Chalamila amalize kwanza tatizo la Daladala na Bajaj Mbeya Kabla hajapelekwa Mwanza

Mpingamkoloni

Member
Feb 14, 2021
6
45
Mheshimiwa Samia!

Ninakubaliana na uteuzi wako kwa Mhe. Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Kijana mdogo, mchapakazi, lakini mara nyingi huwa anakuwa moto na kukosa busara, kitu ambacho kwa umri wake bado ana muda mwingi wa kujifunza.

Lakini taarifa zinasema, kwa muda mrefu sana Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Chalamila, ameshindwa kutatua mgogoro wa Bajaj na Daladala barabarani. Taarifa zaidi zinasema Mkuu wa Mkoa amekuwa akiegemea sana upande wa bajaj na kuwajibu hovyo waendesha daladala, huku tetesi zikidai hii inatokana na mmoja wa wanasiasa mashuhuri hapo Mbeya kuwa na taasisi inayokopesha bajaj ambazo zimetapakaa katikati ya mji.

Mpaka sasa ninapoongea wananchi wanaotegemea usafiri wa daladala jijini Mbeya wanahaha kutafuta usafiri.

Chalamila kijana mzuri sana, ila asiache tatizo kwa Mkuu wa Mkoa Homera. Alimalize. Pia, wanasiasa waache kuleta migongano ya kimaslahi.
 

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
715
1,000
Acha wivu
Binafsi sijafurahia Chalamila kutolewa kwenye nafasi ya Ukuu wa Mkoa. Yupo vizuri ukiacha mihemko ya ujana. Atarudi tu.

Ila huyu jamaa hapa hakuonesha wivu, kamsifu kuwa ni kijana mzuri (sana). Lakini haya mambo huwa ni sum of all.. Akirudi atakuwa kajifunza.
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,430
2,000
Kwani hakuna shughuli nyingine za kujiingizia kipato anaweza fanya zaidi ya ukuu wa Mkoa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom