CHADEMA, Zitto, Tundu Lissu jifunzeni kwa Jeremy Cobyn

ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
1,550
2,000
Ndugu zangu,

Nimekuwa nikifuatilia mjadala wa Brexit katika Bunge la makabwela (house of commons) la UK.Nilichogumdua kambi ya upinzani chini ya Jeremy Cobyn wanajenga uhalali wa hoja zao huku wakitaka kuungwa mkono na waingereza na si mataifa ya nje.

Leo tumeshuhudia maspika wa mabunge yote lile la mabwanyenye (house of Lords) na makabwela (house of commons) walitangaza kuahirisha mijadala kwa wiki tano hadi tarehe 14 October,2019,kufuatia amri iliyosainiwa na malkia wa Uingereza ambayo haiwezi kupingwa kortini kwani wabunge,mawaziri na waziri Mkuu UK huapa kutii maagizo ya mfalme au Malkia.

Ninayasema haya kwa sababu najua Jeremy Cobyn ni bosi wa Zitto Kabwe,na vile vile Chadema na Tundu Lissu wamekukuwa wakiishitaki Tanzania kwa waingereza ili washinikize wananchi kupitia serikali kurejea utumwa wa fikra.Mara kadhaa Zitto,Tundu na Chadema wameandika barua kwenye ofisi za Balozi na Bunge la UK ili Watanzania washindwe na kurudi kwenye utumwa bila mafanikio.

Jeremy Cobyn,hajawahi kutaka msaada wa nchi za nje ili kumpa shinikizo Borris au Malkia bali anashawishi wananchi na wabunge.Hili ni fundisho,kama wanasiasa wa upinzani wataendelea kukumbatia utumwa na fikra za kushikiwa akili hakika wananchi tutawapuuza.

NB:Katika andiko hili,Chadema inamaanisha Mbowe na wafuasi wa Chadema, Tundu Lissu ni Tundu Lissu na Zitto Kabwe ni Zitto Kabwe.

Tujadili kwa mantiki.
Wenzetu maslahi ya Taifa i kwanza.
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
14,981
2,000
Umechemka, hakuna kusichopingwa kortin.

Kwa taarifa tu leo mahakama imeamua kulifunga bunge ni batili na kinyume cha sheria.

Sijui aliyekuambis maamuzi ya malkia hayapingwi ni nani?
Sasa hao walishitaki nchi za nje?subiri rufaa ya korti kuu ya UK
 

mulaga

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
3,163
2,000
Serikali yetu inawaogopa wafadhili kuliko wananchi.Japo uwaita mabeberu wakiwakumbusha wajibu wa kutenda haki ila wakipewa hela aachi kupokea na kuwaita wafadhili.Sema wazungu wameumbwa na mioyo tofauti
Utetezi dhaifu
Sera zao watauzia wapi kama uwanja si huru
 
Top Bottom