Kitwa-Mulomoni
JF-Expert Member
- Oct 25, 2016
- 1,779
- 1,119
Malalamiko yako hayo ukiwaelezea wapiga kura kwenye kampaini ni % ndogo sana yao watakaokuelewa na kuamua kukupa kura ya ndiyo! Ni kama 2%! Maana yake CCM itakuwa inaongoza kwa 98%. Hivyo nakushauri haya mambo mnayoyasema kila kukicha yanaboa, tafuta habari mpya zitakazo weza kuipiku CCM kwa wakati huu. Kama mmeishiwa point, jiungeni CCM ieleweke.Kuna haja gani ya kushiriki uchaguzi wakati CCM wamejipitisha bila kupingwa, wakati mgombea akiteuliwa bila kupingwa ina maana hakuna uchaguzi.
Kuna hivyo vyama vya kipuuzi eti vimesema vinashiriki, wakati havijaweka mgombea hata mmoja, na wala havina hata muwakilishi mmoja bungeni. Ni wapuuzi waliobobea.
Siku za CCM zinahesabika, muda si mrefu wataangukia pua.
1) Ubaguzi/Uonevu/Uadui/Mgawanyiko wa "WANA CCM KWA WANA CCM" ndani ya chama chao (LUMUMBA) haujakwisha bado.
2) Uadui kwa vyama vya upinzani umezidi.
3) Uadui kwa raia umezidi mara 100.
4) Wafanyakazi wa umma toka 2015 - leo hawajaongezewa hata sh100 katika mishahara (licha ya ahadi wanazopewa).
5) Ufsadi wa Sh Trillioni 1.5, na Sh Trillioni 2.0 - Za Prof Assad CAG.
6) Ufisadi wa ununuz wa ndege kwa bei "MARA MBILI".
7) Utekwaji/Kupotea/Kuuliwa kwa raia.
8) Uonevu wa kufunga watu/viongozi wa upinzani gerezani bila sababu.
9) Uminywaji wa wanahabari/vyombo vya habari.
10) Ubakwaji wa demokrasia (RAPE OF DEMOCRACY).
11) Ajira/Biashara kufa kifo cha mende.
12) DPP na TRAFICK POLICE kugeuzwa TRA (Wakusanya mapato).
13) Mauwaji ya kibiti (watu wasiojulikana).
14) Watu wasiojulikana.
15) Uongo uliokithiri kutoka kwa viongozi kwa raia.
16) Figisu kwa CAG (Mtetezi wa kodi za raia)
17) Bunge kua dhaifu.
18) Kupigwa marufuku kwa wapinzani kufanya vikao/kampeni (wakati CCM wamefanya kampeni na vikao kuanzia 2015 mpaka sasa)
19) Kufukuza/Kwaonea/Kuwadhalilisha "WAFANYAKAZI WA UMMA" mbele ya hadhara bila hata kuwapa haki ya kwasikiliza (Kwa kutafuta sifa).
Na mengine mengi. . . . . . .