Chadema, ZEC waingia kwenye mzozo Z’bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema, ZEC waingia kwenye mzozo Z’bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Feb 4, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  tume ya Uchaguzi Zanzibar imeipa barua ya karipio Chama Cha CHADEMA baada ya kukiuka sheria ya Uchaguzi wa Jimbo la Uzini kwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
  kwa mujibu wa barua hiyo, Chadema ilifanya mkutano wa kampeni wa tarehe 27/1 Huko Kitundu uliohutubiwa na Dk slaa.
  Kwa mujibu wa msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Ndugu Mussa Ali Juma, Chadema imekiuka sheria na kupewa karipio kali.


  MY TAKE.
  Chadema ijiangalie, vyenginevyo inaweza ikapigwa mstari mwekundu ktk uchaguzi ule,kwani ZEC wapo makini sana tofauti na NEC
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Duhu, cdm nayo bana
   
 3. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 641
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MY TAKE.
  "Chadema ijiangalie, vyenginevyo inaweza ikapigwa mstari mwekundu ktk uchaguzi ule,kwani ZEC wapo makini sana tofauti na NEC"

  Mbona una majibu kabisa? nna wasiwasi kama ndo hivyo.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ZEC wameshindwa tu kusema kwamba huku Zenji hatuhitaji upinzani
   
 5. Sihali

  Sihali Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa huwezi kuwaona wkijibu wale wanaopenda kuona CHADEMA inasemwa vizuri tuu ( viherehere ) imewagonga pabaya. na wanashuhudia ugumu wa kampeni Unguja. Mtakula kwa ugumu.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  SLAA mtu wa kukurupuka sana.
   
 7. mchadema

  mchadema JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Tumekuachia we mshakunaku urukie huu udaku!!
   
 8. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]CHADEMA yalimwa barua ya karipio


  na Nasra Abdallah


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [​IMG] [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupitia kwa kwa ofisi ya uchaguzi wilaya ya Kati, imekiaandikia barua ya karipio Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kitendo chake cha kufanya mkutano wa hadhara katika maeneo ya Shehia ya Tunduni, ikidai ni kinyume na kifungu cha 34 cha kanuni za uchaguzi za mwaka 2010.
  Katika barua hiyo ZEC ilisema kuwa CHADEMA ilifanya mkutano huo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, Januari 27 mwaka huu saa 10 jioni katika eneo ambalo si ofisi ya chama hicho ambapo kwa mujibu wa mwenendo mzima wa uchaguzi, mkutano huo umetambulika kama ni kampeni.
  "Kumbuka kwamba kwa mujibu wa ratiba ya tume ambayo umepatiwa kipindi cha kampeni ni Januari 28 hadi Februari 11 mwaka huu, hivyo basi mkutano huo ni haramu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi tuliyokubaliana," ilisema sehemu barua hiyo.
  Hata hivyo, CHADEMA kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Musa Yussuf, ilijibu karipio hilo ikisema kuwa inasikitishwa na barua hiyo kwani kwa mujibu wa maadili ya uchaguzi, chama na mgombea, wakifanya kitu ambacho ni kinyume na maadili, watatakiwa kufunguliwa malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi.
  Alisema baada ya msimamizi wa uchaguzi kupata malalamiko hayo, atamwandikia mlalamikiwa, akimfahamisha juu ya tuhuma zinazomkabili na kuambatanisha na tuhuma husika na kisha mtuhumiwa atatakiwa kujibu tuhuma hizo na kuwasilisha kwa msimamizi.
  "Huu ndio mchakato wa kushughulikia malalamiko uliowekwa na maadili ya Tume ya Uchaguzi ambayo unatakiwa kuyasimamia, kinachotushangaza na kufanya tuhoji ni uelewa wa ofisi yako.
  "Barua yako haina ambatanisho la malalamiko uliyopokea na kukusukuma wewe kutoa karipio na wala hukuelekeza kama mlalamikaji ni wewe au ni nani, vitendo vya ofisi yako kujigeuza kuwa mlalamikaji, msikiliza malalamiko na hakimu bila kuhusisha vikao ni kinyume na tarartibu," alisema Yussuf.
  Katika hatua nyingine CHADEMA imetetea maamuzi yake ya kuamua kukodi nyumba nane katika jimbo la Uzini baada ya Chama cha Mapinduzi kuirushia vijembe kuhusu kitendo chake hicho.
  Akizungumza katika mikutano miwili ya hadhara katika shehia ya Kiboje Mwembeshauri na Kiboje Mkwajuni, ofisa msaidizi wa kampeni, Benson Kigaila, alisema kukodi nyumba hizo huko ni kwamba fedha zote watakazotumia kila siku zitaenda kwa wananchi wa Uzini.
  Naye mgombea wa chama hicho katika jimbo hilo, Ally Mbarouk Mshimba, alisema katika uzinduzi wa kampeni za CCM, Rais mstaafu, Aman Abeid Karume, aliwaambia wakazi wa Uzini wasimchague mtu mgeni jambo ambalo limewafagilia njia CHADEMA kwa kuwa Mohamed Raza, ndiye mgeni.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  mbona kwenye blue hujaripoti.......................?

  chanzo: CHADEMA yalimwa barua ya karipio
   
 9. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Asante Mungu,hivi cdm nayo nigumuzo Zanzibar mpaka kufikia ZEC ya ccm kuilalamikia?!!!!ama kweli acheni Mugu aitwe Mungu
   
 10. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,966
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  hao zec wasicheze na chadema..wataumbuka..hii taasisi ipo makini sana..ukitaka kujua hilo angalia barua ilivyojibiwa..yaani zec imeelekezwa cha kufanya kabla ya kutoa malamiko..ni kama wamevaa suruali kabla hawajavaa chupi..take care zec
   
 11. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Zec walikuwa wajisahau baada ya ndoa ya ccm na cuf hawakutegemea kupata mpinzani mwingine znz sasa mziki wa cdm unawachanganya sana
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sasa Vanuatu CDM wanafanya nini
   
 13. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nawe nawe wa ajabu. Umeshaambiwa walianza kampeni kabla ya wakati. Ugumzo ndiyo huo? Au una maana nyingine?
   
 14. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Chezea CDM weyeee!! Songa mbele makamanda, kama ZEC wataka kukiuka taratibu ili kuvibeba vyama tawala na wafanye hivyo ili kurahisha kazi huko mbeleeni!!
   
 15. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Alaa! Unasema kweli?
   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  aseeeeeeeee!!
  Ccm bana, wanafundishwa kazi kila siku!
   
 17. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inamshika pabaya, anaona haya
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwamba hao bibi na bwana wanatosha?
   
 19. only83

  only83 JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Uoga wa ZEC huo..
   
 20. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwandishi Wetu, Zanzibar
  KUMEIBUKA msigano kati ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu ya ratiba ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini huku ZEC ikiituhumu Chadema kuanza kampeni kabla ya wakati.

  Kufuatia hali hiyo ZEC imeiandikia barua ya karipio Chadema, huku chama hicho kikijibu kuwa tume hiyo inapaswa kuwa makini katika utendaji wake, na kuitaka isifanye kazi isiyokuwa yake.

  Katika barua yake kwa Chadema, ZEC imekituhumu chama hicho kuanza kampeni kabla ya muda kupitia mkutano wake uliouita wa ndani Januari 27, mwaka huu ambao ZEC imeuita kuwa haramu, ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alizungumza na wanachama wa chama hicho.

  Kupitia barua yake ya Februari mosi mwaka huu yenye kumbukumbu namba TUZ/WKATI/BZO/VOL.1/2011/151, ikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘MKUTANO HARAMU ULIOFANYIKA SHEHIA YA TUNDUNI, TAREHE 27/01/2012,” ZEC imelaani mkutano huo uliokuwa wa hadhara ikieleza kuwa umefanyika kinyume na kifungu cha 34 cha Kanuni za Uchaguzi za 2010.

  “Ofisi ya Uchaguzi Wilaya ya Kati kwa masikitiko makubwa inalaani na kukaripia kitendo cha kufanyika kwa mkutano wa hadhara katika maeneo ya Shehia ya Tunduni…siku ya Ijumaa tarehe 27/01/2012, majira ya saa kumi za jioni katika eneo ambalo si afisi ya chama hicho, na kwa mujibu wa mwenendo wa ucahgzui, mkutano huo umetambulika kuwa ni kampeni,” ilisema sehemu ya barua hiyo, iliyosainiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Uzini, Mussa Ali Juma.

  Hata hivyo katika majibu yake kwa ZEC kupitia barua ya Februari 3, mwaka huu Chadema ilieleza kusikitishwa kwake na barua hiyo ya ZEC.Chadema ilisema kuwa ZEC imekwenda kinyume cha maadili ya uchaguzi ambayo yanaelekeza kuwa chama au mgombea akifanya jambo lililo kinyume cha maadili, anapaswa kufunguliwa malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi.

  “Baada ya msimamizi wa uchaguzi kupata malalamiko hayo, atamwandikia mlalamikiwa akimfahamisha juu ya tuhuma zinazomkabili na kuambatanisha na tuhuma husika. Mtuhumiwa atatakiwa kujibu tuhuma hizo na kuwasilisha kwa msimamizi . Baada ya msimamizi kupokea utetezi wa mtuhumiwa ataitisha kamati ya maadili ili kusikiliza pande zote mbili;…ndipo hukumu hutolewa,” ilieleza barua hiyo ya Chadema kwa ZEC na kuongeza:
  “Barua yako haijaambatana na malalamiko uliyopokea na kukusuma wewe kutoa karipio na wala hukueleza kama mlalamikaji ni wewe au ni nani.”

  Chadema ilisema kuwa hatua hiyo ya ZEC ni kujigeuza kuwa mlalamikaji, msikilizaji wa malamaiko na hakimu, bila kuhusisha vikao na kinyume cha taratibu na kwamba kinaondoa imani ya wadau juu ya ofisi hiyo juu ya uadilifu wake.

  Barua hiyo ya Chadema iliyosainiwa na Hamad Yusuf, Mratibu wa Kampeni, Jimbo la Uzini, ambayo gazeti hili liliiona nakala yake ililalamika: “Barua yako ni karipio kwetu na wewe unafahamu kuwa karipio ni adhabu ambayo hutolewa baada ya pande zote kusikilizwa.

  Kwa sababu hukutaka kutupatia muda wa kujieleza juu ya tuhuma ambazo hujatufahamisha, tunataka kuiarifu ofisi yako kuwa hukumu yako ni batili kwa kuwa kikao hicho kilikuwa ni kikao cha ndani cha viongozi na wanachama na tume yako kujulishwa ufanyikaji wake

  Wakati huo huo, Chadema kimeituhumu ZEC kufanya mabadiliko ya ratiba yanayokibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo kama hayataangaliwa kwa makini, kimedai yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani
   
Loading...