Chagonja: Ni kweli Bomu, Bastola na SMG vilitumika tukio la Arusha

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Leo asubuhi kupitia Radio One, kamanda wa Upelelezi Chagonja amethibitisha Kauli ya Mbowe kuwa ni kweli tukio la mlipuko wa Arusha lilihusisha silaha tatu tofauti, yaani BOMU, BASTOLA na BUNDUKI(SMG).

Amesema ni kweli Bomu ni la kurushwa na pia lilitengenezwa China tena kiwandani. Pia amethibitisha kuwa baada tu ya bomu kulipuka wahusika walikuwa wakifyatua risasi kulenga watu na maeneo mahali bomu lilipolipuka.

MY TAKE:
1/Tukio hili la Arusha lilikuwa na wahusika wasiopungua watatu tena wakifanya kazi tatu tofauti, Mrusha bomu(BOMBER), Mfyatua risasi(SHOOTER) na Mlenga shabaha(SNIPER).

2/Kuna ukweli kuwa wahusika ni watu wanaofanya kazi na taasisi za kiusalama ama wamewahi kupata mafunzo ya kiusalama(Polisi, Jeshini nk)

3/Hili ni tukio la KUPANGWA MAHUSUSI, kwani inaonekana kulikuwa na uratibu maalum mpaka lifanikiwe.

UPDATES
*Chagonja anadai uchunguzi wake wa awali unaonyesha kuwa mtu huyo huyo aliyerusha Bomu ndiye pia huyo huyo aliyetumia bastola kupiga watu na ndiye huyo huyo alitumia SMG kulenga watu kama njia ya kujihami asikamatwe na watu, polisi walimwona ila raia wakazuia polisi wasimkamate!!!
 
Sasa huo ushahidi amepewa na Mbowe?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mnaanza kukubali maneno sababu imedhibitika kuwa majeruhi wengi wanamajeraha ya risasi. Mbona ulimjia juu Mh. Mbowe kuwa asipodhibitisha hili utamchukulia hatua? Mmeona ushahidi upo wazi kama ule wa Mwandishi Mwangosi (RIP) sasa mnatafuta namna ya kuupotezea. Baada ya kumkosa kijana aliyetaka kumkamata mlipuaji na akapigwa risasi na polisi ili mlipuaji atoroke, sasa mnaanza kuweweseka mkijua ushahidi upo clear. Katika hili tunaomba wachunguzi wa nje waje na siyo KAMATI ya Mh. Nchimbi iliyofukia tukio la polisi kumuuwa mwandishi Daudi Mwangosi kule Iringa.
 
Polisi ni wahusika wa hizo risasi kwa mujibu wa majeruhi lakini bomb ni mpango wa Mwigulu!
 
Leo asubuhi kupitia Radio One, kamanda wa Upelelezi Chagonja amethibitisha Kauli ya Mbowe kuwa ni kweli tukio la mlipuko wa Arusha lilihusisha silaha tatu tofauti, yaani BOMU, BASTOLA na BUNDUKI(SMG).
Amesema ni kweli Bomu ni la kurushwa na pia lilitengenezwa China tena kiwandani. Pia amethibitisha kuwa baada tu ya bomu kulipuka wahusika walikuwa wakifyatua risasi kulenga watu na maeneo mahali bomu lilipolipuka.

1. wahusika anamaanisha wahalifu?

2. 'wahusika' maana yake walikuwa zaidi ya mmoja(mrusha bomu)?

3. polisi sababu wana mafunzo walichukua hatua gani kuwadhibiti 'wahusika'?

4. Risasi zililenga watu waliopo bomu lilipoangukia, anathibitisha 'wahusika' walinuia kuwadhuru viongozi wa cdm?
 
Jeuri ya mwigulu ina lindwa na mamlaka ya juu,ambayo haiwezi kumgeuka labda aanze yeye kuigeuka na hapo ndipo shahidi mbali mbali za matukio yote since awe kiongozi wa juu wa chama zitawekwa wazi,kama ilivyotokea uganda mkuu wa usalama msaatafu kaongea jana bbc kuwa ni kweli ile barua aliandika yeye na ni kweli m7n anataka mtoto wake awe rais<ikumbukwe yule alikuwa kiongozi wa juu tena wa usalama wa Taifa> hapo hapo msemaji wa serikali ya uganda akakanusha habari hizo ila ujumbe ushatufikia na ukweli ushajulikana japo huyu mkuu yupo uhamishoni UK
 
Mwigulu ni nani ndani ya siasa za Tanzania hadi aandae mauaji yatekelezeke na asichukuliwe hatua.?
 
NADHANI sasa dozi inaanza kuwapata taratiiiiiiiiiibu, watawala walidhani itabaki siri kubwa kumbe ukimtumaini mungu anakuweka huru.Mungu amewaweka huru Mowe na Lema.Chagonja kagundua na kusikia harufu ya THE HAGUE wanachomokaje hapo.ndiyo swali, kaanza jana mh.pinda kakiri ni product from CHINA.Maandiko yanasema wote watakiri kuwa YESU NI MWANA WA MUNGU.ccm watakiri mwishoni kuwa chadema ni mpango wa mungu
 
Sasa kama Chagonja anayajua hayo wanafanya nini badala ya kuwakamate kina Mwigulu, Kinana, Nape et al kwa uhalifu huo wa wazi dhidi ya Watanzania???????

Kwa nini wanakosa weledi na kuishia kufanya kazi kwenye media ili-hali vitendo ni kinyume chake???????
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom