Chama cha ACT - Wazalendo chajiondoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Tatizo vyama vingine navyo vingetakiwanao wawe na msimamo huo ili zoezi la uandikishaji lirudiwe upya
 
Ni Jambo la busara walilo amua ili uchaguzi usiwepo ili tuwajue watakaoshangilia ujinga Hulu mtaani tuanze na vichwa vyao
 
Kufuatana na matikeo ya utafiti wa TWAWEZA, CCM imrjaa watu wajinga, wenye elimu na upeo mdogo. Kwa nini watu wenye uelewa na akili nzuri tukubali kuyumbishwa na kunyanyaswa na wwtu wajinga?

Tushikamane, tusipoteze wakati, tuwagomee wajinga wenye upeo mdogo kwa kutumia akili na uelewa wetu. Siyo lazima kuingia katika mapigano au kufanya maandamano.

Tutumie akili na uelewa wetu kulidhibiti hili kundi la wajinga.

Kuanzia sasa, hawa wajinga watengwe katika kila kitu - kuanzia mashirikiano ya kijamii mpaka kiuchumi.
 
Huu ni uamuzi mzuri na wa busara
Uzuri wa uamuzi huu unawaongezea credibility na kukubalika kwa wananchi zaidi maana wananchi wanaona namna gani serikali ya CCM inavyotawala kwa ridhaa ya Mitutu ya bunduki badala ya chaguzi halali
 
Hayo yametangazwa na kiongozi wa chama hicho Mh Zitto Kabwe.

ACT WAZALENDO CHAIFUATA CHADEMA, CHAJITOA KUSHIRIKI UCHAGUZI. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza kuwa chama hicho kimejitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa sababu kuwa wagombea wa chama hicho wengi wameenguliwa.
View attachment 1257821
ACT-WAZALENDO IMEJIONDOA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA:

MILANGO YA DEMOKRASIA IMEFUNGWA: TUSILAUMIANE

MSIMAMO WA ACT WAZALENDO KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI WA NOVEMBA 24, 2019:

Chama cha ACT Wazalendo, kikiwa Chama cha siasa makini chenye usajili wa kudumu nchini, kiliitikia wito wa kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliokuwa ufanyike tarehe 24 Novemba 2019, tukiamini kuwa ni nafasi nyeti ya kuimarisha ushindani wa kisiasa nchini.

Licha ya miaka minne ya changamoto kubwa, na licha ya wananchi wengi kutuonya mapema kuwa hapatakuwa na Uchaguzi wa Haki, bado tuliamua kushiriki kikamilifu tukiamini kuwa taratibu, sheria na Katiba ya nchi itaheshimiwa na wahusika wote wa mchakato huu.

Wanachama wetu 173,593 walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kwa kujaza fomu za uteuzi na kuzirejesha na wengine wengi kwa maelfu walikataliwa kupewa fomu na au ofisi kufungwa kwa wakati wote. Wagombea Uenyekiti wa Mitaa walikuwa 2,481 kati ya Mitaa yote 4,264 nchini, Uenyekiti wa Vijiji walikuwa 8,218 katika ya Vijiji vyote 12,316 nchini, na uenyekiti wa Vitongoji walikuwa 35,457 kati ya Vitongoji vyote 64,384 nchini. Kwa upande wa Wagombea wa nafasi za Ujumbe wa Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mtaa (wajumbe wa kawaida na wajumbe Wanawake) wanaACT 135,675 walijitokeza kuomba nafasi hizo.

Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.

Sababu zote zilizotolewa na Serikali na Chama cha Mapinduzi kuondoa wanachama wetu katika kinyanganyiro cha Uchaguzi hatukubaliani nazo. Kamati ya Uongozi ya Chama taifa iliyoketi leo imeelekeza kuwa wanachama wetu wote waliobakizwa katika Uchaguzi WAJIONDOE katika Uchaguzi huo kwani kushiriki kwao ni kuhalalisha ubakaji wa Demokrasia uliofanywa na Serikali. Kwani kwa uenguaji huu wa wagombea kwa kutumia sababu zisizo na mantiki, si tu wamenyima wagombea wetu haki yao kikatiba, bali wamewanyima Wananchi wote wa Tanzania waliotimiza miaka 18 na zaidi haki yao, iliyopo katika Ibara ya 5 ya Katiba, ya kupiga kura. KWA KUWA CCM IMEONDOA WAGOMBEA WETU asilimia 96%, na sisi TUMEWASAIDIA KUONDOA asilimia 4% ya WALIOBAKIA.

Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa inaona kuwa Dola imeshatuamulia vyama makini vya upinzani tusishiriki kwenye uchaguzi huu. Hawataki ushindani. Wanaogopa ushindani. Wanaogopa sanduku la kura. Wanawaogopa Watanzania. Kwa msingi huo, Kamati ya Uongozi inaona hakuna mantiki ya kushiriki uchafuzi ambao asilimia 96 ya wagombea wetu wameenguliwa. Unashiriki vipi uchaguzi ambao wagombea wako wameondolewa? Kamati ya Uongozi imeamua kuwaachia CCM uchafuzi wao na kwa hivyo ACT - Wazalendo inajiondoa kwenye uchafuzi huo.

Mwaka jana mwishoni, baada ya majadiliano marefu na wenzetu katika Upinzani, tulipitisha na kulitangza Azimio la Zanzibar, ambalo liliutangaza mwaka 2019 kuwa ni “MWAKA WA KUDAI DEMOKRASIA”, mwaka ambao tungepambana kuzidai haki zetu zote tunazonyimwa kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujalitekeleza hilo, kwa matendo ya sasa ya CCM na Serikali, tumepewa nafasi ya kutekeleza Azimio la Zanzibar. ACT-Wazalendo tutakwenda kwa wenzetu wa Upinzani, ili kurudi kutekeleza Azimio la Zanzibar.

TUNAWAPA ARI wanachama na wafuasi wetu, pamoja na wananchi wote kwa ujumla, wakati ni sasa wa kuondoa hofu, kushikamana nasi katika kulinda Demokrasia ya nchi yetu. Hatupaswi kuwa waoga, hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja mmoja na kama KUNDI ZIMA LA KIJAMII.

Tumejitahidi kufuata njia zote za kisheria Lakini CCM na Serikali yake wameamua vinginevyo kwa kutuondoa katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Tumeamua kutafuta njia nyingine za kulinda demokrasia yetu. TUSILAUMIANE.

Mwisho; Kumekuwepo na vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na watendaji wa Serikali kuwabughudhi Wagombea wetu, wanachama na viongozi wetu maeneo mbalimbali nchini. Serikali ya Rais Magufuli isitufikishe kuvuka mstari wa Uvumilivu.

Kabwe Z, Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Dar es Salaam.

Novemba 8, 2019
Hongera sana Kiongozi kwa uamuzi wa busara kupika Machafuko
 
Acha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao

Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama

State agent
We dogo, Hata ndugu yenu lipumba kawananga kuwakataa sembuse zito, hamkujipanga kumwaga mihela kama wakati ule wa kuunga juhudi,

Hao ccm B mmeishawaonjesha mibulubgutu safari hii wamewagomea
 
Ubakaji wa demokrasia nchini lazima ulaaniwe. Hongera ACT tupo pamoja nanyi.
 
Watakaopata taarifa kuhusu vyama vingne vivyobaki basi watujuze hapa
 
Kanuni ya kusamehe ni kusahau Makosa au Ubaya aliokufanyia Binadamu mwenzio ,ukiona bado inauma Moyoni jua hukusamehe kwa Dhati Mkuu.
Hahah nakubaliana na wewe mkuu,kinyongo kiko palepale.
 
Huu ni uamuzi mzuri na wa busara
Uzuri wa uamuzi huu unawaongezea credibility na kukubalika kwa wananchi zaidi maana wananchi wanaona namna gani serikali ya CCM inavyotawala kwa ridhaa ya Mitutu ya bunduki badala ya chaguzi halali
Nawaza kama watatangaza maandamo tarehe hiyo ya uchaguzi, kutafanyika kweli Huo uchaguzi?
 
Acha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao

Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama

State agent

Waweke poll wasiweke, hakuna mtu yoyote wa ACT anayejitambua atashiriki huo uchaguzi wa kishenzi hata viongozi wa juu wakisema watashiriki. Ukweli ni huu, hata Zitto ili aweze kupata support ya wapinzani, hana budi kufuata njia ya cdm kwani ndio hasa wapiga kura za upinzani walipo kwa huku bara. Kwa tangazo la cdm kususia huo uchaguzi ni kama wameshafanya huo uchaguzi kuexpire. Kubali kataa lakini habari ndio hiyo.

Muambieni jiwe hana mvuto wa siasa, hata angejenga mabomba ya maziwa nchi nzima, bado hana mvuto. Fanyeni uchaguzi na hao akina Dovutwa lakini ccm ni chama analogue hakipendwi na vijana digital. Hampendwi hata mkilazimisha.
 
Ipitishwe sheria

Chama kikisusia Uchaguzi kinafutwa kabisa

Msisubiri hata hiyo sheria, vifuteni hata jioni hii, lakini ccm ni chama outdated hakina mvuto tena. Mwanamke mzee hata ajipambe na kuwa na hela, bado vijana watafuata hela zake tu lakini hawawezi kumpenda. Hata mkitangaza chama kimoja cha siasa, bado ccm haitapendwa na wananchi maana watu wameshakinai. Msitumie nguvu kubwa kulazimisha kukaa madarakani, nature hairuhusu ccm kuendelea kupendwa na kizazi cha sasa. Sio kwamba ccm haijafanya kitu wala Magufuli hajafanya kitu, bali nature ndio ilivyo, watu wakichoka wamechoka tu.
 
bado NCCR nao watoe dira yao

Hata hao NCCR wasilazimishwe waachwe waamue wenyewe, lakini wananchi wameshasusia huo uchaguzi, hata wakishiriki hawatakuwa na mtu wa kuwapigia kura. Huwa uchaguzi umeshatiwa najisi, hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu atashiriki huo ushenzi.
 
November 8, 2019

Tamko kuhusu mwenendo wa TAMISEMI na CCM kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji mwaka huu 2019



Source: MCL Digital
ACT- Wazalendo wajitoa kushiriki uchaguzi Serikali za mitaa
Friday November 8 2019
Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

BY Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mhama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Dar es Salaam.
Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Kamati ya uongozi ya chama hicho imewaagiza wagombea wake 173,593 kutoshiriki uchaguzi huo.

Kati ya wagombea 173,573 waliochukua fomu za uteuzi na kurejesha, wagombea 6,944 ndio waliopitishwa sawa na asilimia nne huku 166,649 wakienguliwa.

Uamuzi wa ACT- Wazalendo umekuja ikiwa imepita siku moja tangu Chadema kutangaza kujitoa kushiriki uchaguzi huo kutokana na figisufigisu zilizofanyika katika uchukuaji, urejeshaji wa fomu za kugombea na uteuzi wa wagombea.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 8, 2019 kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema sababu kubwa ya kutoshiriki ni namna wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walivyowaengua wagombea wa chama hicho.
Source: www.mwananchi.co.tz
 
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP na CUF zitatoa ushindani sasa

Huyo Zitto kule kigoma wanasema hata Hawataki kumwona,
Wanasema hawakumpigia kura ili akatukane Rais kipenzi cha Watanzania
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom