Chakula cha usiku: Wahanga sasa ni wanawake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chakula cha usiku: Wahanga sasa ni wanawake!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 18, 2009.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Zamani ilikuwa ni wanaume waliokuwa wakilalamika, kwamba wake zao hawataki kuwapa chakula cha usiku kama wanavyotaka. Lakini baadae yaani siku hizi ni zamu ya wanawake kulalamika.

  Katika nyumba nyingi siku hizi hasa mijini wanawake ndio wanolalamika zaidi kukosa chakula cha usiku kama wanavyotaka kutoka kwa waume zao.

  Kwa nini hali hii?

  Ukweli ni kwamba maisha yamebadilika sana na kila mtu anajitahidi sana kutaka kuhahakisha kwamba anafanya kazi hadi anaishiwa nguvu kabisa, akili na mwili vinachoka. Wanaume wengi wanaolalamikiwa na wake zao kuhusu kupata uhaba wa chakula cha usiku ni wale wanaofanya kazi sana.

  Ningependa kuwashauri wanaume kwamba wakati wanafanya kazi zao mchana wakumbuke kwamba kuna wake zao wapendwa ambao wanawasubiri jioni kuzungumza nao na zaidi ya hapo. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake. Pamoja na kwamba ni muhimu kwao kufanya kazi, lakini wakumbuke kwamba kazi hazina mwisho.

  Kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi. Mtu anapofanya mazoezi anawezesha damu kuzunguka na kufikia sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa. Kukaa ofisini kutwa na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi na kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa chakula cha usiku na kukipokea huwa kubwa.

  Lakini mbaya zaidi ni kwa wanawake wenyewe pia. Kuna wanawake ambao bado wanaishi kwa miiko ya karne moja nyuma. Hawa wanangoja wanaume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati chakula cha usiku. Tukumbuke kwamba hata wanaume nao ni binadamu pia, huhitaji wakati mwingine kushtuliwa, kwani wakishtua wao tu kila siku, kuna wakati hukinai.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu mbona hujaongelea wale wanaopitia Ohio na maeneo mengine baada ya kazi kupata kile kinachoitwa "kazi na dawa". Kwani hao akina dada (Ma Changu) wanapata huduma kutoka wapi kama si kwa baadhi ya hao wanaume wanaofanya kazi sana? Inawezekana kuchoka ina maana nyingine, "nimeshiba".
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,544
  Trophy Points: 280
  Kwa kadri unavyotumia akili kusaka pesa/kufanya kazi ndivyo unavyoshiba mapema na kadri unavyotumia nguvu munual ndivyo unavyozidisha hamu ya kula.
  Watumiao nguvu/mazoezi ndio walao sana, hivyo hao walalamikao ni wake wa watumiaji akili.
  Kadri maisha yanavyokuwa mazuri ndivyo upishi unavyotumia viungo kidogo na chakula hakinogi sana. Ukulinganisha madiko diko ya Kempiski na mama ntilie wa feri, utakuta feri sio mchezo. Hivyo wazee wengi hupenda kuanzia feri kupata ladha ya kuku wa kienyeji ndipo aende home kala dinner kama za Kempinski.

  Hata hao wahanga wanawake, sio wote, nao hupitia nazi gengeni, nyanya sokoni, fundi simu, fundi bomba, fundi umeme, na hata madereva kusaidia kumpashia mzee maana kila akirudi kachoka.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Haha!hahahahaaa!.....Pasco, usinikumbushe kule uswazi vingweta...tiiihiiiitihiii! hao wahanga wengine hupashwa kweli magengeni......mnakumbuka ule wimbo wa ''KISA CHA MPEMBA''

  Mtambuzi....thread yako nzuri, ila ungeiweka kule kny mapenzi, ingenoga zaidi!
   
  Last edited: Feb 18, 2009
 5. b

  bernard frank New Member

  #5
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is it the right place 4 this thread wadau?
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mbaya zaidi kuna wale wanaowaacha wake zao kule Moshi mpaka warudi huko Krismas, kisingizio? wanatafuta pesa. Hii ni balaa
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hapa si mahali sahihi kwani inabana uhuru wa kutoa vitu kama vilivyo. kuleeee kwenyeweee itakuwa ipo mahala pake, hatutasikia mambo ya mamantilie wala mamalishe, ni nyumba ndogo n.k vitachukua mkondo.
   
 8. M

  Muoldmoshi Member

  #8
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hii thread siyo pahala pake, please pelekeni kwenye jokes
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii kitu ilitakiwa iwe kule kwenye mahusiano na mapenzi.
  Sijui mods siku mnalala au majukumu mengi wazee?
  Lakini najua mna kazi kweli kweli poleni hii thread mtaipeleka mahala pake.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii kitu ilitakiwa iwe kule kwenye mahusiano na mapenzi.
  Sijui mods siku mnalala au majukumu mengi wazee?
  Lakini najua mna kazi kweli kweli poleni hii thread mtaipeleka mahala pake.
   
 11. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,811
  Likes Received: 2,514
  Trophy Points: 280
  Mwambie, usione haya

  Zamani ilikuwa ni wanaume waliokuwa wakilalamika, kwamba wake zao hawataki kuwapa chakula cha usiku kama wanavyotaka. Lakini baadae yaani siku hizi ni zamu ya wanawake kulalamika.

  Katika nyumba nyingi siku hizi hasa mijini wanawake ndio wanolalamika zaidi kukosa chakula cha usiku kama wanavyotaka kutoka kwa waume zao.

  Kwa nini hali hii?

  Ukweli ni kwamba maisha yamebadilika sana na kila mtu anajitahidi sana kutaka kuhahakisha kwamba anafanya kazi hadi anaishiwa nguvu kabisa, akili na mwili vinachoka. Wanaume wengi wanaolalamikiwa na wake zao kuhusu kupata uhaba wa chakula cha usiku ni wale wanaofanya kazi sana.

  Ningependa kuwashauri wanaume kwamba wakati wanafanya kazi zao mchana wakumbuke kwamba kuna wake zao wapendwa ambao wanawasubiri jioni kuzungumza nao na zaidi ya hapo. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake. Pamoja na kwamba ni muhimu kwao kufanya kazi, lakini wakumbuke kwamba kazi hazina mwisho.

  Kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi. Mtu anapofanya mazoezi anawezesha damu kuzunguka na kufikia sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa. Kukaa ofisini kutwa na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi na kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa chakula cha usiku na kukipokea huwa kubwa.

  Lakini mbaya zaidi ni kwa wanawake wenyewe pia. Kuna wanawake ambao bado wanaishi kwa miiko ya karne moja nyuma. Hawa wanangoja wanaume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati chakula cha usiku. Tukumbuke kwamba hata wanaume nao ni binadamu pia, huhitaji wakati mwingine kushtuliwa, kwani wakishtua wao tu kila siku, kuna wakati hukinai

  wakuu hivi Haya ni ya kweli!
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ulijuaje?? Ni kweli kabisa kuna wanawake kila siku ukitaka kula mzigo lazima ulianzishe wewe na siku ukikaa kimya nae anakaa kimya usipomuuliza hata mwezi anakaa utasikia wewe mwenyewe hutaki as if ni shida yako wewe tu mwanaume sijui wakoje??
   
 13. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Aisee!... Nice lecture...
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii imetulia
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  aaah wanakera asee!
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mke wangu hajalalamika bado
  ingawa niko bize ila naprovide bedtime menu bila kumiss the point.

  ila sometimes nahisi uchovu wa ajabu sana lakini najimaliza tu kwenye kujipinda bila wasiwasi.
   
 17. a

  agika JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nice thread chaku hongera,

  ila nasemaga kila siku kuna umuhimu mwanamke akawa malaya(ashakum si matusi) kwa mumewe, tukubali tusikubali saa nyingine waume zetu wanaenda kutafuta nyumba ndogo sababu wamechoka kila siku style ndo hiyohiyo mahala ndo hapohapo, kuanzwa ndo mpaka uanzwe wewe, akienda nyumba ndogo anadandiwa toka mlangoni shughuli inashia bafuni. unategemea akirudi atakuwa na nguvu ya kukupapasapapasa weee mwenye shombo la chakula cha jioni na watoto? tunawalaumu wanaume lakini na sisi wanawake sometimes tumezidi jamaniii hata ukioga jioni hujipaki manukato ukatandika chumba vizuri kuondoa vumbi la kutwa nzima, unamsubiri mumeo umevaa kagauni ka uchokozi , akija mumeo lazima hata kama amechoka vipi lazima atajipinda tu kukupa raha zako, lakini weee ndo kwanza anakukuta na tenge lako au kanga mama au hiyo night dress umeivaa siku tatu itaacha kunuka jasho? wakati yeye mwenyewe anajasho lake la kutoka kazini akukute na wewe huna tofauti hiyo appetite ataiotoa wapi?

  tabia ya mwanaume kila siku akuanze yeye anaweza dhani kwamba wewe humtamani yeye kama mumeo ila ni yeye tu mwenye shida na wee, which is not true, kuna wanawake wengine hata kumwambia mumewe nakupenda hawezi anasubiri mume aanze na yeye aseme' nakupenda pia' mwanamke unapojisikia kwamba nataka shughuli basi ushughulike bibiee. mrukie mumeo expolre his body en yours too, halafu uone kwamba haaamki, hapo sasa ndo upate pa kusemea.

  KABLA HATUJAWANYOOSHEA WANAUME VIDOLE TUJIANGALIE NA SISI WENYEWE JE? TUNAWATENDEA HAKI?
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,747
  Likes Received: 82,686
  Trophy Points: 280
  Umenifurahisha sana bibie, uliyoyasema ni kweli tupu. Nimeyaona sana haya ya wanawake kwenye ndoa kujisahau. Halafu njemba ikihamia nyumba ndogo wanaanza kulalama. Halafu mwanamke huyu huyu ambaye kwa mume wake hajitengenezi kama akipata nyumba ndogo yake basi vipodozi huwa kwa sana tu ili kuivutia zaidi nyumba ndogo yake. Sasa sijui hili ni aje la mdada kuweza 'kutafuta muda' wa kuhangaika na vipodozi kwa njemba wa nje lakini wakati huo huo nyumbani kwa mume wake amejiachia yuko nyukunyuku!
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mambo ya pakua ule, ukimaliza funika...
  Kwanini Wanawake hawawezi kujipakulia?
  ...au hakiliki? :D
   
 20. t

  tunza Member

  #20
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Habari yenyewe hii hapa:

  [​IMG]

Loading...