Chaguzi zetu za kila mara hazina athari kwa uchumi wetu omba omba?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Taifa linaingia katika kipindi kigumu cha uchumi wetu kuwa tegemezi,tumeona deni la Taifa linaongezeka siku hadi siku toka tilioni 6 mwaka 2005 hadi kufikia tilioni 23 mwaka 2013.Matumizi yasiyo ya lazima yanaendelea kuitesa serikali yetu kwa kushindwa ama kwa makusudi kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali(tea allowance and hospitality).

Pamoja na sera mbovu za matumizi ya pesa za umma,serikali imeshindwa kusimamia taratibu na sheria ambazo zinaliingiza taifa katika majanga makusudi kwa kuwa tu serikali kupitia chama chake ina bariki misingi hiyo kuvunjwa.Taratibu za chaguzi zetu mbalimbali hapa nchi zinaendelea kuvunjwa kwa makusudi ikiwa ni pamoja na kanuni na sheria za uchaguzi kutokufutwa na kusababisha nchi kuingia kwenye mtego wa kufanya chaguzi mbalimbali huku ikishindwa kusimamia miradi ya maendeleo.

Mara ngapi tumeona taratibu na sheria za uchaguzi zinavunjwa kutokana na serikali kutumia rasilimali za umma katika chaguzi ambazo CCM ina mgombea wake.Tumeona mawaziri wakitumia rasilimali muda na kutumika katika chaguzi mbalimbali kama makampeni meneja katika majimbo na kata mbalimbali na kuacha kutumikia umma uliowaweka madarakani.

Tumeona safari zisizo za lazima za viongozi wetu kwenda na kurudi wakiwa wamebeba ahadi kem kem kutokana na mipangilio yao madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa koloni la mataifa makubwa kwa kukabidhi ardhi na rasilimali za taifa kwa misaada isiyo na tija.

Sipendi kusema napinga utawala wa kidemokrasia,najua fika gharama za demokrasia ni kubwa lakini tujikite katika kusimamia kanuni na sheria ili wagombea wawe ni hazina ya uongozi wa taifa kuliko kutumia muda na rasilimali za taifa katika kukiuka kwa makusudi kwa kuwa chaguzi zina halalisha matumizi mabya ya pesa za umma.

Nichukue fursa hii kuwaomba wadau wenzangu kuliangalia hili kwa kina ili tujue kuwa pamoja na gharama za demokrasia ni kubwa lakini tujikite zaidi katika kuzalisha mali ndani ya taifa kuliko serikali kupitia idara zake kuendelea kusimamia udhaifu wa vyombo hivyo husika katika kufikia malengo ya watu wachache wasio na nia nzuri na Tanzania
 
mkuu rais anatengeneza autobiograph ambayo ita base kwenye safari zake na picha alizopiga na akina 50cent na zile alipokabidhiwa jezi na timu za ulaya ila tuvumilie kwasababu hi pepo la magamba litapita tu!
 
je chaguzi hizi haziathiri uchumi wetu?maana tuna lazimishwa kufanya uchaguzi kama sehemu ya deal za wakubwa
 
Back
Top Bottom