Chakula kipi uliwahi kutana nacho ugenini ukajutia ugeni wako?

Nilikuwa Zanzibar forodhani sehemu ile karibu na bandari,jioni nikaenda kununua mishikaki,nikanunua mishikaki ya ng'ombe ,si nikaona tena mishikaki mirefu membamba ,nikadhani ni mishikaki ya firigisi ,nikachukua kama nne,nilivyokula niliona tamu sana ,nikamwambia jamaa aongeze,kuja kuuliza baadaye kumbe ni konokono wa baharini ,sahivi nikiviona napita mbali .
 
Niliwahi kutengewa nyama ya bata
Nilitengewa kula peke yangu huku pembeni akiwa kakaa Mwenyeji wangu tukipiga soga
Ebana kumbe mboga ile ilikua imechacha (imeharibika)
Ilibidi nile kwa kujikaza huku nikijizuia kutapika

Baada ya kufika home niliendesha (kuhara) siku mbili non stop
 
Mimi hakikua kibaya ila Vilikuwa vitamu balaa mpaka nikasema hawa kuku mbona wamepikwa kwa style ya kuchambuliwa chambuliwa minofu yake....hapo najiuliza sana sipati majibu ikapita kama week siku hiyo nachat na yule rafiki yangu nkamuuliza nyie why wale kuku mliwapika vile??? alicheka sana akasema kuku gani nkasema nlokula siku ile.... duuh akasema wew ule ni uyogaa..... nisisngeuliza ningeishi maisha yangu yote nkijua nimekula KUKU kumbe ni UYOGA😃 😃 😃
 
Nawe,,,,sipendi kabichi,sipendi mchicha yaani sipendi hizo mboga,,

Hizo chipsi nimeanza kujifunza kula ukubwani,japo home tokeapo viazi vilikuwa havipungui,,,wakipika chipsi napikiwa chakula changu,

Kwetu tunalima mabustani ya mboga uwanjani,kila aina ya mboga za majani tunalima,

Sent using Jamii Forums mobile app
kabichi,mchicha,biringanya,ndizi za kupika

hapana aisee.
 
Kuna makitu yanaitwa mashelisheli yako kama matikiti yanachemashwa yanatumika kama kitafunwa yalinishinda.
Mlenda pia kukaa kote ugenini sikuweza kuula mpaka leo
Kabichi nakula like la kupashwa tu kama kachumbari ila likipikwa likaiva siliwezi hata liekwe nyama.
ya kifala sana hayo madude,yana ladha plain watu wanakula harufu yake tu na mengine home tunaita mamung'unya yanapandwa na kuota kama maboga,ndio yale wamasai hutengenezea vibuyu,mabovu kishenzi halafu watu wanakula wana enjoy yaani
 
Juzi hapo nilinunua samaki warefu hivi kwa akili yangu nikajua ni Chuchungi kwani walikuwa na midomo mirefu. Toka wife apike wale samaki yani tukisikia harufu ya samaki kichefuchefu hata chakula sili. Kumbe ni nyoka wa baharini, yule mzeee nilimpiga marufuku na vikwazo asije nyumbani kwangu kamwe. .

Docta kanishauri nitumie Zentel na dawa flani zitakata kichef chefu. Ndo nimetumia dozi ya siku tatu hopefully it will be alright. .
Siku nyengine Muulize kwanza
 
Halafu umenikumbusha dona zamani ililiwa na maskini wa hali ya chini, watu wenye uwezo nakumbuka mahindi yalikua tunakoboa halafu mnaloweka kwenye maji kama siku mbili au tatu, halafu ndio mnayatoa mnaaanika yakikauka mnakoboa, sijui nani akaja kupigia chapuo dona likashika kasi kidogo watu wakaanza kuchanganya na muhogo walau liwe laini lakini dona kavu ni mtihani linakuaga zito hatari mdomoni.
Umenikumbusha kuloweka mahindi haha, ilikua lazima yalowekwe then yaanikwe yani yakipelekwa.mashine yanatoa unga mweupe saanaaaa na unakua na radha flani amazing yani,.me pia dona nilikuja kula wakati niko form 1 boarding school ole wiki ya kwanza nilipata shida sana kula hilo dona nikawa mchana siendi kula nangoja rice usiku ni bahati tu ile shule ilikua rice ni everyday jioni na Sunday Pilau ila tu mchana wote ni ugali dona na maharagwe au nyama ila yalinishinda.
 
kabichi,mchicha,biringanya,ndizi za kupika

hapana aisee.
Kuna mwana jf alikuja home,tulimuandalia ndizi alikula kisi,

Alivyosepa,nikamuuliza vipi msoai umeupwnda? Akaniambia sijawahi kukuambia huwa silagi ndizi,lakini najua nisingekula mngejisikia vibaya,,,,,,,,,,,aisee nilijisikia vibaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo mafuta anayoweka yako kama blueband ila akiweka kwenye maharage yananukia kama nyama ila taste yake unaona kama unakula maharage na mchuzi wa nyama uliooza..
Yale ni mafuta ya ng'ombe huwa wanachukua mafuta ya kwenye nyama zinawekwa jikoni mpaka yanabaki mafuta then yanaachwa kwenye chombo yanaganda(kama nipo sahihi lakini)
Yale unaweza kutumia kupikia mboga ila Kuna wengine huyala hivo hivo kama chakula.
 
Binafsi sintosahau safari ambayo nilipofika, dakika tano baadae katoto ka miaka saba kanakuja kuniuliza, "eti unaondoka lini?"

Msosi wa jioni ulikuwa wali wenye washawasha na chai yenye pilipili tena ya moto! ila wao wanakula vizuri tu kwenye sahani zao na vikombe vyao mikononi! Halafu nilieenda kumtembelea anamuuliza mkewe, "mbona chachandu kwenye chai iko kwa mbali?"

Chakula gani uliwahi kutana nacho ugenini ukajutia ugeni wako?

UZI TAYARI
Mimi Hata niende ukweni Au wapi...

Ukinipa mlenda wa Aina Yoyote Ile Mimi sili kabisa wala sijawahi Kuelewa.

Ukiweka kwenye mboga yako nyanya chugu,bamia,bilinganya aisee nitakuja nyama Tu kama ipo .
 
Kuna siku nimeenda kwa jiran nikakuta wamepika ugali na mboga maharage shida wakaiwekea mafuta ya mawese yale mafuta sijawahi yaelewa mpKa leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom