Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kimezindua rasmi kanda ya Zanzibar ya chama hicho.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Hamad Yusuf.Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Jamat Khan mjini Unguja.
Viongozi mbalimbali wa mikoa, wilaya,matawi na Makamanda wa chama hicho upande wa Zanzibar walihudhuria.Pia walikuwepo wabunge wa viti maalum Zanzibar.
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wanachama wa chama hicho kushikamana na kuzidi kuisimika Chadema Zanzibar.
Pia Kiongozi huyo aliwamiminia sifa viongozi wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwa kazi kubwa wanayofanya huku akisema viongozi hao wamekuwa kama Nembo ya chama hicho.
Uzinduzi huu wa Kanda ya Zanzibar umefanyika baada ya kukamilika zinduzi za Kanda za Tanzania Bara.