Chain Of Command: Dkt. Mpango hajui mipaka yake

Labda mama anamuagiza mwenye nchi kwa chini amsaidie. Kila kiongozi na style yake mkuu. Nyerere alikuwa akimuagiza Kawawa halafu ambo yakiwa negative anamkana hadharani na Kawawa kwa utiifu wake hakuwahi mkosea Nyerere adabu hadi anastaafu.

Kawawa alpoagwa kustaafu utumishi wa umma Nyerere alitoa machhozi hadi akatamka" Kawawa asante sana ulibeba lawama zangu wewe miaka yote" Dr Mpango kwa utiifu wake na uadilifu wake anaweza akawa Kawawa wa SSH. KInyume chake atakuwa Lowassa wa Kikwete. Mabega hayajawahi kupanda .kuzidi kichaa.

Time will tell yeye ni nani. Bado mapema.
Ha haa wewe umenikumbusha mbaaaali, enzi za vijiji vya ujamaa Kawawa alipobebeshwa zigo la kufeli ule mpango wa villagisation.
 
Hicho cheo cha Makamu wa Rais ni cha kipuuzi but kipo kama Reserve tuu.

Hayo maagizo ni ya Rais na Waziri mkuu,yeye Kazi yake ni kuwakumbusha maneno ya Rais sio kutoa maagizo sijui maelekezo.

Rais Samia kipindi ni VP alikuwa akija ziarani haagizi unless aseme nimeelekezwa na Rais ,kama kuna jambo kaliona alikuwa anasema atalifikisha kwa Rais,sasa huyu wa sasa sijui Ana shida gani
Zile semina za Ngurdoto na kujulishana majukumu ya viongozi mbalimbali ni muhimu sana.
 
Wewe unataabika na nini juu ya hilo? Kuwa wewe unajua kuliko yeye?
Au unadhani amepata nafasi hiyo kwa kubahatisha?
Muache afanye kazi zake, hutaki, hama nchi.
Hakuna anayejua Kila kitu. Ndio maana tunakosoana. Hapa VP kakosea.
 
Kumbe humu jamvini kuna watu vilaza kweli2! MR ana mamlaka makubwa kumfuatia Rais sema wengi huwa ni wapole, lakini anaweza kuchukua hatua kwa kiongozi yoyote kasoro boss wake. Kama mambo hamyajui ulizeni siyo ujinga kufanya hivo!
Katiba Mkuu, Katiba. Hayo Mamlaka Mahsusi yako wapi nje ya Yale ya Muungano na Mazingira?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom