Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
Kwanza kwa unyenyekevu mkubwa naomba msinielewe vibaya kwa kuanza na kichwa chenye ukakasi kiasi, nikaonekana natumia lugha mbaya.Ujinga ni hali ambayo inaweza kuondolewa kwa kuelimishwa, so it is not a permanent condition na isieleweke kuwa ni tusi.
Nimekuwa naangalia chaguzi ndogo kwa jicho la pili, na kujaribu kuwa realists na sio idealist. Nimefanya hivi kwa kuangalia gharama na manufaa yake, na kufikia hitimisho kuwa hizi changuzi ni kama mtindo fulani wa kutwisha mzigo wavuja jasho kuwanufaisha wanasiasa, na kuwafurahisha wahisani na jumuiya ya nchi za magharibi. Yaani ni kama tunalipia bili ya mtu ambaye anajiburudisha kwa mchezo wa kisiasa.
Kwanza nimejiuliza: Kwanini kila uchaguzi mdogo unapotokea, fedha za kuugharamia hazijawahi kukosekana? Kila ukisikia uchaguzi mdogo katika jimbo fulani, fedha zinakuwa tele. Lakini kwenye majimbo hayo hayo ya uchaguzi, unaweza kusikia fedha ambazo ni pungufu ya zile zinazotumika kugharamia uchaguzi, zinakosekena kwenye miradi kama ya ujenzi wa zahanati, madaraja, barabara, umeme, maji, shule etc …
Najiuliza kama ni kweli huwa zinakosekana au si kweli, au hali halisi ni kuwa mambo hayo yanayowagusa wananchi sio kipaumbele kama ilivyo kwa mambo ya siasa. Inawezekana sina busara za kutosha kujua hekima iliyomo ndani ya jambo hili. But I do believe we can find our own formular which can be acceptable to vyama vyote bila kufuja hela kwenye bi-elections ambazo kimsingi hazibadilishi mwelekeo wa bunge.
Pili, kwa mtu mwenye akili timamu kwa sasa atajua kabisa kuwa chaguzi ndogo zote iwe kwa Nassari, kwa Lissu au kwingine kokote, mshindi atakuwa mgombea wa CCM. Matokeo yatakuwa hiyo… kama kuna mtu atabisha basi aseme… lakini swali langu ni kuwa kwa nini tutumie mapesa mengi kwenye kufanya kitu ambacho tayari matokeo yake tunayajua? Kwanini tuzitumie akili na busara ya kutafuta njia ya kuweka mtu wa CCM, halafu pesa zote hizo tutumie kwenye jambo la kijamii litakalowanufaisha wanajimbo wote kwa muda mrefu? Au ni kwamba tunafanya mizungu kuwafurahisha wazungu wakati tunaoumia ni walipa kodi? Ninachokiona ni kuwa chaguzi hizo hazifanywi kwa ajili ya wanajimbo, au kwa ajili ya Tanzania, ni chaguzi kwa ajili ya kufurahisha nchi za magharibi, lakini kwa gharama zetu. Kweli inauma sana.
Tatu, tukiangalia mbali zaidi…in realistic terms … 2020 mshindi atakuwa mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais, labda Bunge litakuwa asilimia 90 CCM, asilimia 10 upinzani, more or less. Tujaribu kuangalia pesa zitakazotumika kwenye jambo hili ambalo tayari kimsingi liko wazi. Swali ni je, ina maana tumeshindwa kutafuta njia zetu wenyewe watanzania za gharama nafuu kufanikisha hilo? Hela ambazo zinagharamia uchaguzi zingeenda kwenye maendeleo ya jamii, naamini ingekuwa ni matumizi mazuri ya fedha kwa manufaa ya muda mrefu.
Mwanzo kabisa nimejitaja kuwa mimi ni realist na sio idealist. Kwa hiyo niseme wazi tu kuwa demokrasia ya uchaguzi hapa Tanzania naiona kama ni mizungu kwa ajili ya wazungu. Ni bora tufute ujinga, na hizo pesa tunazopeleka kwenye uchaguzi zitumike kwenye maendeleo kwenye majimbo. Bora mizungu kwa ajili ya maendeleo yetu, kuliko kwa wazungu.