Chaguzi za CCM na tambo za waumini wapya

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
634
1,000
Nianze Kwa nukuu ifuatayo kutoka Kwa gwiji Jenerali Ulimwengu, wakati huo akimjibu Daniel Nswanzugwako, baada ya kutoka NCCR Mageuzi na kujiunga ccm huku akiwabeza waliokuwa wakihoji mwenendo ndani ya CCM.

Jenerali ulimwengu aliandika" ni kawaida Kwa waumini wa imani au dhehebu jipya, kuwa na msimamo mkali pengine zaidi hata ya makasisi wa imani hizo'.

Nimelazimika kuibuka na hitimisho hilo kutokana na chaguzi za ndani ya ccm zilivyokumbwa na vitendo vya hovyo, hasa rushwa.

Vitendo hivi vimefanyika huku kukiwa na waumini wapya waliojiunga ccm Kwa maelezo ya kuwa wapinzanj hawana hoja tena kwani CCM chini ya magufuli imebadilika!.

Vitendo vya rushwa vimetamalaki kila kona ya nchi, ndani ya uchaguzi wa ccm na jumuiya zake, lakini waumini wapya hawaoni!

Ndio maana kuna watu wanahoji kuwa kwaninj wananchi wa kawaida hawayaoni na kujiunga na imani mpya kama hawa waliokuwa viongozi waandamizi wa upinzani?
 

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
634
1,000
Hahaha, sikio la kufa..... Mwingine naye kajitoa naye saa hizi huku akiimba mapambio zaidi ya makuhani walioko!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom