Chaguzi za serikali za mitaa ziwe bakora kwa watawala dhalimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chaguzi za serikali za mitaa ziwe bakora kwa watawala dhalimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jun 6, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Chaguzi za serikali za mitaa zinategemea kufanyika nchi nzima mnamo tarehe 26/6/2012.Hii inatokana na serikali kugawa mitaa mipya ambayo hapo nyuma haikuwepo,lengo kuu ni kufikisha huduma za jamii kwa ukaribu.Kuna baadhi ya mitaa imegawanywa kisiasa zaidi kuliko mahitaji asilia.Lakini lengo hasa la mada hii si kugawanywa kwa mitaa bali uchaguzi huu uwe na changamoto zipi kufikia malengo ya watawala kuwaheshimu wapiga kura.

  Kwanza uchaguzi huu hautatumia vitambulisho vya mpiga kura kama tulivyokwish zoea.Utaratibu utakao tumika ni wa kujiandikisha kama mkazi wa sehemu husika,sifa kuu ni kuwa mkazi wa mtaa unapofanyika uchaguzi.Hivyo basi natumia nafasi hii kuwasihi wakazi wa maeneo husika kutumia haki yao ya kikatiba kujiandikisha ili wapate sifa ya mpiga kura katika chaguzi hizi.

  Pia ni fursa kwa wale ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura kutokana na kutofikia umri ulioruhusiwa kisheria.Pili fursa hii ni majukumu ya mpiga kura kutumia haki yake kikatiba ya kutoa dhamana kwa kiongozi atayeona anamfaa kwa kipindi cha miaka mitano.Fursa hii itumike vizuri katika kurekebisha makosa uliyoyafanya kutokana na kuchagua watu kiushabiki bila kujali mustakabali wa maisha yao.

  Kama ulichagua kiongozi kwa mategemeo ya kukutumikia katika ustawi wa maendeleo ya jamii husika na mtu huyu akageuka Mungu mtu basi,hii ndiyo fursa pekee ya kufanya maamuzi thabiti.Epukeni kupewa 5000/- kwa kipindi chote cha miaka mitano,ambayo kihesabu utakuwa umeuza haki yako ya msingi kwa shilingi 1000/- kila mwaka ambayo ni sawa na shilingi mbili na senti sabini na nne(2.74) kwa siku.

  Uchaguzi huu uwe ndiyo fimbo ya kuwachapia wale wote waliotumia kiti hiki cha mwenyekiti kama mradi binafsi wa kukusanya mapato ya kuendesha familia zao, kwa kuwachangisha wananchi pesa za kuandikiwa barua za dhamana mahakamani ama barua za utambulisho wa mkazi kwa kina mama wanaomba mikopo ya ukandamizi isiyo na tija katika kuendesha shughuli zao za kimaisha.

  Ni wakati wa kutafakari aina ya kiongozi bora na kufanya maamuzi yasiyo na shinikizo bila kujali vitisho toka kwa watawala.Kura yako iwe bakora kwa watawala waliojifanya Mungu watu na kusahau kuwa cheo ni dhamana.

  Udhalimu wa watawala huishia pale chaguzi zinapofikia.Mtaahidi ahadi kem kem ikibidi hata kupigiwa magoti.Mtakuwa wafalme kwa kipindi kifupi lakini madhara yake mtayapata mara baada ya uchaguzi.Mtasomewa mapato na matumizi japokuwa hamkuwahi kusomewa toka mlipo wachagua.

  Mwisho wana JF nakaribisha mchango wa mawazo kuwatahadharisha wapiga kura na kutumia uchaguzi kama bakora kwa viongozi madhalimu katika kuelekea kuipata Tanzania tuitakayo.Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  ungeweka na sehemu zinazotarajiwa ingekuwa njema
   
Loading...