CHADEMA, Zitto, Tundu Lissu jifunzeni kwa Jeremy Cobyn

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Nimekuwa nikifuatilia mjadala wa Brexit katika Bunge la makabwela (house of commons) la UK.Nilichogumdua kambi ya upinzani chini ya Jeremy Cobyn wanajenga uhalali wa hoja zao huku wakitaka kuungwa mkono na waingereza na si mataifa ya nje.

Leo tumeshuhudia maspika wa mabunge yote lile la mabwanyenye (house of Lords) na makabwela (house of commons) walitangaza kuahirisha mijadala kwa wiki tano hadi tarehe 14 October,2019,kufuatia amri iliyosainiwa na malkia wa Uingereza ambayo haiwezi kupingwa kortini kwani wabunge,mawaziri na waziri Mkuu UK huapa kutii maagizo ya mfalme au Malkia.

Ninayasema haya kwa sababu najua Jeremy Cobyn ni bosi wa Zitto Kabwe,na vile vile Chadema na Tundu Lissu wamekukuwa wakiishitaki Tanzania kwa waingereza ili washinikize wananchi kupitia serikali kurejea utumwa wa fikra.Mara kadhaa Zitto,Tundu na Chadema wameandika barua kwenye ofisi za Balozi na Bunge la UK ili Watanzania washindwe na kurudi kwenye utumwa bila mafanikio.

Jeremy Cobyn,hajawahi kutaka msaada wa nchi za nje ili kumpa shinikizo Borris au Malkia bali anashawishi wananchi na wabunge.Hili ni fundisho,kama wanasiasa wa upinzani wataendelea kukumbatia utumwa na fikra za kushikiwa akili hakika wananchi tutawapuuza.

NB:Katika andiko hili,Chadema inamaanisha Mbowe na wafuasi wa Chadema, Tundu Lissu ni Tundu Lissu na Zitto Kabwe ni Zitto Kabwe.

Tujadili kwa mantiki.
 
SIYO HAYO TU ... FIkiria nini kingetokea iwapo wabunge wa CCM wangeungana na wa upinzani, ktk kukwamisha hoja ya serikali, na wakafukuzwa (whip withdraw). Naamn CCM ingetukanwa hakuna mfano, lakn kumbe n jambo la kawaida. Wabunge wa conservative wamefukuzwa kwa kuungana na waupinzani kupinga serikali ya BO JO, huo ndo utaratibu wa siasa za vyama vingi... WASICHONGE, WAJIPANGE!
 
''Kufuatia amri iliyosainiwa na malkia wa Uingereza ambayo haiwezi kupingwa kortini kwani wabunge mawaziri na waziri Mkuu UK huapa kutii maagizo ya mfalme au Malkia.''

Hapo juu ukweli umepindishwa kidogo.
 
SIYO HAYO TU ... FIkiria nini kingetokea iwapo wabunge wa CCM wangeungana na wa upinzani, ktk kukwamisha hoja ya serikali, na wakafukuzwa (whip withdraw). Naamn CCM ingetukanwa hakuna mfano, lakn kumbe n jambo la kawaida. Wabunge wa conservative wamefukuzwa kwa kuungana na waupinzani kupinga serikali ya BO JO, huo ndo utaratibu wa siasa za vyama vingi... WASICHONGE, WAJIPANGE!
Hoja jadidi
 
Mkuu Kaka Wakudadavua, naunga mkono hoja, na kiukweli hapa sasa ndio nakuona ukiwathibitishia hawa wajinga wajinga wa humu kuwa Kaka Wakudadavua alipiga shule ya ukweli, maana hii mada imekwenda shule.

Hili somo la Wapinzani wa Uingereza ni somo zuri sana kwa Wapinzani wa Tanzania waige wapinzani wenzao wa ukweli wa Uingereza, ila pia Kaka Wakudadavua, mweleleze na Spika na Naibu Spika, na wao waendeshe Bunge letu kwa haki kama linavyoendeshwa Bunge la Uingereza ili kina Lissu, kina Zitto, kina Mbowe na Wapinzani, nao wawe kama wenzao.

Ukisoma bandiko hilo, naomba niweke msisitizo kabla, uangalie kuna alama ya kuuliza maana...

Sitaki kuitwa tena mahali kujieleza kama ilivyotokea mwanzo mtu kufunga safari all that way, kwenda kuwafundisha watu kusoma alama tuu ya kuuliza!.
P
 
Wakudadavua huko unapopasema wapinzani wanafanya kazi zao za kuwashawishi wananchi kikatiba bila kuingiliwa na dola. Je hapa kwetu wapinzani wako huru kufanya kazi zao kama kina Corbyn ?!. Hapa kwetu mpinzani bungeni tu hapewi nafasi, na hazingatiwi kama naye ni muhimu ktk kuamua.

Ukiangalia kilichotokea England. Bunge halikukubali kuvuruzwa na waziri mkuu . Kwetu hapa bunge letu linaweza kupinga maoni ya kiongozi mtawala ?! . Wakudadavua unalinganisha usiku wa giza na mchana kweupe. Au hata mbingu na ardhi.
 
Hata Wasudan hakuhitaji msaada wa wazungu kumwondoa Al Bashir.Ni wananchi wenyewe,kama wananchi wakiona wanasiasa wa upinzani ni warongo ni dhahiri watawapuuza.Mmeacha nguvu ya umma mmekamata nguvu ya mange
 
Pascal umelewa makombo ya Lumumba hulaumiki ?? au unaogopa kubambikiziwa kesi ??? Hivi Uingereza mpinzani gani ana kesi ya kubambikiziwa mahakamani ??
 
Abii wa Ethiopia alikwenda kula tende Khartoum ??
 
Hata Wasudan hakuhitaji msaada wa wazungu kumwondoa Al Bashir.Ni wananchi wenyewe,kama wananchi wakiona wanasiasa wa upinzani ni warongo ni dhahiri watawapuuza.Mmeacha nguvu ya umma mmekamata nguvu ya mange
Mbona kama unachanganya mambo, unaongelea ishu ya kujenga hoja bungeni wakati huohuo unachanganya ni ishu ya wananchi kuandamana kumtoa mtawala kwenye nchi ambayo hata umoja wa wanawake wa chama cha upinzani wakikaa kikao cha ndani kujadili mambo yao wanafurumushwa kwa mabomu na virungu.
 
Pascal umelewa makombo ya Lumumba hulaumiki ?? au unaogopa kubambikiziwa kesi ??? Hivi Uingereza mpinzani gani ana kesi ya kubambikiziwa mahakamani ??
Hapa Tanzania nani kabambikiziwa kesi?
 
Ndugu zangu,

Nimekuwa nikifuatilia mjadala wa Brexit katika Bunge la makabwela (house of commons) la UK.Nilichogumdua kambi ya upinzani chini ya Jeremy Cobyn wanajenga uhalali wa hoja zao huku wakitaka kuungwa mkono na waingereza na si mataifa ya nje.

Leo tumeshuhudia maspika wa mabunge yote lile la mabwanyenye (house of Lords) na makabwela (house of commons) walitangaza kuahirisha mijadala kwa wiki tano hadi tarehe 14 October,2019,kufuatia amri iliyosainiwa na malkia wa Uingereza ambayo haiwezi kupingwa kortini kwani wabunge,mawaziri na waziri Mkuu UK huapa kutii maagizo ya mfalme au Malkia.

Ninayasema haya kwa sababu najua Jeremy Cobyn ni bosi wa Zitto Kabwe,na vile vile Chadema na Tundu Lissu wamekukuwa wakiishitaki Tanzania kwa waingereza ili washinikize wananchi kupitia serikali kurejea utumwa wa fikra.Mara kadhaa Zitto,Tundu na Chadema wameandika barua kwenye ofisi za Balozi na Bunge la UK ili Watanzania washindwe na kurudi kwenye utumwa bila mafanikio.

Jeremy Cobyn,hajawahi kutaka msaada wa nchi za nje ili kumpa shinikizo Borris au Malkia bali anashawishi wananchi na wabunge.Hili ni fundisho,kama wanasiasa wa upinzani wataendelea kukumbatia utumwa na fikra za kushikiwa akili hakika wananchi tutawapuuza.

NB:Katika andiko hili,Chadema inamaanisha Mbowe na wafuasi wa Chadema, Tundu Lissu ni Tundu Lissu na Zitto Kabwe ni Zitto Kabwe.

Tujadili kwa mantiki.

Hao wananchi wataonana nao wapi ili waongee nao?.Kama mikutano ya ndani tu au hata wakikutana misibani wanasambaratishwa ili wasiongee na wananchi.
 
Back
Top Bottom