Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Ni wakati sahihi kwetu watanzania kujichagulia wenyewe chaguo la Mungu na si kuchaguliwa na wachache. Tumepata fundisho kuwa aliyedhaniwa kuwa chaguo la Mungu 2005 kumbe hakuwa. Si chaguo la Mungu kwa vile hasikii kilio cha watanzania walio wengi, haachani na mafisadi na haashi safari nyingi za nje kana kwamba maendeleo yetu yataletwa kwa safari zake. Rais wetu wa sasa afike mahali atambue kwamba nadharia ya maendeleo ya misaada imepitwa na wakati. Sayansi imekataa kuwa misaada kutoka nje inaleta maendeleo ya nchi.
Hatukupata chaguo la Mungu mwaka 2005 kwa vile tuliangalia sura ya mtu, tulisikiliza maneno matupu ya mgombea, hatukutafuta historia ya Mgombea, tulidanganywa na watu wachache kuwa tuna chaguo la Mungu kumbe la. Sasa nani changu la Mungu mwaka huu 2010. Ni huyu hapa:
1. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuwa amelinda maliasili ya nchi- Maliasili
2. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla wake
si kuiba huku na kupeleke kwa wapiga kura- Maendeleo ya kweli
3. Aliyethibitika kuwa hakuiba pesa za Watanzania ili kununua uongozi- Si mtoa
rushwa wala hakutumia pesa za wizi
4. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuwa ametetea katiba ya nchi yetu- Katiba
5. Alitethibitika wazi kuwa anaipenda nchi yetu si kuleta wezi Tanzania kwa jina la
wawekezaji- Mpenda nchi
6. Aliyethibitika wazi kuwa ana dira sahihi ya elimu- si ubabaishaji wa maboma ya
shule za kata-Elimu bora
7. Aliyethibitika wazi kuwa anajali utu wa Watanzania si muigizaji huku anaenda
safari akiacha watanzania wakilipukiwa na mabomu, wakifukiwa na milima,
wakisombwa na mafuriko, wakifa njaa- Anayejali utu si msanii