CHAKUA waitaka Serikali kuwabana wamiliki wa magari kugharamia majeruhi pindi gari lipatapo ajali

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
CfmuMt1WcAAEn5p.jpg

Chama cha kutetea haki za abiria nchini(CHAKUA),imeitaka serikali kuwabana wamiliki wa magari ya abiria,pindi magari yanapopata ajali na kusababisha majeruhi wa abiria,ili kuwagharimia matatibu na fidia.
2 (1).JPG

Mwenyekiti wa CHAKUA, Hassan Mchanjama

Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Hassan Mchanjama amesema kuwa, kutokuwa na usimamiaji wa kuridhisha kwa vyombo hivyo, imekuwa ukisababisha umekosaji wa haki za abiria pindi wanapopata ajali.

Bwana Mchajama amesema kuwa hali imekuwa ikisababisa malamiko mengi kutoka kwa wahanga wa ajali wa mabasi,na hata pindi wakati wakitaka kupewa haki zao wamekuwa wakizikosa.

Kwa upande mwingine amesema kuwa CHAKUA wamebaini kuwa watu wengi wanaopata ajali hukosa haki zao kufuatilia kutozijua sheria za usafiri.
 
Hata huyu naye anaonekana hazijui sheria, ndiyo maana kuna insurance ambazo zinacover mambo yote hayo na serikali inapata kodi zake
 
tunahitaji kupewa elimu na wanasheria kuhusu kudai fidia pale tunapopata ajali. wananchi wengi wanaishi na ulemavu wa kudumu na wamiliki wa kampuni za bima wanaendelea kutanua tu
 
Back
Top Bottom