Chaguzi zote za CCM nilizoshudia, hazijawahi kukosa rushwa, kila kiongozi wa siasa iwe kwa kuteuliwa au kuchaguliwa, ni zao la rushwa

dolomon

JF-Expert Member
Jun 5, 2018
595
1,193
Nimeandika suala hili kwa kuanzia mbali sana...tangu nikiwa darasa la kwanza shule msingi kijijini kwetu.

Mwaka 1995 ndio Tanzania kama nchi tulifanya kwa mara ya kwanza uchaguzi wa vyama vingi vya siasa,mwaka huo nilikuwa ndio naanza la kwanza japo ki umri nilikuwa na miaka kumi,sema nilichelewa kuanza kusoma kwa vile nilikuwa nachunga kondoo,ndama na mbuzi wa baba,na hakukuwa na mtu, ikabidi nivute hadi nilipofikisha miaka takribani 10 ndio tukahamia kijijini kwa maana karibu na shule ili nisome..ulikuwa ni mpango na ahadi ya baba.

Nilipofika shule nilibahatika kupata rafiki mpya,mtoto wa mwalimu..sasa nikawa karibia muda wote nipo mazingira ya hapohapo shule na kucheza na watoto wenzangu.

Mwaka huo wa uchaguzi kulikuwa na zoezi la uandikishaji wapiga kura,watendaji wa vijiji na kata ndio walikuwa wanaandikisha wapiga kura hao,maana pale nilimuona mtendaji wa kijiji ndio alikuwa na zile kadi ambazo ndio zilikuwa kama kitambulisho...kwa wahenga wanajua hiki kitu ninachosema. Uandikishaji huo ulikuwa unafanyika pale shuleni....nadhani shule zilifungwa,maana asubuhi alifika na kuandikisha hadi jioni kisha anaondoka. Wakati wa kuondoka alituita na kumsaidia kuingiza dawati alilokuwa akitumia kuandikishia.

Sasa,kilichokuwa kinanishangaza, mtu akija kujiandikisha...anamwambia asichague vyama vingi,achague CCM, akichagua vyama vingi,vita itatokea...na alikuwa na bulungutu kubwa la pesa pembeni kwenye mfuko wa mariboro wa noti za tsh mia tano,zile zenye picha ya mtu anachuma karafuu kama mnaikumbuka. Sasa kila aliyejiandikisha, alimpatia pesa, japo kwa kumkadiria...kuna waliopata zaidi. Alifanya hivyo kila nilipokuwa nikimkuta hapo chini ya mti..na ilikuwa kwa kila mtu.

Nilikuja kujua baadaye kumbe ile ilikuwa ni RUSHWA,kwa hy hayati Mkapa alishinda uchaguzi kwa RUSHWA,nadhani hata na wale wabunge na madiwani kwa ujumla wake,rushwa na propaganda ya wapinzani wakishinda, vita itatokea.

Kimbembe mwaka huuu.....rushwa imetamalaki kupita maelezo, yaani wajumbe wamenunuliwa hadi laki 3 kwa mjumbe mmoja..

KUMMUNGA MKONO MGOMBEA YEYOTE WA CCM, NI KUUNGA MKONO RUSHWA.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom