Chadema yazidi kutikisa - Yazoa wana CCM kila kona ya nchi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

• YAZOA WANA CCM KILA KONA YA NCHI

na Waandishi wetu

WIMBI la viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) limezidi kushika kasi kote nchini, ambapo zaidi ya watu 300 wamejiunga na chama hicho mwishoni mwa wiki.

Mkoani Tabora, aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tabora mjini, na diwani katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005, Moses Singu Sangu, ametangaza kujivua uanachama wa CCM na kujiunga na CHADEMA.

Sangu alifikia hatua hiyo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igundu, Kata ya Ifucha Manispaa ya Tabora, akiwa ni miongoni mwa wana CCM 100 waliotua CHADEMA, wakidai kuchoshwa na kukithiri kwa rushwa ndani ya CCM ambayo anaamini hakuna wa kuiondoa.

Sangu ambaye ana kadi namba CDM 0562559, alisema kuhama huko kwa wana CCM mkoani Tabora ni mwanzo tu kwa madai kuwa kuna kundi kubwa zaidi la wanachama litamfuata.

Alisema rushwa imekithiri ndani ya CCM na kutoa mfano wa chaguzi za mwaka 2000 na 2005 ambapo alidai aliongoza katika kura za maoni katika kuteuliwa kugombea udiwani wa kata ya Itonjanda kwa kura 380 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 101, lakini nusura jina lake liondolewe baada ya kufuatwa na mtoto wa kigogo mmoja ndani ya CCM mkoa akitakiwa atoa chochote ndipo jina lipite.

“Nilipofuatwa niligoma kutoa chochota na baadaye nilisikia jina langu limepitishwa kama mshindi halali.... hata hivyo baada ya muda kwenda,” alisema.

Hata hivyo, mwaka 2005 jina lake lilikatwa licha ya kuongoza katika kura za maoni kwa alama 148 huku wa pili akipata kura 48 kwa sababu muhula uliopita alikataa kutoa chochote kwa “mzee”.

Alisema hali ndani ya kata hiyo kwa sasa ni mbaya kutokana na kushamiri kwa rushwa kunakofanywa na watendaji wengi wa vijiji, vitongozi na kata kwani wananchi wamekuwa wakipigwa faini hadi sh milioni moja wanapotenda makosa.

Aliongeza kuwa kutowajibika kwa watendaji wa CCM na serikali, kumechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa ukosefu wa miundombinu, maji na huduma za afya.

Ameeleza kukerwa kwake na tabia ya serikali kuwathamini wananchi kipindi cha uchaguzi tu na baada ya hapo wanaachwa wakiwa hoi.

Mkutano huo uliondaliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA, (BAVICHA), Manispaa Tabora, Saimon Lameck, ulishuhudiwa zaidi ya vijana 100 wakijiunga na chama hicho.

Huko mkoani Singida takriban watu 298 akiwemo mjumbe wa kamati ya utendaji ya jumuiya ya wazazi ya wilaya ya Singida vijijini, Michael Wawa, wamejiunga na CHADEMA katika jimbo la Singida Kaskazini.

Kujiunga kwa wanachama hao kulitokana na ziara ya siku tatu ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Godbles Lema, na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Manyara, Rose Kamili, katika jimbo hilo linalowakiliswa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Katika siku ya kwanza katika kata ya Ilongero, CHADEMA iliwanyakua wana CCM 27, ambapo katika kata ya Ngamu jumla ya wana CCM 210 walijiunga na chama hicho akiwemo Wawa.

Idadi ya walioikimbia CCM iliongezeka katika mkutano uliofanyika kata ya Msange ambapo waliojiunga ni 35 na kijiji cha Mwanyonye wakaingia wanachama 26, na hivyo kufanya jumla ya wanachama wapya waliojiunga na chama hicho kufikia 298.

Juzi jijini Dar es Salaam, zaidi ya wanachama na watu mbalimbali 3,000 walijiunga na CHADEMA katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Jangwani na kuhutubiwa na viongozi wakuu wa chama hicho.

na Waandishi wetu
"na Waandishi wetu" sisi kina nani, wanachama wa JamiiForums?

Au mwandishi wa gazeti la chama kwenda kwa wanachama? Mwandishi umeficha chanzo cha habari, kwa sababu unajua kuwa mtu yeyote mwenye half a brain akisikia imesemwa "chama kinashamiri" lazima atatafuta "nani kasema"? Hahahahaaa...

CHADEMA "yazidi kutikisa" kwa sababu inazoa wanachama wa CCM, lakini hukusema CCM imeshazoa wangapi! Hahahahahhaaaaa...
 
huyu nae....
 
Hivi hapo unacheka?
 
Juzi kwenye mkutano wa Chadema mheshimiwa Tundu Lissu alisema kwamba watanzania walio wengi hawana vyama ambayo ni zaidi ya 85% ya watanzania wote. Sasa inakuwaje Chadema inaweka nguvu nyingi kwenye kuwachukua wana CCM kuliko kuwapata wananchi ambao si wanachama wa chama chochote?
 
Mkutano wa Jangwani, naomba nikiri moyo wangu umetekwa na Mh. Halima Mdee, Nasari chunga mzigo wako?
 
Juzi kwenye mkutano wa Chadema mheshimiwa Tundu Lissu alisema kwamba watanzania walio wengi hawana vyama ambayo ni zaidi ya 85% ya watanzania wote. Sasa inakuwaje Chadema inaweka nguvu nyingi kwenye kuwachukua wana CCM kuliko kuwapata wananchi ambao si wanachama wa chama chochote?

kuanza uana attack adui then unakusanya wengine kiarahisi.
 
Back
Top Bottom