Chaguo la Mchungaji Mgombea Urais kupitia CCM

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
1. Awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya mpito, inahitaji utashi wa hali ya juu wenye busara na hekima kuturudisha mstari ulionyooka ili tushikamane
2. Ni ndoto, hasa kwa Watangaza Nia wanaokuja na ahadi za maziwa na asali, kuwa bila kurudisha Taifa katika mshikamano na unyoofu, tutaneemeka!
3. Busara na hekima zenye kutuunganisha na kuleta mshikamano na si mgawanyiko ndio uongozi tunaouhitaji, turudi kuwa Taifa imara la Umoja na Utu!
4. Ni kwa sababu hizo, za kujenga Taifa linaloaminiana na kuheshimiana Kiitikadi na tofauti zetu zote nyingine, Awamu ya 5 inahitaji busara kubwa sana na si ahadi za kuleta neema!
5. Ningekuwa mjumbe wa CC, NEC na hata Mkutano Mkuu wa CCM, anayefaa kuleta umoja wa kweli, kuzingatia haki, utu na chachu ya uwajibikaji na uadilifu
6. Ningepiga kura yangu kwa Mwana CCM ambaye Taifa linamhitaji wakati huu mgumu wa majaribu na mpito Mh. Jaji Augustine Ramadhani agombee Urais wa Tanzania
7. Sambamba ya kumchagua Jaji Augustino, Bi. Asha Migiro angekuwa chaguo langu kuwa mgombea mwenza na makamu wa Rais. Hii ndio tiketi ya ushindi kwa CCM yenye kutaka kuirudisha Tanzania katika umoja, uaminifu, uadilifu, mshikamano na uwajibikaji
8. Lakini kama nitakuwa upande ule wa maslahi na ahadi zisizoeleweka, basi Watangaza Nia wengine wote watapitishwa kulinda maslahi ya Chama na maslahi binafsi ya makundi yanayovutana na kugombania utawala ndani ya Chama
9. Hatuwezi kujenga nchi, kupiga vita na umasikini, ujinga na maradhi tukiwa tumetengamana na tuna visasi au kukosa busara kujenga umoja
10. Tukiamua kuwa vipofu wa hali tete ya miaka 15 iliyopita, tukakimbilia maslahi na kutafuta utajiri eti kuondoa adha na tabu, tutapotea!
11. Hatuwezi kutengeneza Asali na Maziwa tukiwa na mivutano ya kitaifa au hata ndani ya vyama (CCM), huko ni kujenga nyumba mchangani!
12. Amani na mshikamano wetu, umeingia dosari kutokana na udhaifu unaotokana na tamaa za kutajirika na sera uchwara za neema za giza na za haraka haraka kutafuna rasilimali zetu
13. Tusipokuwa na Serikali makini yenye busara na hekima, inayoendesha mambo kwa pupa, kejeli,kukiuka demokrasia na sauti tofauti, tutajuta na kuangamia zaidi katika dimbwi la umasikini, ufisadi na utengamano
14. Tunaweza kurudi kwenye mstari mnyoofu bila kukurupuka kumaliza rasilimali zetu kiholela kwa haraka ya kuongeza pato la Taifa
15. Shubiri ya kujenga mfumo imara wa uzalishaji mali ni Seikali imara iliyo sikivu, inayojihoji na kujikosoa, inayoangalia maslahi ya umma kwa ujumla na kwa manufaa ya umma mzima wa Watanzania na si maslahi ya Watanzania wachache au wawekezaji wa kigeni
16. Hatutaweza futa umasikini, tengeneza ajira au kuota Matumaini, Upya na Mabadiliko bila kuwa na viongozi wenye Busara na Hekima
17. Narudia tena, awamu ya 5 ni ya kutupitisha nyikani ambako tuna mifarakano mikubwa ya itikadi, kidini, kipato, maslahi na vipaumbele
18. Tunajitaji kiongozi imara na ndani ya CCM atakayeweza kazi hii kwa hekima ni Jaji Ramadhani! Wengine tunaweza kuwataka Ila hawahitajiki !
 
Kwa hiyo chaguo lako ni Augustine Ramadhan na Asha Rose Migiro akiwa mgombea mwenza? mimi nilidhani ni kazi ya mgombea mwenyewe kumchagua mwenza na ndio maana wagombea wengi wamejipanga kwa tumaini kwamba hata wakikosa Urais kuna nafasi ya mwenza ambayo kwa imani yao kama rais atatoka Zanzibar, mwenza atatoka bara hivyo kuna nafasi nyingine kubwa ya kuteuliwa kama mwenza..tatizo kubwa la hawa ulowataja ni kutokuwa na nguvu ama uwezo wa kupingana na kundi lolote.

Kwa maana hiyo Mtandao utawaendesha, kumbuka mtandao ni Cartel na huwa hawatafuti makundi au urafiki bali kulinda interest zao. Hawahitaji kuwa IKULU bali wanataka kutawala kiuchumi, kujua kila hatua inayochukuliwa itakuwa na madhara gani, faida gani na kadhalika.

Mimi kusema kweli sina Imani kubwa na CCM kwa sababu rais yeyote atakaye chaguliwa ataendeshwa tu hakuna mule mwenye moyo kama Nyerere pengine Makongoro kwa sababu ana watu wazito nyuma yake. Akichaguliwa makongoro nina hakika kina Butiku, Salim, Warioba watakuwa washauri wake halafu kuna kundi la TISS ambalo bado bado wana Uzalendo mkubwa wa Tanzania ya Mwalimu.

Hivyo maadam haitawezekana Makongoro na macho yote yapo kwa Augustine Ramadhan nadhani huko mbali sana na ukweli..
 
Dahhh, @Rev.Kishoka kumbe bado upo? Nina kitambo sijakusikia humu JF. Nilifikiri umeshapotea kimoja.

Enzi naingia, ndiyo mlikuwa mkiwasha moto na akina Mzee Field Marshal ES.......

Welcome back and nice to see you again humu JF. Mtanzania na wewe rudi sasa ingawa najua umebwana na kazi.
 
Last edited by a moderator:

Nipo mtani, naangalia mwaka wa siasa za maji taka na vitisho, kuruniana na ulaghai!
 
Back
Top Bottom