Uchaguzi 2019 Chama cha ACT - Wazalendo chajiondoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
65,450
Points
2,000

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
65,450 2,000
Hayo yametangazwa na kiongozi wa chama hicho Mh Zitto Kabwe.

ACT WAZALENDO CHAIFUATA CHADEMA, CHAJITOA KUSHIRIKI UCHAGUZI. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza kuwa chama hicho kimejitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa sababu kuwa wagombea wa chama hicho wengi wameenguliwa.
1573221842233.png

ACT-WAZALENDO IMEJIONDOA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA:

MILANGO YA DEMOKRASIA IMEFUNGWA: TUSILAUMIANE

MSIMAMO WA ACT WAZALENDO KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI WA NOVEMBA 24, 2019:

Chama cha ACT Wazalendo, kikiwa Chama cha siasa makini chenye usajili wa kudumu nchini, kiliitikia wito wa kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliokuwa ufanyike tarehe 24 Novemba 2019, tukiamini kuwa ni nafasi nyeti ya kuimarisha ushindani wa kisiasa nchini.

Licha ya miaka minne ya changamoto kubwa, na licha ya wananchi wengi kutuonya mapema kuwa hapatakuwa na Uchaguzi wa Haki, bado tuliamua kushiriki kikamilifu tukiamini kuwa taratibu, sheria na Katiba ya nchi itaheshimiwa na wahusika wote wa mchakato huu.

Wanachama wetu 173,593 walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kwa kujaza fomu za uteuzi na kuzirejesha na wengine wengi kwa maelfu walikataliwa kupewa fomu na au ofisi kufungwa kwa wakati wote. Wagombea Uenyekiti wa Mitaa walikuwa 2,481 kati ya Mitaa yote 4,264 nchini, Uenyekiti wa Vijiji walikuwa 8,218 katika ya Vijiji vyote 12,316 nchini, na uenyekiti wa Vitongoji walikuwa 35,457 kati ya Vitongoji vyote 64,384 nchini. Kwa upande wa Wagombea wa nafasi za Ujumbe wa Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mtaa (wajumbe wa kawaida na wajumbe Wanawake) wanaACT 135,675 walijitokeza kuomba nafasi hizo.

Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.

Sababu zote zilizotolewa na Serikali na Chama cha Mapinduzi kuondoa wanachama wetu katika kinyanganyiro cha Uchaguzi hatukubaliani nazo. Kamati ya Uongozi ya Chama taifa iliyoketi leo imeelekeza kuwa wanachama wetu wote waliobakizwa katika Uchaguzi WAJIONDOE katika Uchaguzi huo kwani kushiriki kwao ni kuhalalisha ubakaji wa Demokrasia uliofanywa na Serikali. Kwani kwa uenguaji huu wa wagombea kwa kutumia sababu zisizo na mantiki, si tu wamenyima wagombea wetu haki yao kikatiba, bali wamewanyima Wananchi wote wa Tanzania waliotimiza miaka 18 na zaidi haki yao, iliyopo katika Ibara ya 5 ya Katiba, ya kupiga kura. KWA KUWA CCM IMEONDOA WAGOMBEA WETU asilimia 96%, na sisi TUMEWASAIDIA KUONDOA asilimia 4% ya WALIOBAKIA.

Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa inaona kuwa Dola imeshatuamulia vyama makini vya upinzani tusishiriki kwenye uchaguzi huu. Hawataki ushindani. Wanaogopa ushindani. Wanaogopa sanduku la kura. Wanawaogopa Watanzania. Kwa msingi huo, Kamati ya Uongozi inaona hakuna mantiki ya kushiriki uchafuzi ambao asilimia 96 ya wagombea wetu wameenguliwa. Unashiriki vipi uchaguzi ambao wagombea wako wameondolewa? Kamati ya Uongozi imeamua kuwaachia CCM uchafuzi wao na kwa hivyo ACT - Wazalendo inajiondoa kwenye uchafuzi huo.

Mwaka jana mwishoni, baada ya majadiliano marefu na wenzetu katika Upinzani, tulipitisha na kulitangza Azimio la Zanzibar, ambalo liliutangaza mwaka 2019 kuwa ni “MWAKA WA KUDAI DEMOKRASIA”, mwaka ambao tungepambana kuzidai haki zetu zote tunazonyimwa kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujalitekeleza hilo, kwa matendo ya sasa ya CCM na Serikali, tumepewa nafasi ya kutekeleza Azimio la Zanzibar. ACT-Wazalendo tutakwenda kwa wenzetu wa Upinzani, ili kurudi kutekeleza Azimio la Zanzibar.

TUNAWAPA ARI wanachama na wafuasi wetu, pamoja na wananchi wote kwa ujumla, wakati ni sasa wa kuondoa hofu, kushikamana nasi katika kulinda Demokrasia ya nchi yetu. Hatupaswi kuwa waoga, hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja mmoja na kama KUNDI ZIMA LA KIJAMII.

Tumejitahidi kufuata njia zote za kisheria Lakini CCM na Serikali yake wameamua vinginevyo kwa kutuondoa katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Tumeamua kutafuta njia nyingine za kulinda demokrasia yetu. TUSILAUMIANE.

Mwisho; Kumekuwepo na vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na watendaji wa Serikali kuwabughudhi Wagombea wetu, wanachama na viongozi wetu maeneo mbalimbali nchini. Serikali ya Rais Magufuli isitufikishe kuvuka mstari wa Uvumilivu.

Kabwe Z, Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Dar es Salaam.

Novemba 8, 2019
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
2,512
Points
2,000

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2018
2,512 2,000
Kuna haja gani ya kushiriki uchaguzi wakati CCM wamejipitisha bila kupingwa, wakati mgombea akiteuliwa bila kupingwa ina maana hakuna uchaguzi.

Kuna hivyo vyama vya kipuuzi eti vimesema vinashiriki, wakati havijaweka mgombea hata mmoja, na wala havina hata muwakilishi mmoja bungeni. Ni wapuuzi waliobobea.

Siku za CCM zinahesabika, muda si mrefu wataangukia pua.

1) Ubaguzi/ Uonevu/ Uadui/ Mgawanyiko wa "WANA CCM KWA WANA CCM" ndani ya chama chao (LUMUMBA) haujakwisha bado.

2) Uadui kwa vyama vya upinzani umezidi.

3) Uadui kwa raia umezidi mara 100.

4) Wafanyakazi wa umma toka 2015 - leo hawajaongezewa hata sh100 katika mishahara (licha ya ahadi wanazopewa).

5) Ufsadi wa Sh Trillioni 1.5, na Sh Trillioni 2.0 - Za Prof Assad CAG.

6) Ufisadi wa ununuz wa ndege kwa bei "MARA MBILI".

7) Utekwaji/Kupotea/Kuuliwa kwa raia.

8) Uonevu wa kufunga watu/viongozi wa upinzani gerezani bila sababu.

9) Uminywaji wa wanahabari/vyombo vya habari.

10) Ubakwaji wa demokrasia (RAPE OF DEMOCRACY).

11) Ajira/Biashara kufa kifo cha mende.

12) DPP na TRAFICK POLICE kugeuzwa TRA (Wakusanya mapato).

13) Mauwaji ya kibiti (watu wasiojulikana).

14) Watu wasiojulikana.

15) Uongo uliokithiri kutoka kwa viongozi kwa raia.

16) Figisu kwa CAG (Mtetezi wa kodi za raia)

17) Bunge kua dhaifu.

18) Kupigwa marufuku kwa wapinzani kufanya vikao/kampeni (wakati CCM wamefanya kampeni na vikao kuanzia 2015 mpaka sasa)

19) Kufukuza/ Kwaonea/ Kuwadhalilisha "WAFANYAKAZI WA UMMA" mbele ya hadhara bila hata kuwapa haki ya kwasikiliza (Kwa kutafuta sifa).

Na mengine mengi. . .
 

adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
10,401
Points
2,000

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
10,401 2,000
Acha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao

Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama

State agent
Wewe huwezi kuwa naakili zaidi ya chadema
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Messages
5,646
Points
2,000

Ndikwega

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2012
5,646 2,000
Hayo yametangazwa na kiongozi wa chama hicho Mh Zitto Kabwe.

ACT WAZALENDO CHAIFUATA CHADEMA, CHAJITOA KUSHIRIKI UCHAGUZI. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza kuwa chama hicho kimejitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa sababu kuwa wagombea wa chama hicho wengi wameenguliwa.
View attachment 1257821
Mungu mwema! Tunaona Upinzani kiamarika sasa. Tuko Pamoja. Ahsante kwa Kuhuisha Mioyo ya Watanzania.
 

mwayena

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2016
Messages
2,341
Points
2,000

mwayena

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2016
2,341 2,000
Acha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao

Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama

State agent
Badili user name jiite jiwe agent au ccm agent...
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
32,064
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
32,064 2,000
Acha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao

Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama

State agent
Baki na matamanio yako! Utaliwa mjini hapa, kaa hapo Lumumba mjadili maumivu.
Kuiba ushindi mlikuwa mnataka lakini mnaachiwa mgawane nafasi mnahangaika kwa aibu tena.
Mkoje nyie?
 

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
7,019
Points
2,000

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
7,019 2,000
Acha uongo mods kuweni makini maana kulingana na twiti ya zito bado wanafanya tathmini na wameweka poll mtandaoni kuwauliza wanachama wao

Hawataki kutumia upumbavu kama wa chadema kubaka haki za wanachama

State agent
Wewe ni mpungukiwa? Azimio limesomwa kwa uwazi, kama umekosa uelewa, umekosa hata macho?
 

Forum statistics

Threads 1,358,436
Members 519,294
Posts 33,168,245
Top