Mja wa Peponi.

CUF- Chama Cha Wananchi kinatoa Salamu za Pole kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi; Kiongozi wa ACT-Wazalendo Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Maalim Seif kufuatia Msiba huu mzito.

Kufuatia Msiba huu Mkubwa bendera za CUF- Chama Cha Wananchi zitapepea nusu mlingoti kwa muda wa siku saba (7) kuanzia leo Jumatano Februari 17, 2021.

CUF- Chama Cha Wananchi kinawaombea Subira Njema wale wote waliokutwa na Msiba huu mzito.

Hakika sisi sote ni wa Allah na kwa Hakika sote tunarejea kwake!

HAKI SAWA KWA WOTE!

Prof. Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti - Taifa
CUF- Chama Cha Wananchi
Februari 17, 2021
 
R.I.P
 
Amekwenda kukutana na Alhaji Jumbe, naona watabadilishana notes.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom