Chaguzi ndogo na "ujinga" wetu watanzania

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,030
2,000
Kwanza kwa unyenyekevu mkubwa naomba msinielewe vibaya kwa kuanza na kichwa chenye ukakasi kiasi, nikaonekana natumia lugha mbaya.Ujinga ni hali ambayo inaweza kuondolewa kwa kuelimishwa, so it is not a permanent condition na isieleweke kuwa ni tusi.

Nimekuwa naangalia chaguzi ndogo kwa jicho la pili, na kujaribu kuwa realists na sio idealist. Nimefanya hivi kwa kuangalia gharama na manufaa yake, na kufikia hitimisho kuwa hizi changuzi ni kama mtindo fulani wa kutwisha mzigo wavuja jasho kuwanufaisha wanasiasa, na kuwafurahisha wahisani na jumuiya ya nchi za magharibi. Yaani ni kama tunalipia bili ya mtu ambaye anajiburudisha kwa mchezo wa kisiasa.

Kwanza nimejiuliza: Kwanini kila uchaguzi mdogo unapotokea, fedha za kuugharamia hazijawahi kukosekana? Kila ukisikia uchaguzi mdogo katika jimbo fulani, fedha zinakuwa tele. Lakini kwenye majimbo hayo hayo ya uchaguzi, unaweza kusikia fedha ambazo ni pungufu ya zile zinazotumika kugharamia uchaguzi, zinakosekena kwenye miradi kama ya ujenzi wa zahanati, madaraja, barabara, umeme, maji, shule etc …

Najiuliza kama ni kweli huwa zinakosekana au si kweli, au hali halisi ni kuwa mambo hayo yanayowagusa wananchi sio kipaumbele kama ilivyo kwa mambo ya siasa. Inawezekana sina busara za kutosha kujua hekima iliyomo ndani ya jambo hili. But I do believe we can find our own formular which can be acceptable to vyama vyote bila kufuja hela kwenye bi-elections ambazo kimsingi hazibadilishi mwelekeo wa bunge.

Pili, kwa mtu mwenye akili timamu kwa sasa atajua kabisa kuwa chaguzi ndogo zote iwe kwa Nassari, kwa Lissu au kwingine kokote, mshindi atakuwa mgombea wa CCM. Matokeo yatakuwa hiyo… kama kuna mtu atabisha basi aseme… lakini swali langu ni kuwa kwa nini tutumie mapesa mengi kwenye kufanya kitu ambacho tayari matokeo yake tunayajua? Kwanini tuzitumie akili na busara ya kutafuta njia ya kuweka mtu wa CCM, halafu pesa zote hizo tutumie kwenye jambo la kijamii litakalowanufaisha wanajimbo wote kwa muda mrefu? Au ni kwamba tunafanya mizungu kuwafurahisha wazungu wakati tunaoumia ni walipa kodi? Ninachokiona ni kuwa chaguzi hizo hazifanywi kwa ajili ya wanajimbo, au kwa ajili ya Tanzania, ni chaguzi kwa ajili ya kufurahisha nchi za magharibi, lakini kwa gharama zetu. Kweli inauma sana.

Tatu, tukiangalia mbali zaidi…in realistic terms … 2020 mshindi atakuwa mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais, labda Bunge litakuwa asilimia 90 CCM, asilimia 10 upinzani, more or less. Tujaribu kuangalia pesa zitakazotumika kwenye jambo hili ambalo tayari kimsingi liko wazi. Swali ni je, ina maana tumeshindwa kutafuta njia zetu wenyewe watanzania za gharama nafuu kufanikisha hilo? Hela ambazo zinagharamia uchaguzi zingeenda kwenye maendeleo ya jamii, naamini ingekuwa ni matumizi mazuri ya fedha kwa manufaa ya muda mrefu.

Mwanzo kabisa nimejitaja kuwa mimi ni realist na sio idealist. Kwa hiyo niseme wazi tu kuwa demokrasia ya uchaguzi hapa Tanzania naiona kama ni mizungu kwa ajili ya wazungu. Ni bora tufute ujinga, na hizo pesa tunazopeleka kwenye uchaguzi zitumike kwenye maendeleo kwenye majimbo. Bora mizungu kwa ajili ya maendeleo yetu, kuliko kwa wazungu.
 
joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
3,693
2,000
Mkubwa joshydama kweli hili hata tukisema tulaumiane haitasaidia sana. Ni kuwashawishi wenzetu kukubaliana na ukweli kuwa tunapoteza pesa kwenye mambo ambayo hayana tija.

Pesa za uchaguzi zikijenga shule moja ya kisasa ni bora sana. Tunaweza kulaumu Katiba, lakini siamini kama ikibadilika itabadilisha jambo hili.
Mkuu, hakika nakwambia watanzania tungekuwa tunajitambua we could raise red flag na seriakli ingeshituka kwa kiasi Fulani kuhusiana na suala linaloendelea. kwa sababu ya uoga ambao unasababishwa na ujinga na upumbavu ndiyo maana unaona kodi zetu zinatumika vibaya and we can't even hoji kuhusu hayo matumizi mabaya ya fedha.

Kodi za wananchi kutumika vibaya sisi ndiyo chanzo maana ndivyo tunavyowalea viongozi wetu na ndiyo maana viongozi hawana uoga hata kidogo kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika mambo ambayo hayana tija kwa wananchi na kuyaweka pembeni mambo ambayo ni ya msingi.
 
Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
1,859
2,000
Kwanza kwa unyenyekevu mkubwa naomba msinielewe vibaya kwa kuanza na kichwa chenye ukakasi kiasi, nikaonekana natumia lugha mbaya.Ujinga ni hali ambayo inaweza kuondolewa kwa kuelimishwa, so it is not a permanent condition na isieleweke kuwa ni tusi.

Nimekuwa naangalia chaguzi ndogo kwa jicho la pili, na kujaribu kuwa realists na sio idealist. Nimefanya hivi kwa kuangalia gharama na manufaa yake, na kufikia hitimisho kuwa hizi changuzi ni kama mtindo fulani wa kutwisha mzigo wavuja jasho kuwanufaisha wanasiasa, na kuwafurahisha wahisani na jumuiya ya nchi za magharibi. Yaani ni kama tunalipia bili ya mtu ambaye anajiburudisha kwa mchezo wa kisiasa.

Kwanza nimejiuliza: Kwanini kila uchaguzi mdogo unapotokea, fedha za kuugharamia hazijawahi kukosekana? Kila ukisikia uchaguzi mdogo katika jimbo fulani, fedha zinakuwa tele. Lakini kwenye majimbo hayo hayo ya uchaguzi, unaweza kusikia fedha ambazo ni pungufu ya zile zinazotumika kugharamia uchaguzi, zinakosekena kwenye miradi kama ya ujenzi wa zahanati, madaraja, barabara, umeme, maji, shule etc …

Najiuliza kama ni kweli huwa zinakosekana au si kweli, au hali halisi ni kuwa mambo hayo yanayowagusa wananchi sio kipaumbele kama ilivyo kwa mambo ya siasa. Inawezekana sina busara za kutosha kujua hekima iliyomo ndani ya jambo hili. But I do believe we can find our own formular which can be acceptable to vyama vyote bila kufuja hela kwenye bi-elections ambazo kimsingi hazibadilishi mwelekeo wa bunge.

Pili, kwa mtu mwenye akili timamu kwa sasa atajua kabisa kuwa chaguzi ndogo zote iwe kwa Nassari, kwa Lissu au kwingine kokote, mshindi atakuwa mgombea wa CCM. Matokeo yatakuwa hiyo… kama kuna mtu atabisha basi aseme… lakini swali langu ni kuwa kwa nini tutumie mapesa mengi kwenye kufanya kitu ambacho tayari matokeo yake tunayajua? Kwanini tuzitumie akili na busara ya kutafuta njia ya kuweka mtu wa CCM, halafu pesa zote hizo tutumie kwenye jambo la kijamii litakalowanufaisha wanajimbo wote kwa muda mrefu? Au ni kwamba tunafanya mizungu kuwafurahisha wazungu wakati tunaoumia ni walipa kodi? Ninachokiona ni kuwa chaguzi hizo hazifanywi kwa ajili ya wanajimbo, au kwa ajili ya Tanzania, ni chaguzi kwa ajili ya kufurahisha nchi za magharibi, lakini kwa gharama zetu. Kweli inauma sana.

Tatu, tukiangalia mbali zaidi…in realistic terms … 2020 mshindi atakuwa mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais, labda Bunge litakuwa asilimia 90 CCM, asilimia 10 upinzani, more or less. Tujaribu kuangalia pesa zitakazotumika kwenye jambo hili ambalo tayari kimsingi liko wazi. Swali ni je, ina maana tumeshindwa kutafuta njia zetu wenyewe watanzania za gharama nafuu kufanikisha hilo? Hela ambazo zinagharamia uchaguzi zingeenda kwenye maendeleo ya jamii, naamini ingekuwa ni matumizi mazuri ya fedha kwa manufaa ya muda mrefu.

Mwanzo kabisa nimejitaja kuwa mimi ni realist na sio idealist. Kwa hiyo niseme wazi tu kuwa demokrasia ya uchaguzi hapa Tanzania naiona kama ni mizungu kwa ajili ya wazungu. Ni bora tufute ujinga, na hizo pesa tunazopeleka kwenye uchaguzi zitumike kwenye maendeleo kwenye majimbo. Bora mizungu kwa ajili ya maendeleo yetu, kuliko kwa wazungu.
Mtoa mada umesahau kitu kimoja! Kama tuamua kuacha kufanya uchaguzi huo, basi CCM watajisahau na kuweka mtu wao yeyote ambaye hatahitaji kuwajibika saana kwa hao wananchi! Na hii italeta vurugu nyingine ya kupachina maajina ya watu hata wasiotosheleza kubeba majukumu hayo. Ilivyo sasa japokuwa % kubwa ushindi unaelekea kwa CCM, CCm wanavyanye 'veting' ya kutosha ili yule wanayepleka kwa wananchi awe na kukubalika kwao. Kwani kama watapeleka tu yyeyote, kazi inaweza kuwa ngumu sana kupata ushindi kwa CCM! Hivyo chakuzi ndogo kwa muktaza huu haziepukiki!
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,942
2,000
Mkubwa joshydama kweli hili hata tukisema tulaumiane haitasaidia sana. Ni kuwashawishi wenzetu kukubaliana na ukweli kuwa tunapoteza pesa kwenye mambo ambayo hayana tija.

Pesa za uchaguzi zikijenga shule moja ya kisasa ni bora sana. Tunaweza kulaumu Katiba, lakini siamini kama ikibadilika itabadilisha jambo hili.
Mkuu tatizo lote liko ndani ya katiba. Kwenye katiba ambayo rais hashitakiwi kwa kosa lolote akiwa madarakani, kwa vyovyote amri yake inakuwa na nguvu kuliko katiba. Katiba yetu inatoa nguvu kubwa isiyo na msingi kwa rais, ikitegemea rais atakuwa na busara. Hizi chaguzi na matokeo unayoyaona sasa ni matokeo ya nguvu isiyo na sababu ya rais.

Matokeo haya unayosema kiunyonge kwamba ccm inashinda na ni matokeo yanayojulikana ujue huko ni kuidhinisha dhuluma. Je unajua madhara ya kubariki dhuluma? Unadhani hiki anachokifanya rais huyu kisa ana mamlaka kinapaswa kupewa baraka za maneno ya kupotosha kwa kusema tunawaridhisha wazungu? Nimefedheheka kuona mtu muelewa kama ww unaongea kuhalilisha haramu kisa mshindi anafahamika, huku ukijua fika sio mshindi anayepatikana kihalali.
 
ROMUARD KYARUZI

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
684
500
Umasikini na ujinga ni vikwazo kwa maendeleo ya demokrasia.Bado wapo wanaoamini kuwa viongozi uchaguliwa na Mungu hata kama amepita through wizi wa kura .Watu kama hawa hawapigi kura wanadai atakayechaguliwa ni huyo huyo.
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
6,209
2,000
Mkuu ni kwamba upumbavu ni zao la kutokuwa na maarifa. Maarifa yanakusaidia ujitambue kwa kiasi kikubwa sana. Ukikiosa maarifa hakika ndipo suala la ujinga na upumbavu huwa linakuja. Pindi utakapokuwa mjinga/mpumbavu hakika utashindwa kuhoji hata pale unapoona mambo hayaendi sawa kwa sababu ujinga na upumbuvu huambatana na uoga.
Mkuu maarifa gani unazungumzia na yanapatikana vipi? Hivi viongozi wa institutions za serikali kuside na chama badala ya nchi inatokana na kukosa maarifa kweli au ni upumbuvu wa kuzaliwa nao,sasa Kama mtu anaweza kusoma mpaka kiwango cha master degree,akapanda cheo mpaka kufikia level ya CDF au IGP na still akawa hana maarifa ya kumuwezesha kujua nani amtumikie kati ya nchi na watu wake au aliyemteua na chama chake basi tunatatizo kubwa kama taifa
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
18,921
2,000
Kwani hatuwezi kutafuta utaratibu mwingine wa kuchagua viongozi, ambao hauhusishi vyama vya siasa? kama CCM ni tatizo, tukumbuke kuwa ni chama cha siasa, kikija kingine nacho kitakuwa tatizo...itakuwa ni kurudi pale pale.
Ni vigumu sana ndugu yangu, watu wanatamani mno lakini mazingira ni magumu sana; CCM inalijua hili hivyo inahakikisha kila sehemu wameweka makada wao kuanzia vyombo vya usalama, wakuu wa mikoa na wilaya, Wakurugenzi wa local government pia ni makada watiifu...na kwenda mbali zaidi wamepandikiza hadi vyama vya upinzani vinavyo riport kwao..

Ni kazi ngumi mno na unavyowajua watanzania wanabakia kununghunika tu pembeni...

Kwa mfano kiuhakisia kabisa hakuna mtanzania anayefurahia maisha haya kwa sasa!! Hayupo...na ukimwona anajitokeza kifuambele basi anajua anapata chochote kitu si bure.

Safari ni ndefu..Jua ni kali ..ila tusikate tamaa....wacha tuone dk zado zipo...
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,030
2,000
Mkuu tatizo lote liko ndani ya katiba. Kwenye katiba ambayo rais hashitakiwi kwa kosa lolote akiwa madarakani, kwa vyovyote amri yake inakuwa na nguvu kuliko katiba. Katiba yetu inatoa nguvu kubwa isiyo na msingi kwa rais, ikitegemea rais atakuwa na busara. Hizi chaguzi na matokeo unayoyaona sasa ni matokeo ya nguvu isiyo na sababu ya rais.

Matokeo haya unayosema kiunyonge kwamba ccm inashinda na ni matokeo yanayojulikana ujue huko ni kuidhinisha dhuluma. Je unajua madhara ya kubariki dhuluma? Unadhani hiki anachokifanya rais huyu kisa ana mamlaka kinapaswa kupewa baraka za maneno ya kupotosha kwa kusema tunawaridhisha wazungu? Nimefedheheka kuona mtu muelewa kama ww unaongea kuhalilisha haramu kisa mshindi anafahamika, huku ukijua fika sio mshindi anayepatikana kihalali.
Mkuu baada ya uchaguzi tukifanya cost benefit analysis utakuja kujua kuwa i am more realaistic. Ni bora kuwe na njia ya sisi kunufaika na hizo hela, kuliko kuwanufaisha wanasiasa.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,942
2,000
Mkuu baada ya uchaguzi tukifanya cost benefit analysis utakuja kujua kuwa i am more realaistic. Ni bora kuwe na njia ya sisi kunufaika na hizo hela, kuliko kuwanufaisha wanasiasa.
Bila hata huo uchaguzi, wanasiasa ndio wanaofaidi hizo hela. Mfano mrahisi mfaninishe Polepole ambaye ni katibu mwenyezi wa ccm linganisha na daktari bingwa. Hapo ni bila uchaguzi. Angalia malipo ya mbunge, fafanisha na mtaalamu yoyote unayemjua.
 
Dharra

JF-Expert Member
Jun 23, 2017
1,611
2,000
ikiwa akili ya Mtanzania inaanza kujadili ushindi wa ccm kabla ya chaguzi kufanyika, tukiri tu tumefikia hatua mbaya sana, kwamba mtu anatoa hadi asilimia ya ushindi kumpa huyu na asilimia ya kushindwa kumpa yule!!!! halafu anatetea yeye ni m realistic kweli!!!! Naamini kabisa kauli ya kiongozi mmoja wa dini kuwa Watanzania walio wengi sasa tumebaki kupiga ramli tu, Tupo hatarini sana.
 
Blackman

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
752
250
Cheap is expensive yes, but new is even more expensive. Ukweli ni kuwa ni hatari kuwanyima watu haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Lakini kama kiongozi atakayechaguliwa tayari tunamfahamu, kwanini asisimikwe tu, na hizo hela tutumie kwenye mengine kama maji, dawa, barabara ... ?
wazo lako baya
 
Blackman

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
752
250
Mkuu baada ya uchaguzi tukifanya cost benefit analysis utakuja kujua kuwa i am more realaistic. Ni bora kuwe na njia ya sisi kunufaika na hizo hela, kuliko kuwanufaisha wanasiasa.
Kwa mfano huo uchaguzi usipofanyika una uhakika gani kuwa hizo pesa zitaelekezwa kwenye kwenye miradi?
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
9,107
2,000
Ndio Maisha tuliyochagua! Tuishi tu siku tukiyachoka tutabadilika
 
Phinias Oyugi

Member
Sep 3, 2016
5
20
kibongo bongo tunaona poa sana lakini madhara yake sijui, bila shaka katika kipindi hiki ambacho nchi hii inawasomi wengi wanaoweza ona jambo kama hiki wakalitorea ufafanuzi na ushauri watu wakapata kufahamu. Kwanini tuharibu pesa zinazokusanywa kwa mbinde na wasomi wetu hawa wachache katika style isio rasmi sana......?
 
NorthJuu

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
387
250
ikiwa akili ya Mtanzania inaanza kujadili ushindi wa ccm kabla ya chaguzi kufanyika, tukiri tu tumefikia hatua mbaya sana, kwamba mtu anatoa hadi asilimia ya ushindi kumpa huyu na asilimia ya kushindwa kumpa yule!!!! halafu anatetea yeye ni m realistic kweli!!!! Naamini kabisa kauli ya kiongozi mmoja wa dini kuwa Watanzania walio wengi sasa tumebaki kupiga ramli tu, Tupo hatarini sana.
cyo ramli, wala ramli chonganishi, mtoa mada anaongea fact. Ni ufujaji wa hela za mlipa kodi, chama kitakachotoa washindi ni cha muunganiko wa TANU na ASP.
 
Ankazominiotra

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
607
500
Tabia ya watanzania kuwa makondoo ni mifumo ya maisha inayowalea kuanzia kwenye familia hadi shuleni.

Mtoto anakulia katika mazingira ya kumjaza uoga hadi anakuwa mtu mzima ni mtu hasiyejiamini.

Ili kuweza kubadili huu ujinga wa watanzania wengi ni lazima mabadiliko yaanzie ngazi ya familia. Demokrasia ya kweli ianzie kwenye familia zetu.
Umeeleza kwa ufupi lakini hukuacha kitu, mwenye akili na atambue. Umefunga mjadala.
 
BenKaile

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
448
500
Kwanza kwa unyenyekevu mkubwa naomba msinielewe vibaya kwa kuanza na kichwa chenye ukakasi kiasi, nikaonekana natumia lugha mbaya.Ujinga ni hali ambayo inaweza kuondolewa kwa kuelimishwa, so it is not a permanent condition na isieleweke kuwa ni tusi.

Nimekuwa naangalia chaguzi ndogo kwa jicho la pili, na kujaribu kuwa realists na sio idealist. Nimefanya hivi kwa kuangalia gharama na manufaa yake, na kufikia hitimisho kuwa hizi changuzi ni kama mtindo fulani wa kutwisha mzigo wavuja jasho kuwanufaisha wanasiasa, na kuwafurahisha wahisani na jumuiya ya nchi za magharibi. Yaani ni kama tunalipia bili ya mtu ambaye anajiburudisha kwa mchezo wa kisiasa.

Kwanza nimejiuliza: Kwanini kila uchaguzi mdogo unapotokea, fedha za kuugharamia hazijawahi kukosekana? Kila ukisikia uchaguzi mdogo katika jimbo fulani, fedha zinakuwa tele. Lakini kwenye majimbo hayo hayo ya uchaguzi, unaweza kusikia fedha ambazo ni pungufu ya zile zinazotumika kugharamia uchaguzi, zinakosekena kwenye miradi kama ya ujenzi wa zahanati, madaraja, barabara, umeme, maji, shule etc …

Najiuliza kama ni kweli huwa zinakosekana au si kweli, au hali halisi ni kuwa mambo hayo yanayowagusa wananchi sio kipaumbele kama ilivyo kwa mambo ya siasa. Inawezekana sina busara za kutosha kujua hekima iliyomo ndani ya jambo hili. But I do believe we can find our own formular which can be acceptable to vyama vyote bila kufuja hela kwenye bi-elections ambazo kimsingi hazibadilishi mwelekeo wa bunge.

Pili, kwa mtu mwenye akili timamu kwa sasa atajua kabisa kuwa chaguzi ndogo zote iwe kwa Nassari, kwa Lissu au kwingine kokote, mshindi atakuwa mgombea wa CCM. Matokeo yatakuwa hiyo… kama kuna mtu atabisha basi aseme… lakini swali langu ni kuwa kwa nini tutumie mapesa mengi kwenye kufanya kitu ambacho tayari matokeo yake tunayajua? Kwanini tuzitumie akili na busara ya kutafuta njia ya kuweka mtu wa CCM, halafu pesa zote hizo tutumie kwenye jambo la kijamii litakalowanufaisha wanajimbo wote kwa muda mrefu? Au ni kwamba tunafanya mizungu kuwafurahisha wazungu wakati tunaoumia ni walipa kodi? Ninachokiona ni kuwa chaguzi hizo hazifanywi kwa ajili ya wanajimbo, au kwa ajili ya Tanzania, ni chaguzi kwa ajili ya kufurahisha nchi za magharibi, lakini kwa gharama zetu. Kweli inauma sana.

Tatu, tukiangalia mbali zaidi…in realistic terms … 2020 mshindi atakuwa mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais, labda Bunge litakuwa asilimia 90 CCM, asilimia 10 upinzani, more or less. Tujaribu kuangalia pesa zitakazotumika kwenye jambo hili ambalo tayari kimsingi liko wazi. Swali ni je, ina maana tumeshindwa kutafuta njia zetu wenyewe watanzania za gharama nafuu kufanikisha hilo? Hela ambazo zinagharamia uchaguzi zingeenda kwenye maendeleo ya jamii, naamini ingekuwa ni matumizi mazuri ya fedha kwa manufaa ya muda mrefu.

Mwanzo kabisa nimejitaja kuwa mimi ni realist na sio idealist. Kwa hiyo niseme wazi tu kuwa demokrasia ya uchaguzi hapa Tanzania naiona kama ni mizungu kwa ajili ya wazungu. Ni bora tufute ujinga, na hizo pesa tunazopeleka kwenye uchaguzi zitumike kwenye maendeleo kwenye majimbo. Bora mizungu kwa ajili ya maendeleo yetu, kuliko kwa wazungu.
SWALA LA UCHAGUZI LITABAKI PALE PALE EITHER LIWE LA KIMIZENGWE AU NAMNA SAHIHI. CHAGUZI NI SWALA LA KIDEMOKRASIA KWA JAMII INAYOAMINI USHIRIKI WA MWANANCHI KUCHAGUA KIONGOZI MWAKILISHI AU YEYE BINAFSI KUPATA FURSA YA KUWAKILISHA JAMII YAKE KWAHIYO KUFUTWA AU UCHAGUZI USIFANYIKE NI KISOCHOINGIA AKILINI KWANI TAIFA LETU SIO LA KIFALME/UMALKIA, TUNAONGOZWA NA KATIBA NA SHERIA ZINAZOLINDA UHURU WETU.
 
cosmonaut

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
1,251

Mkuu hapo TU ndipo ambapo waafrica tunazingua kwenye kukariri kuwa demokrasia Ni uchaguzi TU(Tena kwenye nafasi za uongozi wasiasa)...

Wakati nguzo za utawala wa sheria, uwajibikaji, Uhuru wa maoni, uwazi, na nk Ni vya muhimu vyote vitekelezwe kwa kiwango Cha juu ili kuhakikishwa maslahi ya walio wengi wanafikiwa bila kuwaminya/ kuwaonea wale wachache....

KATIBA Ni misingi ambayo watu Kama taifa wanajiwekea ili itoe miongozo wa namna inchi na taifa litakavyo ongozwa na kusimamia au kufuata matakwa na maslahi ya watu)raia.
Ukiangalia utaona maneno muhimu ni Miongozo, kusimamia Masilahi/matakwa ya watu,
HIVYO kama kitu chochote kitakachokua kianenda kinyume na KATIBA(kupingana na Masilahi ya walio wengi)basi kitakuwa batili.
kwakuwa maslahi au matakwa ya watu/raia hubadilika baada ya muda/miaka hivyo ni vema KATIBA ikawa inafanyiwa marekebisho inapobdi au kuindaa upya kabisa pale inapokuwa inamapungufu makubwa na mengi Sana yanayo tishia utawi wa masilahi na matakwa ya watu husika....
************"
Sasa basi tunaposema demokrasia ya uchaguzi ni pamoja watu kuchagua namna gani rasilimali zao/Kodi zao/ keki ya taifa vitumike kwenye kustaawishi mahitaji yao kijamii na uchumi kuweza kupata maendeleo na kuboreshwa maisha.
Sasa hebu sasa watu wenye akili timamu ( wanaojitambua na wanaelewa elimu ya uraia) Jimbo la singida Mashariki wakipewa machuguo ya namna ya kutumia hiyo hela zaidi ya 2.5 billion ya uchaguzi wa marudio

#1 mbuge, ambaye ataenda kuwakikisha bungeni kwa miezi 12(kupiga kura uchaguzi wa marudio/ambao utachoma zaidi ya bilioni 2.5 gharama za uchaguzi, posho na mshahara wa mbuge Hadi mwakani, kiinua mgongo Cha mbuge)
AU
#2 wodi safi za kinamama kwenye zahanati 5 za Jimbo hilo, pamoja na vitanda, magodoro na kuboreshwa kwa miundo mbinu ya maji(vyoo) kwenye zahanati huskia.
AU
#3 Kujenga shule moja ya A level ya kisasa KABISA ya michepuo ya sayansi, maabara zenye vifaaa Kama vyoteee, ya Kama bilioni 1.6
-wanafunzi kutoka kwenye shule za kata kwenye jimbo hilo wasome bure kwa miaka mi 5 ya mwanzo( assume wanafunzu 300 kwa mwaka * 5* 60k= 36 milioni TU)
-walimu wapewe posho za milioni 3 kwa Kila A watakazo toa kwa miaka 5 ya mwazo( assume A 20 @3M * miaka 5= 300 milioni TU)

#4 maji, wachimbiwe visima 10 complete @ 200M vya maji ya uhakika....

Tutafakari na kuchukua hatua kwa maendeleo yetu wenyewe tusisubiri kupewa stori feki na wanasiasa, sisi ndo mabosi wao tuwapangie nini tunataka kutokana na Kodi na rasilimali zetu.. OVER.

Cc faizafoxy MKWEPA KODI
 
MAPITO Mwanza

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
1,364
2,000
Kwa ujumla wetu sisi watanzani hatujui samani ya nchi yetu tukiondoa uchama tulionao tunafanywa Kama wapangaji kwenye nchi yetu wenyewe kiongozi tuliempigia kula sisi wenyewe anatugeuka nakuamua kufanya tofauti nakatiba isemavyo nasisi kwa wingi tunaanza kusifu na kuabudu bila hata soni watu wanapotea wanapigwa marisasi hazalani Hakuna wa kuhoji vyombo vywetu vywa ulinzi na usalama vimegeuka maadui wakubwa wa laia utazani vipo kwaajili ya viongozi tu Kwakifupi safali yetu Kama taifa kwenda kutambua hakizetu ni ndefu sana. Nb uzi Kama huu Huwaoni watu Kama jingalao lizaboni kina chakubimbi na tem nzima ya lumumba FC
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom