Chai kavu, ugali maharage mchana na usiku kila siku, kibaha cotc sawa si sawa????????????

Roxea

Senior Member
May 18, 2012
182
48
Habari za mchana wana jamvi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwanza napenda radhi ka kutokuwepo jamvini kwa kitambo kikubwa sana hii ni kkutokana kna ukweli kuwa maisha yamenihitaji kuwa very busy on the fields kuliko ofisini.
Back to the heading: Jana jumatatu tarehe 16/12/2103 wanachuo walikataa kuingia darasani na pia kula chakula, suala ambalo linaendelea mpaka leo. Kwa siku nzima ya jana, zilifanyika juhudi za hapa na pale ikiwa ni pamoja na kumtafuta Managing Director wa Shirika la elimu kibaha ambalo kimsingi chuo kipo chini ya shirika hilo la elimu kibaha ambaye alishindwa kutatua kero za wanafunzi hao maafisa tabibu watarajiwa.. Mpaka leo juhudi za kutatua kero hizo zinaendelea lakini muafaka bado haujapatikana na wanafunzi hao bado wanaendelea kutokubaliana na solution zinazotolewa... Kero zao ni pamoja na ada kupanda kila mwaka na pia kutoendana kwa ada hizo na huduma wanazopata wanafunzi hao ikiweno chakula, mfano wa chakula hicho ni chai kavu, ugali maharage mchana na jioni na pia gharama zinazojirudiarudi kama vitambulisho, dharura na michezo kila mwaka na matumizi yake hayaainishwi na kero nyinginezo nyingi...
 
ni kwamba zamani wizara ilikuwa inatumia wazabuni kutoa huduma ya chakula, lakini sasa kutokana na madeni makubwa kutoka kwa wazabuni, mfumo umebadilika, vyuo vinatumia catering services, sasa hawa wako kibiashara zaidi, ndiyo maana hayo yanatokea, chai kavu, maharage na ugali mchana na jioni
 
Wewe umeenda chuo kusoma au kula vizuri?unataka ule vizuri kwa ada gani yakutosha uliyoitoa wewe?embu someni huko acheni kuwaza kula vizuri kama vile mpo majumbani kwenu,na hapo utakuta nyie wengine mkiwa makwenu hata hiyo chai kavu hamnywagi.
 
Wampe hiyo ada yake shillingi1,000,000 kwa mwaka tuone kama ataweza kuandaa bajeti ya chakula ya mwaka mzima.Hebu endeleeni kugoma ili wawatimue ieleweke
 
kilaza wewe ungetaka raha ungesoma ukaenda kuchukua degree upate mkopo, ridhika na hicho maana nfo level yako, ustake raha, soma
 
hahahaha safi sana
 
ni kwamba zamani wizara ilikuwa inatumia wazabuni kutoa huduma ya chakula, lakini sasa kutokana na madeni makubwa kutoka kwa wazabuni, mfumo umebadilika, vyuo vinatumia catering services, sasa hawa wako kibiashara zaidi, ndiyo maana hayo yanatokea, chai kavu, maharage na ugali mchana na jioni

Katika vitu vya kipuuzi vya kuepuka kwa Mwanafunzi ni kugoma kwa ajili ya chakula. Wengi wataponzwa na mobu saikoloji lakini wakitimliwa kwa kila mmoja mmoja kuna baadhi watakoswa hata hicho wanachogomea wakiwa makwao.
 
...loh! kizazi cha bongoFlava mnapenda starehe kama paka!
...soma' acha kulalama...!
mna bahati kwa hivyo mnavyopata. "MNATAKIWA KUPIKIWA DONA NA MAHARAGWE YENYE WADUDU
 
Miss M4C hilo jina hali fanani na unachoongea ila kwa data nilozopata nikua kwa miaka 3 mfululizo kumekuwepo ongezeko la gharama za uchangiaji huku huduma zikishuka,
Mg: 2011~2012: huduma zilikua nzuri ma ada ilikua 300,000/=
2012~2013: huduma zilianza kuwa duni na ada ilipanda kuwa 850,000/=
2013~2014: huduma ndo kama heading inavosema na ada imepanda kufikia 1.2 Mill.
Cha kusikitisha zaidi gharama hizi zinapanda wanafunzi wakiwa chuoni tayari mf. Mwaka wa kwanza waliripoti chuoni wakiwa hawajui ada na michanganuo yake ikoje hata join instruction hawana mpaka sasa,kuna waraka ambao unaonyesha maongezeko hayo.
 
Inawezekana hujui vizuri unacho kiongea,
Please re-thinkand bring out an idea
 
Inawezekana hujui vizuri unacho kiongea,
Please re-thinkand bring out an idea

Kwa hiyo mnachotaka ni nini sasa?gharama za maisha zinapanda kila siku.unashangaa nini kuhusu ada sasa?ombeni mpewe hela yenu ya chakula muone kama itatosha.
 
kilaza wewe ungetaka raha ungesoma ukaenda kuchukua degree upate mkopo, ridhika na hicho maana nfo level yako, ustake raha, soma

Unafikiri ni utani Dadaa,walipokuwa O-level na A-Level badala ya kusoma kwa bidii wafaulu ili waeweze pata mkopo ili wajipangie bajeti zao wenyewe wao wanaleta ubishoo then wanafeli wakienda hivyo vyuo vyao ambavyo Msosi wa kengele wanajifanya kulalamika na wakati wengi wao wakiwa majumbani mwao hiyo chai kavu wanaisikiaga tuu kwa majirani.
 
Wampe hiyo ada yake shillingi1,000,000 kwa mwaka tuone kama ataweza kuandaa bajeti ya chakula ya mwaka mzima.Hebu endeleeni kugoma ili wawatimue ieleweke

Wewe mwache adundedunde kama kitenesi,kama wanaona ada yao haiendani na huduma wanayopata wagome kabisa ili Chuo kichukue maamuzi stahiki kwao.
 
Huenda mleta mada unahoja ya msingi.Ila kwa jinsi ulivyoileta ndo tatizo.Umeshindwa kuuelezea uma matatizo ya chuo yaliyopelekea wanafunzi kugoma na badala yake umeanza wanafunzi kugoma tena wamegomea ugal maharagwe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom