Chalamila alipotoshwa, Mhandisi Gabriel usikubali

Naamini kuna sababu nyingine iliyofanya Chalamila akaondolewa ofisini tofauti na hiyo uliyoandika hapa.

Kama ulichokiandika kina ukweli basi watendaji wake Chalamila ndio watakuwa wamemponza, hivyo sikutegemea wewe uje hapa uanze kumlaumu Chalamila moja kwa moja wakati mtu hata miezi mitatu alikuwa bado hajamaliza ofisini.

Hata kama shida yako ni hiyo taarifa kuondoa umiliki wa serikali wakati kimsingi bado upo kama unavyodai, bado sioni sababu ya kumuondoa Chalamila ofisini kwa issue ambayo ingemalizwa ndani ya dakika chache tu kwa kufanyia marekebisho palipokosewa kwenye hiyo taarifa.
Kama upo serious na nafasi hiyo na nifuatiliaji wa mambo huwezi kupotoshwa kibwege namna hiyo
 
Mradi unaandiko na hatua za utekelezaji chini wizara madini nk, kwamba taarifa ya RC iondoe share za serikali Kama zipo!?
Shangaa na wewe....Hii kelele inaashiria jambo nyuma ya hii kitu, jiwe limetupwa gizani lika bonda mtu akasahau halikulengwa kwake...
Masalia ya magufuli yanaondolewa taratibu.
Acha uchonganishi...
 
Mimi sijakuelewa. Hebu rudi kwenye microphone tena utueleweshe vizuri....

1. Kwamba, huo mgawanyo wa hisa miongoni mwa wanahisa/wamiliki wa hiyo kampuni ya MPMR ni wa maneno tu au uko kisheria na kimaandishi/kimkataba...?

2. Kama ni wa kisheria, sasa inawezekanaje matamshi tu ya RC kwa kupitiwa au kukosea yatengue uhalali wa serikali kumiliki hisa 25%...?

NOTE:
å Aliyekuwa RC Mwanza ndugu Chalamila Albert iko sababu nyingine iliyomfanya aondolewe kwenye nafasi hiyo

å Hii unayoitaja, niungane na wengine kusema kuwa hai - make sense hata kidogo. Na kwa ufupi sana ni kuwa, huyu (Chalamila) kwa kauli na matendo yake hakuwa ana qualify kuwa kiongozi ktk level ya u - RC...

å Huyu anatakiwa apekekwe Chuo cha Sanaa Bagamoyo akawe mkufunzi huko...!!
Siku nyingine tumia akili yako vizuri. Unadhani hisa za Serikali (TTCL) zilizoibiwa katika kampuni ya Celtel (sasa Airtel) hazikuwa katika maandishi ya kisheria?
 
Mradi unaandiko na hatua za utekelezaji chini wizara madini nk, kwamba taarifa ya RC iondoe share za serikali Kama zipo!?
Hata hisa za Serikali zilizoporwa katika Celtel zilikua katika utekelezaji chini ya wizara ya mawasiliano.
 
Ofisi ya RC pale mwanza 90% ya staff tangu kafika walikua hawamkubali.

Probably watakua wamempotosha maksudi ili avimbe mabega ili aliwe kichwa
 
Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila alipotoshwa na yeye akapotosha umma, wewe usirudie kosa hilo. Tafuta chapisho langu la June 9 lenye kichwa cha habari "RC Chalamila-Mwanza amepotosha au amepotoshwa!?", litakusaidia. Ukifika ofsini irudie taarifa ya ziara ya Rais Mkoani Mwanza. Itangazie Dunia, pamoja na mambo mengine Rais atatembelea na kufungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery) kinachomilikiwa kwa ubia baina ya kampuni tatu, katika hizo Kampuni ya STAMICO inaiwakilisha Serikali ya Tanzania kwa asilimia 25.

Taarifa ya Chalamila iliiondoa Serikali ya Tanzania katika umiliki huo, akaifanya kampuni ya Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa Kampuni binafsi (Sekta binafsi). Hili ni kosa, zilikua dalili za kuiba hisa za (STAMICO) Serikali kama ilivyofanyika miaka ya nyuma kwenye Kampuni ya Celtel. Kama sio JPM kuzirudisha ndio tulikua tumeliwa hivyo hadi sasa. Hata nilipomwandikia hapa kumuomba Chalamila abadilishe statement yake aombe radhi, hakunisikiliza.

Mhandisi Gabriel, irudie taarifa hiyo. Iweke Serikali (STAMICO) katika position yake, Rais wa nchi hawezi kufungua kiwanda kinachomilikiwa kwa ubia na Serikali bila Serikali kutajwa. Haiwezekani! Usiwasikilize wanaosema hisa zetu ni kidogo (25%) hivyo hazina uamuzi katika Kampuni kwa hivyo kutozihesabu ni haki. Hawa hawajui lolote kuhusu aina za umiliki wa biashara, wapuuze. Ingalikua wenye hisa kidogo hawatambulishwi katika umiliki, sisi tusingalitambulishwa katika umiliki wa kampuni ya kusafirisha mafuta ya EACOP ambapo tuna hisa 15% sawa na Uganda. Itambulishe Serikali katika umiliki wa MPMR utakuja kunishukuru baadae.

Usiwasikilize wenye kusema kuwa mabango ndio yamemuondoa Chalamila Mwanza. Hakuna Rais asiyependa Mabango kwa sababu ndio mawasiliano ya haraka kutoka chini kwenda juu. Mabango ndiyo yenye kumfahamisha Rais uwajibikaji wa watendaji wake, mabango yangalikua sababu Chalamila angaliondolewa baada ya mabango kusomwa. Mabango hayaondolewi kwa kupigwa marufuku bali kutatua changamoto za watu. Kauli ya Chalamila kuhusu mabango ilikua ni ya uwajibikaji kwake na wenzake, sio kosa. Rais mwenyewe alisema mabango yasizuiliwe, kwa vyovyote vile hilo haliwezi kuwa kosa la kumuondoa Mkuu wa Mkoa. Nisikilize mimi, irudishe nafasi ya Serikali katika umiliki wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu halafu usisahau kuwa Katibu Tawala uliyenaye hapo ametoka Ikulu.

Utanikumbuka baadaye!

MenukaJr,

Da'slama-Tanzania.
Acha uongo Mkuu wa Mkoa hana uwezo wa kuondoa kampuni kwenye umiliki wa share hapo umedanganya
 
Chalamila bangi sana kama Boban tu
Bangi mnaionea tuh,after all bangi ni mmea tuh,unakosa gani mmea ule?

Mbona Kuna mimea Mingi tuh haisemwi vibaya,ule mmea kama hujachanganya na chochote ni dawa ule buji buji,it's a weed,just a 🌲 tree,like other trees
 
Tabia za mabega juu, alifanya ziara TRA ,Mza kujitambulisha aliongea lugha za kibabe eti watu hawakumwelewa SSH eti "walipakodi wengi wakorofi si vibaya mkitumia vyombo vya dola, ...RPC... fanyeni kikao waiteni walipakodi korofi nami mniite niwaambie ...' Rejea video you tube " Chalamila TRA Mwanza"
 
Bado sijaelewa kabisa..

Labda Chalamila katumika Tu kuondoa watu
Kwenye mjadala wa bajeti..
Siasa za Tanzania. Ila kila chenye mwanzo kina mwisho. Hawa viongozi wanajisahau sana wakati mwingine. Sisi tunataka maendeleo na maisha bora. Wao wanataka madaraka kwa kujipendekeza pendekeza.
Wanasahau kabisa wanawatumikia wananchi
 
Mimi sijakuelewa. Hebu rudi kwenye microphone tena utueleweshe vizuri....

1. Kwamba, huo mgawanyo wa hisa miongoni mwa wanahisa/wamiliki wa hiyo kampuni ya MPMR ni wa maneno tu au uko kisheria na kimaandishi/kimkataba...?

2. Kama ni wa kisheria, sasa inawezekanaje matamshi tu ya RC kwa kupitiwa au kukosea yatengue uhalali wa serikali kumiliki hisa 25%...?

NOTE:
å Aliyekuwa RC Mwanza ndugu Chalamila Albert iko sababu nyingine iliyomfanya aondolewe kwenye nafasi hiyo

å Hii unayoitaja, niungane na wengine kusema kuwa hai - make sense hata kidogo. Na kwa ufupi sana ni kuwa, huyu (Chalamila) kwa kauli na matendo yake hakuwa ana qualify kuwa kiongozi ktk level ya u - RC...

å Huyu anatakiwa apekekwe Chuo cha Sanaa Bagamoyo akawe mkufunzi huko...!!
Hizo sababu za hisa sijui nini sio za kumwondoa chalamila.huyu alikuwa na ajenda ya siri kisiasa.Kumdhalilisha Madam President.Full stop.
 
Chalamamila " nimempigia Rais Simu asubuhi hii kumshukuru kwa kutupatia milioni mia mbili kwa utekelezaji wa miradi katika jiji la Mbeya". Siku chache Taifa likatangaziwa kwa simanzi na masikitiko makubwa ya kuondokewa na aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati John pombe Joseph Magufuli.

Mkuu wa Mkoa anaetumia hekima, busara na maarifa hawezi kuwahanasisha wananchi kuwa wabebe mabango hata ya matusi katika ujio ziara ya Rais!. Hili ni kosa kubwa sana linalofanywa na mtawala mpayukaji na mropokaji - wewe Chalamila ulipata wapu ujasiri wa kuwahamasisha kuandika matusu kwa Rais?. Nakushauri kasome 14 principles of management (power of command/scalar chain). Mpayukaji aende akapayuke Iringa.
 
Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila alipotoshwa na yeye akapotosha umma, wewe usirudie kosa hilo. Tafuta chapisho langu la June 9 lenye kichwa cha habari "RC Chalamila-Mwanza amepotosha au amepotoshwa!?", litakusaidia. Ukifika ofsini irudie taarifa ya ziara ya Rais Mkoani Mwanza. Itangazie Dunia, pamoja na mambo mengine Rais atatembelea na kufungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery) kinachomilikiwa kwa ubia baina ya kampuni tatu, katika hizo Kampuni ya STAMICO inaiwakilisha Serikali ya Tanzania kwa asilimia 25.

Taarifa ya Chalamila iliiondoa Serikali ya Tanzania katika umiliki huo, akaifanya kampuni ya Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa Kampuni binafsi (Sekta binafsi). Hili ni kosa, zilikua dalili za kuiba hisa za (STAMICO) Serikali kama ilivyofanyika miaka ya nyuma kwenye Kampuni ya Celtel. Kama sio JPM kuzirudisha ndio tulikua tumeliwa hivyo hadi sasa. Hata nilipomwandikia hapa kumuomba Chalamila abadilishe statement yake aombe radhi, hakunisikiliza.

Mhandisi Gabriel, irudie taarifa hiyo. Iweke Serikali (STAMICO) katika position yake, Rais wa nchi hawezi kufungua kiwanda kinachomilikiwa kwa ubia na Serikali bila Serikali kutajwa. Haiwezekani! Usiwasikilize wanaosema hisa zetu ni kidogo (25%) hivyo hazina uamuzi katika Kampuni kwa hivyo kutozihesabu ni haki.

Hawa hawajui lolote kuhusu aina za umiliki wa biashara, wapuuze. Ingalikua wenye hisa kidogo hawatambulishwi katika umiliki, sisi tusingalitambulishwa katika umiliki wa kampuni ya kusafirisha mafuta ya EACOP ambapo tuna hisa 15% sawa na Uganda. Itambulishe Serikali katika umiliki wa MPMR utakuja kunishukuru baadae.

Usiwasikilize wenye kusema kuwa mabango ndio yamemuondoa Chalamila Mwanza. Hakuna Rais asiyependa Mabango kwa sababu ndio mawasiliano ya haraka kutoka chini kwenda juu. Mabango ndiyo yenye kumfahamisha Rais uwajibikaji wa watendaji wake, mabango yangalikua sababu Chalamila angaliondolewa baada ya mabango kusomwa.

Mabango hayaondolewi kwa kupigwa marufuku bali kutatua changamoto za watu. Kauli ya Chalamila kuhusu mabango ilikua ni ya uwajibikaji kwake na wenzake, sio kosa. Rais mwenyewe alisema mabango yasizuiliwe, kwa vyovyote vile hilo haliwezi kuwa kosa la kumuondoa Mkuu wa Mkoa. Nisikilize mimi, irudishe nafasi ya Serikali katika umiliki wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu halafu usisahau kuwa Katibu Tawala uliyenaye hapo ametoka Ikulu.

Utanikumbuka baadaye!

MenukaJr,

Da'slama-Tanzania.
Andiko halina mantiki.
Kwani Mkuu wa Mkoa ndio anahisa katika hicho kiwanda au Treasury Secretary wa Hazina?
Uliyoyaandika hayana msingi kwani Serikali haifanyi kazi kwa matamko yasiyoendana na uhalisia wakile kilicho katika umiliki wa serikali.
Na serikali haiwezi kuondolewa umiliki au hisa zake kwa tamko la Mkuu wa Mkoa.

1623402717127.png

Mkuu wa Mkoa Chaamila kakosa adabu PERIOD.
Kwa kuhamasisha mabango ya matusi kamkosea sana Mama Samia na kutoheshimu madraka na heshima ya Mkuu wa Nchi.
 
Engineer Gabriel sawa na yule jamaa aliyehamishiwa Dodoma, sio watu wa vyombo vya habari kiviiile but ni watu wa KAZI sana, jamaa aliibadiri sana Geita
 
Bado sijaelewa kabisa..

Labda Chalamila katumika Tu kuondoa watu
Kwenye mjadala wa bajeti..
Umeona mbali mkuu. Na it's highly likely na kauli ya Mwigulu pia, naona madam presida kaamua kuwadivert watu
 
Andiko halina mantiki.
Kwani Mkuu wa Mkoa ndio anahisa katika hicho kiwanda au Treasury Secretary wa Hazina?
Uliyoyaandika hayana msingi kwani Serikali haifanyi kazi kwa matamko yasiyoendana na uhalisia wakile kilicho katika umiliki wa serikali.
Na serikali haiwezi kuondolewa umiliki au hisa zake kwa tamko la Mkuu wa Mkoa.

View attachment 1815145
Mkuu wa Mkoa Chaamila kakosa adabu PERIOD.
Kwa kuhamasisha mabango ya matusi kamkosea sana Mama Samia na kutoheshimu madraka na heshima ya Mkuu wa Nchi.

Huyo bila shaka alivuta kidogo.
 
Back
Top Bottom