Chalamila: Nilikuwa likizo kama Injini ya gari lililoharibika

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,589
14,137
Habari Wana JF,

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila Amesema alikuwa likizo tuu kama Injini ya gari lililoharibika..

Kuharibika kwa Board haimaanishi Injini ni mbovu.👇

===

1659690821263.png
MKUU wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema alikuwa likizo kama injini ya gari lililoharibika.
Ameyasema hayo leo Agosti 4, 2022 wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge.

Amesema kwa sasa amerudi kama gari jipya na yuko tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, amewetaka Wakuu wa Wilaya mkoani humo kufanya kazi kwa bidii kwani vyeo vya kuteuliwa ni vya mzunguko na kila mmoja Mungu umpa kwa wakati wake.

Amesema kama watafanya kazi kwa hofu ya kutoteuliwa tena basi wataaribu kazi na kushindwa kuwatumikia wananchi.

Amesema utekelezaji ambao ataanza nao ni maagizo ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu,wakati alipofanya ziara yake mkoani Kagera na kuwataka viongozi kuhakikisha wanatafuta njia ya kuufanya mkoa wa Kagera kuwa mkoa mwenye uchumi wa juu kwa sababu unakila kigezo cha kuwa Mkoa wenye uchumi mkubwa.

Awali akikabidhi ofisi Jenerali Mbuge alimuomba mkuu huyo wa mkoa kufanikisha maswala ya kitaifa kwa kuanza na Sensa ya watu na makazi, kufanikisha kuhitimisha mbio za mwenge kitaifa, kuhakikisha mradi wa bomba la mafuta unafanikiwa na wananchi wanalipwa fidia.

Chanzo: Habari Leo
 
Mmoja ni mtoto WA Baba WA Taifa na mwingine ni mtoto WA Fukara.



Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Chalamila mtoto wa fukara??? tuulize wanyalu tutakwambia...kwa taarifa yako Chalamila ni royal family...ukoo wa Chalamila una link ya damu na ukoo wa Mkwawa wana ukwasi tangu 1800s mwishoni...wanazijua bunduki, mavazi na pesa miaka mingi sana, huyo Chalamila unaemuona haujui umaskini...
 
Chalamila mtoto wa fukara??? tuulize wanyalu tutakwambia...kwa taarifa yako Chalamila ni royal family...ukoo wa Chalamila una link ya dame na ukoo wa Mkwawa wana ukwasi tangu 1800s mwishoni...wanazijua bunduki, mavazi na pesa miaka mingi sana, huyo Chalamila unaemuona haujui umaskini...
Acha urongo

Kina Chalamila wako wengi kama Sanga au Massawe

Huyu haitoki kwa Ramadan Chalamila mbia wa Kwacha enzi zile

Huyu ni kule Ugalatiani kwa akina Betty Mkwasa
 
Chalamila mtoto wa fukara??? tuulize wanyalu tutakwambia...kwa taarifa yako Chalamila ni royal family...ukoo wa Chalamila una link ya dame na ukoo wa Mkwawa wana ukwasi tangu 1800s mwishoni...wanazijua bunduki, mavazi na pesa miaka mingi sana, huyo Chalamila unaemuona haujui umaskini...
Chalamila hawana ukwasi, hii family ndio ilikua na share kubwa kwenye Ile kampuni ya usafirishaji KWACHA, buses zote za kampuni hii mimi nilikua team ya Leyland CD, navolonge swela
 
Back
Top Bottom