Uchaguzi 2020 Chagua CCM 28 Oktoba 2020

Sep 8, 2020
67
133
Ni uchaguzi rahisi kwa CCM, uchaguzi mwepesi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii. Ni uchaguzi wa mafanikio ya CCM dhidi ya ahadi za Wapinzani.

CCM inakwenda ktk uchaguzi huu kuonesha mafanikio iliyoyafanya kwa miaka mitano iliyopita (ambayo kimsingi ni mengi) wakati wapinzani wanakwenda kutoa ahadi.
Kwa asili ya watu ni rahisi kuchagua kitu kinachoonekana kuliko ahadi tupu.
Hapa CCM inayo nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huu kuwa kuwa inakwenda kuonesha matokeo ya uongozi wake.

Watu wenye kumbukumbu sawa watakubaliana nami kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi ambao Chama tawala kinakwenda kushinda kwa kishindo. Sababu kubwa za ushindi huo wa kishindo ni hizi zifuatazo;

1. Utekelezaji wa Ilani 2015-2020.

Kwa kulinganisha awamu mbili zilizotangulia, awamu hii CCM imetekeleza kwa vitendo na kwa kiwango kikubwa zaidi Ilani yake ya Uchaguzi 2015-2020. CCM imetenda mambo mengi makubwa, kuyataja machache ktk makundi yake;

Serikali ya CCM imeboresha miundombinu ya ardhini (barabara, madaraja na reli) kwa kiwango cha juu kupita wakati wote.
Imejenga barabara za juu na baharini kwa kiwango cha juu kupita wakati wowote katika historia ya nchi hii. Barabara ya juu ya Tazara, Ubungo interchange, Barabara nane Kimara -Kibaha Dsm, daraja la New Salenda (Tanzanite), daraja la Magufuli Kilombero, daraja la Furahisha Mwanza, daraja la Busisi Kigongo Mwanza nk. hii yote ni mifano ya wazi kabisa ktk eneo hili.

CCM imejenga vivuko vikubwa na vya kisasa baharini ( Kivuko cha Kilwa), ziwa Victoria na Nyasa. Inajenga reli ya kisasa ya mwendo wa haraka, hii ni ya kwanza ktk nchi yetu.
Imeimarisha usafiri wa anga, ununuzi wa Ndege, kuboresha na kujenga viwanja vya Ndege nchini. Inajenga mradi mkubwa wa kufua umeme mwingi na wa kutosha, imeimarisha nidhamu kazini, imeboresha maslahi ya watumishi kwa kupunguza kodi katika pato halisi hivo kuongeza kiwango cha pato halisi la mtumishi (take home).

Serikali ya CCM imeongeza bajeti ya afya, elimu, maji, utawala bora, nk.
Imeimarisha mifumo ya utoaji haki kwa kuajiri nguvu kazi ktk mahakama zetu, kuboresha miundo mbinu ya mahakama na kurekebisha sheria zetu kwendana na wakatiwa sasa.

CCM imepandisha hadhi ya nchi mbele ya uso wa dunia, sasa Tanzania sio shamba la bibi kama ilivyiotafsirika awali. Tanzania sasa inaheshimika kwa watu wote, Serikali imerekebisha sheria za madini kwa manufaa ya nchi yetu.

Serikali imefanya mambo mengi makubwa kwa kipindi kifupi kuliko wakati mwingine wowote. Imetekeleza kwa kishindo, Imefanikiwa! Huu ni ushahidi kuwa awamu ya pili itafanya mambo mengi makubwa zaidi, tuichague tena CCM.

2. Skendo za Rushwa na Ufisadi.

Huu ndio uchaguzi ambao CCM inaufanya kwa mara ya kwanza katika miongo mitatu bila Serikali yake kuwa na skendo yoyote ya rushwa na ufisadi.

Maana ya jambo hili ni kuwa, kwa miaka mitano Serikali ya CCM imefanikiwa kudhibiti rushwa na ufisadi nchini. Hakuna hoja ya msingi eneo hili kama kashfa kulinganisha na chaguzi zingine. Wenye kumbukumbu watakumbuka skendo za RADA, MEREMETA, EPA, RICHMOND, KAGODA nk.

Ni kweli yote haya yametokea ktk Serikali za CCM zilizotangulia ndio maana kwa kutambua dosari hiyo awamu hii kumefanyika marekebisho makubwa ktk usimamizi wa sheria za nchi.

Huu ni ushindi mkubwa kwa CCM, ni ushindi kwa Tanzania. Ni mafanikio makubwa kwa Serikali! Serikali yenye uadilifu haipaswi kupanguliwa, ichagueni tena. Kazi kubwa iliyo mbele ya Wana-CCM nchi nzima ni kuwafahamisha watu juu ya mambo haya mazuri yaliyofanyika ili waichague tena. Huu ni uchaguzi wa mafanikio ya CCM dhidi ya ahadi za wapinzani, watu watachagua mafanikio yanayoonekana.

3. Uwajibikaji.

Imeandikwa, usiposema wewe mawe yatapaza sauti. Watu wote wanajua kuwa uwajibikaji wa Serikali kwa sasa ni wa mfano. Tanzania inajua, Afrika Mashariki inapigia mfano kwa Tanzania na Dunia inachagiza.

Serikali imesimamia kwa kiwango kikubwa uwajibikaji na nidhamu ktk ofisi za umma. CCM inakwenda katika uchaguzi huu nchi ikiwa imepunguza mizaha katika uwajibikaji. Kila mmoja anatimiza wajibu wake kama inavyomstahili, uzembe kazini na urasimu vimepungua sana. Tuichague tena CCM tumalizie kabisa mambo haya. Haya ni mafanikio ya hali ya juu kwa Chama na Serikali.

Tunakusudia kujenga nchi yenye nidhamu ya hali ya juu, yenye kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya watu. Tanzania inapaswa kusonga mbele zaidi ya ilivyo sasa, ni uchaguzi wa mafanikio dhidi ya ahadi. CCM inaeleza mafanikio, wengine wanaeleza ahadi. ChagueniMafanikio,#ChaguaCCMOctoba28.
#MitanoTena!
MenukaJr.
 
Hali ya umaskini ikoje? Hali ya mzunguko wa biashara ikoje? Waliotumbuliwa na vyeti feki wako wapi siku hizi?wajumbe waliotia Nia na kukosa kura wako wapi? Mishahara waliyokatwa iko wapi? Hata makanisani sadaka hakuna tena hivyo hata makanisa hawataki mgombea wa CCM.
 
Ni uchaguzi rahisi kwa CCM, uchaguzi mwepesi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii. Ni uchaguzi wa mafanikio ya CCM dhidi ya ahadi za Wapinzani.

Hizi post huwa mnaandikiwa na nani asiyetumia akili?
 
Kabla sijamsikiliza Lisu, nilikuwa hivi kimsimamo wa Kura.
1. Rais Magufuli (CCM).
2. Mbunge Upendo Peneza(Chadema).
3. Diwani CCM.

Kwa Sasa baada ya kumsikiliza Lisu ni hivi.
1. Rais Lisu(Chadema)
2. Mbunge, Upendo Peneza(Chadema)
3. Diwani, CCM.

Hata muongee vipi, hata mtoe ahadi vipi, hata mmchafue mgombea niliyepanga kumpigia kura kwa namna yoyoye ile, kura yangu Sasa haitabadilika, tarehe 28/10 ni siku nakwenda kukamilisha uamuzi wangu kwenye karatasi ya kura.
 
Huo msimamo wako uko sahihi mkuu ingawa ingependeza huyo diwani pia ungempiga chini. Unajua kwa nini? Hawa ndio wanahusika kupitisha sheria ndogondogo za miji, hivyo wanaweza kuwatungia kisheria vya kuwaumiza.
 
Wewe mwenyewe hutoipa kura CCM. Hapo umeandika ilimradi mkono uende kinywani
 
Ni uchaguzi rahisi kweli kweli, ndio maana tumewakusanya maDED nchi nzima tunywe nao chai halafu warudi kwenye vituo vyao vya kazi.
 
Ni uchaguzi rahisi kwa CCM, uchaguzi mwepesi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii. Ni uchaguzi wa mafanikio ya CCM dhidi ya ahadi za Wapinzani.

CCM inakwenda ktk uchaguzi huu kuonesha mafanikio iliyoyafanya kwa miaka mitano iliyopita (ambayo kimsingi ni mengi) wakati wapinzani wanakwenda kutoa ahadi.
Kwa asili ya watu ni rahisi kuchagua kitu kinachoonekana kuliko ahadi tupu.
Hapa CCM inayo nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huu kuwa kuwa inakwenda kuonesha matokeo ya uongozi wake.
Huu utakuwa uchaguzi mgumu sana kwa CCM. Amini maneno yangu. Watu hawali flyovers wala SGR. Subiri utaona mwenyewe ngoma itakavyokuwa nzito
 
Watu wenye kumbukumbu sawa watakubaliana nami kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi ambao Chama tawala kinakwenda kushinda kwa kishindo.
Hakuna ushindi wa kishindo mwaka huu. Mtapigika sana mwaka huu kupata ushindi. I tell you guys
 
Eti eeh . . . ngoja wakafanye uzwazwa. Wananchi watawagana pale pale vituoni
Subiri upepo uvume kwa kasi utaziona.....za kuku. Lembeli aliwahi kusema. Sass hivi wamechanganyikiwa, wanashikana uchawi wenyewe. Sasa hivi ni ccm mpya ndio maana huwaoni Nape, Kinana and Makambas. MATAGA eti ndio waongoza dira. Mtawaokota korongoni safari hii
 
Kabla sijamsikiliza Lisu, nilikuwa hivi kimsimamo wa Kura.
1. Rais Magufuli (CCM).
2. Mbunge Upendo Peneza(Chadema).
3. Diwani CCM.

Kwa Sasa baada ya kumsikiliza Lisu ni hivi.
1. Rais Lisu(Chadema)
2. Mbunge, Upendo Peneza(Chadema)
3. Diwani, CCM.

Hata muongee vipi, hata mtoe ahadi vipi, hata mmchafue mgombea niliyepanga kumpigia kura kwa namna yoyoye ile, kura yangu Sasa haitabadilika, tarehe 28/10 ni siku nakwenda kukamilisha uamuzi wangu kwenye karatasi ya kura.
Mimi kama wewe baada kumsikiliza... Na alivozungumza na waandishi jana nimegundua ana akili sana. Sitabadilika tena na familia yangu imeamua

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kura yangu itakuwa kama ifuatavyo;
Rais- chadema
Mbunge -chadema
Diwani-chadema.
Imeisha hiyoo!!
 
Back
Top Bottom