Challenge Cup 2008 - Matokeo

Jibuti wachovu siku zote. Zanzibar Stars ni wazuri sana this year-kwani wametoka 2-2 na Sudan (Sudan ndo wanaenda Ghana Jan) tuwape moyo washinde wasonge mbele!
 
Jibuti wachovu siku zote. Zanzibar Stars ni wazuri sana this year-kwani wametoka 2-2 na Sudan (Sudan ndo wanaenda Ghana Jan) tuwape moyo washinde wasonge mbele!

kwanza nnawapa pongezi ndugu zangu wa zanzibar kwa kutuwakilisha vyema na nnaomba mambo yawe mazuri zaidi

invisible umtuangusha ndugu yangu, kama hujaja ukatoa sababu ya kwa nn umeshindwa kutekelza ahadi yako, basi nitakuwa na shaka kuamini kuwa ww unaiangalia tanzania kama ni tanganyika na zanzibar


masahihisho
mzee invisible nimeiona excuse yako sawa mzee nnafuta malalmiko yangu.

mungu akupe uzima na uje hapa tushirikiane
 
Tuwekeeni ratiba nzima halafu ndio yafuate matokeo. Sio unastukizia sijui Angola 2 - Taifa stars 3 hujua walitarajiwa kucheza lini na wapi.
 
Tumeliwa tena kwa mara nyingine hebu angalia main objective ya Maximo.

Taifa Stars coach Marcio Maximo told BBC Sport that reaching the quarter-finals was the main objective.
 
Tumeliwa tena kwa mara nyingine hebu angalia main objective ya Maximo...
...nadhani malengo ya Maximo ni sawa, huwezi kukwea mti kwa kuanzia katikati lazima uanzie chini. We have to accept the fact that kiwango chetu kwa nchi za E&C Africa bado kiko chini (saana). Tusiwe wagumu kukubali ukweli.
======================
 
...nadhani malengo ya Maximo ni sawa, huwezi kukwea mti kwa kuanzia katikati lazima uanzie chini. We have to accept the fact that kiwango chetu kwa nchi za E&C Africa bado kiko chini (saana). Tusiwe wagumu kukubali ukweli.


Kwani tangu lini tumeshindwa kuchukua kombe la challenge cup? Tumechukua kikombe bila kuwa na makocha kutoka nje ya Tanzania. Huyu alisema atatupeleka Ghana kashindwa sasa hata challenge cup ambayo ni cha mtoto anataka kufika robo fainali tu. Huu ni ujinga wa kuwaendekeza makocha wabovu kama huyu ambaye tutakuwa naye bila kuonyesha ushindi wa kikombe chochote cha maana na baadaye kuambiwa alijitahidi sana (Wakati atakuwa amekwisha komba kitita). Tumechoka na wababaishaji wanaojitahidi tunataka wanaoleta mafanikio.

Hiki kiwango cha chini kimeanza wakati huu wa Max?
 
Kwani tangu lini tumeshindwa kuchukua kombe la challenge cup? Tumechukua kikombe bila kuwa na makocha kutoka nje ya Tanzania...
...teh teh teh, mkuu I salute you, lakini pengine sijakupata vizuri. Unamaanisha mashindano ya Challenge ambayo Tanzania ilishiriki kabla ya ujio wa Mtakatifu Ndoranga? Kumbukumbu zinaonyesha (correct me if I'm wrong) Tanzania imewahi kuchukua hili kombe mwaka 1974 na 1994, wakati ambao kabla ya kipyenga kupulizwa wachezaji walikuwa wakinywa maji ya bendara. Baada ya Mtakatifu kuivuruga FAT, mafanikio yoyote, ikiwemo kufika nusu-fainali mwaka 2002 (tena kwetu) na robo-fainali mwaka 1999, yalikuwa ya kimungu mungu.

Sitaki kusema kuhusu Maximo, lakini siku zote ukitaka kufanya mambo 'professionally' lazima uanze na 'history' husika na kuchambua hali halisi ya wakati huo. Huyu bwana amekuja kipindi ambacho, takribani miaka 10 ya nyuma kulikuwa na uvundo kwenye soka. Kiwango cha 'individual-player' kwa sasa kiko chini saana, lazima tukubali! For instance, with all current incentives, lakini ni aibu (na sijui utaanzia wapi) kulinganisha kiwango cha mchezaji kama Danny Mrwanda na kile cha Peter Tino.

Saluti kaka, mkono kwenye paji la uso
=================
 
mjengwa blog said:
Kili Stars Yatoka Sare Na Burundi
Ni katika mechi ya kuwania kushika usukani wa kundi. Timu zote mbili zimetoka uwanjani bila kufungana. Stars ndio walikuwa wanahitaji ushindi ili waongoze kundi. Inasemwa kuwa washabiki wa soka bado hawaridhiki na kiwango kinachoonyeshwa na Stars. Na kwamba hata leo kumesikika kelele za kuzomea pamoja na serikali kuonya juu ya tabia hiyo ya washabiki wa hapa nyumbani.

kutokana na maneno ya kocha kiwango cha kufika robo fainali ndiyo ilikuwa mpango wake sasa mnategemea nini.
 
Back
Top Bottom