Chalinze, Pwani: Askari trafiki agongwa na kufariki

Taarifa ya uongo ya Police itampeleka Motoni Marehemu... Watende haki hao Police japo sio haiba yao... Dereva apewe ulinzi wa taasisi Nyingine maana watamuonea sana Dereva kwa jinsi walivyo polisi... wanapenda kununua kesi za pilisi wenzao... Watakao muonea huyo dereva walaaniwe Dereva ashitakiwe kwa haki bila uonevu
 
Nimemsikia Kamanda Siro, kaagiza operesheni kamata magari mabovu nchi nzima kuanzia kesho, tuchukue hadhari Wana hasira ya msiba,tii Sheria Bila shuruti .
 
Hawa traffic huwa wanadhani magari ni ndugu zao.any way RIP
Ha ha ha!
Du.......!
Kuna ukweli ndani yake.
Kuna siku natoka Tanga sehemu za Kwedikwazu, mara trafiki huyo kajitokeza barabarani na mimi niko moto wa 120km/hr.
Nilimkwepa halafu nikasimama, kwa kweli nilimkemea na kumwambia uhai wake unathamani sana kuliko ujinga aliofanya.
 
Haya ndio madhara ya kupiga mkono ukitokea kichakani,tena kwenye kona.

Hata ningekua mimi, NAKUPELEKEA TU MOTO.
 
Pamoja na kero ya hawa askari wa barabarani ya kuomba rushwa na kung'ang'ania vikosa vidogo ili uwape rushwa, madereva wa mabasi ni kero sana kwa madereva wengine. Wanakwenda mwendo wa ovyo kama barabarani wako wao tu na hawajali magari madoho kiasi kwamba inabidi uwapishe au usimame wakati uko upande wako. Hawa pamoja na madereva wa magari ya serikali ni kero zaidi kuliko askari wa barabarani. Pamoja na pole kwa ndugu wa askari aliyegongwa nachelea kusema haya ni matokeo ya kuwaendekeza hawa madereva wa mabasi kwa kupokea virushwa. Madereva hawa hawawaogopi tena matrafiki kwani wanaandaa mzigo tu wa kuwahonga na huko barabarani ni vituko tu.
 
Kwa kweli niwe muwazi, ilishanikuta tukio kama hili, (external maji chumvi road) askari alisimamisha gari niliyokuwa naiendesha nikawasha taa ya ishara napark mbele!! Alikuwepo askari mwingine mbele akatoka kwa jazba na kuzuia gari kwa mbele!! My God, kwa kujiweka mbele ya gari!! Nilishika brake hadi brakes pad zilipasuka!! Kweli niwe muwazi afande Sirro ana kazi kubwa kuwaelimisha hawa ndugu zetu!! Fika niseme Huyo marehemu atakuwa na hulka ya huyu wa external makuburi!!
 
Pamoja na kero ya hawa askari wa barabarani ya kuomba rushwa na kung'ang'ania vikosa vidogo ili uwape rushwa, madereva wa mabasi ni kero sana kwa madereva wengine. Wanakwenda mwendo wa ovyo kama barabarani wako wao tu na hawajali magari madoho kiasi kwamba inabidi uwapishe au usimame wakati uko upande wako. Hawa pamoja na madereva wa magari ya serikali ni kero zaidi kuliko askari wa barabarani. Pamoja na pole kwa ndugu wa askari aliyegongwa nachelea kusema haya ni matokeo ya kuwaendekeza hawa madereva wa mabasi kwa kupokea virushwa. Madereva hawa hawawaogopi tena matrafiki kwani wanaandaa mzigo tu wa kuwahonga na huko barabarani ni vituko tu.
Ni bora hawa madereva wawekewe Kamera kuliko kero ya polisi kila kona!! Dereva akiwaona askari mbele na kama alishabambikiwa makosa huko nyuma anapoteza kabisa umakini, ndio maana ajali zinazidi!!
 
Pole kwa familia, isijekuwa alijiona robot akasimama mbele ya gari baada ya kupata radio kuwa huko alikotoka amekaidi kusimama.

Soldier siwaamini sana wanaweza pindua taarifa.
 
Ila kama alifanya kwa kusudi basi hafai huyo dereva

Ova
Kama ni makusudi huyo dereva watampiga na kifungu cha dangerous driving....hili kosa ukitiwa hatiani kuna kifungo na fine hapo......
reckless driving ina kifungo na fine mara nyingi mahakimu wanaishia kupiga fine tu....
manake hakimu anachagua akupige kimoja ama vyote
 
Mimi yananikuta mara kibao. Maana kuna days natembea na pikipiki.......wananing'ang'ania tunamalizana kiwanaume.

Kuna siku nmetoka home Kijichi, Nimefika pale Uhasibu nimesimama kwenye zebra. Sina kosa lingine lote. Aka ms*nge mmoja wamebebana wawili wamevaa kiraia akachomoa funguo. Tulibishana kama nusu saa hivi wanataka kupandisha chombo yangu kwenye roli. Wakaanza kuogopa huenda mi nna connection kali. Nikawatia elfu 5 nikasepa.
Njaa kali zitawamaliza🥵
 
Kama nilivyoipata FACE BOOK nami naileta nzima nzima.....RIP F.3936 CPL ABOUBAKARI s/o SALEHE MWINDADI.

"AJALI YA GARI KUMGONGA ASKARI NAKUSABABISHA KIFO :
(XX) MNAMO TAREHE 07/06/2021 MAJIRA YA SAA 08:29HRS HUKO MAENEO YA KIJIJI CHA BWAWANI KATA YA TUKAMISASA TARAFA YA MDAULA, BARABARA KUU YA DSM/ MOROGORO WILAYA YA KIPOLISI CHALINZE MKOA WA PWANI GARI NO. T. 681 DFX AINA YA YUTONG BUS MALI YA KAMPUNI YA KISBO SAFARI IKITOKEA DSM KUELEKEA KAHAMA IKIENDESHWA NA DEREVA IDDI s/o AYUBU@ KAGEMBE,46YRS,MUISLAM,MSUKUMA, MKAZI WA DSM ILIMGONGA ASKARI AKIWA KAZINI NO. F.3936 CPL ABOUBAKARI s/o SALEHE MWINDADI, 39YRS,MUISLAM, MSHIRAZI, ASKARI WA (K) MDAULA,MKAZI WA KIBAHA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE (XX) MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA TUMBI KUSUBILI UCHUNGUZI WA DAKTARI (XX) DEREVA ALIYESABABISHA AJALI ANASHIKILIWA KITUO CHA POLISI CHALINZE KWA MAHOJIANO ZAIDI (XX) CHANZO CHA AJALI NI DEREVA KUENDESHA KWA MWENDOKASI NA KWA MAKUSUDI KUMFUATA ASKARI ALIPOSIMAMA NA KUMGONGA. KABLA YA KUMGONGA ALISIMAMISHWA MARA KADHAA POINT MBALIMBALI NA KUKAIDI AMRI (XX)"
Mwisho wa kunukuu.View attachment 1812477
Nilikuwepo siku ya ajali aligongewa njia ya kutokea tanga cyo moro na nadhan alikufa akiwa njian kuelekea tumbi hospitali
 
Back
Top Bottom