Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Chakula cha mchana makazini kina siri kubwa katika kuleta ufanisi. Wakati wa Ukoloni mashirika mengi ya watu binafsi yalitoa chakula cha mchana kwa wafanyakazi. Kwakua ubaguzi wakati ule ulikua ni wa wazi Wazungu ambao walikua ni wachache wenye nafasi za juu walitaarishiwa milo mizuri na kwa kiwango. Wazawa walitengenezewa wali maharage au ugali maharage.
Hata kama mfanyakazi atachangia kidogo katika chakula lakini ana uhakika wa kula mlo mmoja kwa siku. Wengine wana matatizo yao binafsi, nyumbani anaondoka hajakula kitu na mchana hana uwezo wa kununua chakula. Watu kama hawa wakipata mlo kazini mawazo yake yanakua katika uzalishaji.
Kupika chakula cha wafanyakazi si gharama kubwa kama kampuni inazalisha faida. Canteen unaweka wali nyama mchicha au ugali nyama mchicha, makande mchicha au chapati maharage au nyama.
Kibaruani kwetu kuna canteen ya wafanyakazi na wageni, bei si sawa na mtaani. Wamepunguza pakubwa, mfano wali nyama na mchicha 1,200.
Ingawa si shirika la mtu binafsi lakini nineona ni wazo zuri.
Waajiri mnapojaribu kutatua changamoto za maisha kwa wafanyakazi wenu inaleta tija. Wakoloni walijenga mpaka quarter’s na walivuna jasho la babu zetu kweli.