CHADEMA yazidi kupukutika kila siku


MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Messages
5,536
Likes
15
Points
135
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2013
5,536 15 135
SASA ni dhahiri kwamba hali si shwari ndani ya Chadema, baada ya viongozi zaidi kuendelea kuachia ngazi kwa kile walichodai kuchoshwa na hali ya mambo katika chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Said Arfi kujiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa wiki iliyopita, jana ilikuwa zamu ya Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, Ally Chitanda aliyetangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama na pia kujivua uanachama.

Mbali ya kuwa Mwenyekiti wa Mkoa, kabla ya uamuzi wake huo uliotangazwa jana, Chitanda pia alikuwa Katibu wa Sekretarieti katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema Taifa katika makao yake makuu yaliyopo Mtaa wa Togo, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa pia Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

Chitanda alianika uamuzi wake huo jana katika mkutano wake na wanahabari mjini Lindi, akisema amechoshwa na unafiki na uonevu unaoendelea ndani ya chama hicho alichojiunga nacho miaka kumi iliyopita akitokea NCCR-Mageuzi.

Alisema kikao cha Kamati Kuu kilichoketi kwa siku mbili na kufikia maazimio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwavua madaraka Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto, Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ndiyo yaliyomchefua na kuchoshwa na mwenendo ndani ya Chadema.

Akitangaza kujiengua, alisema; "Napenda kuwaambia Wanachadema na Watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Mkumbo ni maamuzi ya kijuha na yanayowafanya Watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema."

Alisema Zitto na wenzake wameonewa, kwani hakuna baya lolote walilolifanya, bali wametoswa kutokana na homa ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama.

"Ni fedheha leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita Zitto Kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena. Si dhambi kumhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili" Alisema.

Hakuna usaliti, uhaini

Aidha, Chitanda ameeleza kuwa, akiwa mtendaji wa ofisi ya Katibu Mkuu, alishiriki pamoja na Zitto na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kupanga mikakati mbalimbali, mizuri na mibaya kwa nchi, lakini hawakuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala jina lolote baya.

"Tumekuwa tukiweka mikakati mbalimbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (Jeremiah Sumari), wakati tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.

"Naomba nikiri kwamba nikiwa Katibu wa Sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za chama kuwajenga wajumbe ‘ndio'," alilalamika Chitanda na kudai kuwa, wakati Dk Slaa akisema mjadala wa Zitto umefungwa rasmi, ni uongo kwa kuwa amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguka nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua Zitto.

Kutokana na mambo yanayoendelea ndani ya chama, amedai nafsi yake haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya Watanzania wenzake.

"Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu. Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.

"Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki. Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dk Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.

"Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama. Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa mwanaChadema, sioni tena sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, sioni tena sababu ya kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu," alisema.

`Kubebana' katika madaraka.

Licha ya kile alichodai ni uonevu dhidi ya Zitto na wenzake, Chitanda pia alilalamikia upendeleo wa nafasi nyeti ndani ya chama kwamba zimekuwa zikiegemea watu wa upande mmoja.

Mathalani, alisema pamoja na uamuzi wa kuwavua madaraka Zitto na wenzake hivi karibuni, Kamati Kuu pia iliridhia uteuzi wa wakurugenzi watano na kuwaongezea pia maslahi.

Aliwataja wakurugenzi hao ni Benson Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni), John Mnyika (Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya Ndani), Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji), John Mrema (Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri) na Wilfred Lwakatare (Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama).
Kwa mujibu wa Chitanda, uteuzi huo hauoneshi sura ya kitaifa kwani kati ya kurugenzi zote sita, nne zinaongozwa na watu wanne kutoka Mkoa mmoja wa Kilimanjaro.

Alisema mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na posho nono, akisema wakurugenzi waliokuwa wakilipwa Sh 800,000 kwa mwezi, sasa watakuwa wakilipwa kati ya Sh milioni 1.5 na milioni 2.5 wakati maofisa waandamizi waliokuwa wanalipwa Sh 680,000 sasa watalipwa hadi Sh milioni 1.5.

"Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza Kuu ni pamoja na kulipa posho kwa makatibu wa wilaya na mikoa. Hawa ndio watendaji muhimu katika ujenzi na uhai wa taasisi hii lakini, hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na mali," alisema.

Tangu uamuzi wa Kamati Kuu wa kuwavua madaraka Zitto na wenzake kwa tuhuma za kupanga mikakati ya `uhaini' ndani ya chama, kumekuwa na mpasuko ndani ya chama, wengine wakiunga mkono uamuzi wa uongozi na wengine wakipinga kwa madai kuwa nguvu kubwa imetumika `kuwaonea' wanasiasa hao vijana, lakini pia wenye nguvu na ushawishi wa kisiasa.

Miongoni mwa wanaotajwa kutoridhika kuondolewa kwa Zitto na wenzake ni mwanazuoni na mkongwe katika duru za kisiasa ambaye pia ni mshauri wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyekaririwa kukionya chama kwa hatua hiyo, akisema haikuwa na ulazima kwa sasa, bali mambo yangeweza kusawazishwa kwa mazungumzo.

Naye Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa Baraza Kuu, Patrick Joseph, alitoa kauli iliyodhihirisha kuwa yeye ni mmoja wa wanaomwunga mkono Zitto.

Wengine ni Mwanasheria wa Mbowe, Albert Msando ambaye sasa ni Mwanasheria wa akina Zitto. Wakati Chitanda akiyasema hayo, Ofisa Mwandamizi wa Habari Chadema, Tumaini Makene jana jioni alitoa taarifa inayofafanua madai kadhaa ya Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Lindi aliyejiuzulu.

Katika ufafanuzi wake, alisema hakuna upendeleo katika ugawaji wa madaraka, akisema kati ya wakurugenzi sita waliopo kwa sasa, ni wawili tu ndio wanaotoka Kilimanjaro, Mrema na Komu.

Wengine na mikoa yao ni Mnyika (Mwanza), Kigaila (Dodoma) na Lwakatare (Kagera). Aidha, Makene aliyesema mjadala wa Zitto na wenzake umefungwa na kwamba zinasubiriwa taratibu za kikatiba ndani ya chama, alisema wakurugenzi waliotajwa si wapya katika nafasi zao, bali mpya ni mmoja, ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu. Kibatala ana asili ya Mkoa wa Morogoro.

Amekanusha pia kuwa Chitanda alikuwa Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu, akisema nafasi hiyo ambayo imo ndani ya Katiba ya Chadema haina mtu mpaka sasa.

"Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa Chadema," anasema na kuongeza kuwa, kauli ya Chitanda kwamba Zitto na wenzake wameonewa kwa hofu ya uchaguzi inashangaza kwani ni kauli za mara kwa mara zinazotoka kwa mahasimu wa Chadema kisiasa.

Chanzo: Habarileo.
 
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Messages
5,536
Likes
15
Points
135
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2013
5,536 15 135
Ulaghai unapofika kileleni huko ndiko kwenye point of no return zaidi ya kuparanganyika na kuanza ulaghai tena upya.

CHADEMA kimewalaghai wananchi kwa muda mrefu na kwa sasa kimefikia kikomo cha ulaghai ambapo kwa wananchi wameanza kuufahamu ukweli wa sababu ya CHADEMA kuwepo kwenye uwanja wa siasa.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

These people are just political profiteers.

Waacheni wafu wa siasa wazikane.
 
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Messages
4,701
Likes
569
Points
280
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2007
4,701 569 280
Mamba ni Mjanja akiwa ndani ya maji ila akiwa nje .......
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
527
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 527 280
Chadema imekufa mapema kuliko muda aliotabiri Wassira.

Kweli kauli za watu wazima hazipaswi kubezwa...
 
mtz one

mtz one

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
3,894
Likes
407
Points
180
mtz one

mtz one

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
3,894 407 180
kijiwe cha WALAGHAI
 
Chris Lukosi

Chris Lukosi

Tanzanite Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
4,586
Likes
34
Points
145
Chris Lukosi

Chris Lukosi

Tanzanite Member
Joined Aug 23, 2012
4,586 34 145
Chadema ni nyumba ya barafu, jua limewaka na ndio mwisho wake
 
mtwa mkulu

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Messages
2,552
Likes
564
Points
280
mtwa mkulu

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2013
2,552 564 280
Chama Changu C (C+1) M Kina Hali Ngumu Sasa!
 
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,983
Likes
7,817
Points
280
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,983 7,817 280
Ulaghai unapofika kileleni huko ndiko kwenye point of no return zaidi ya kuparanganyika na kuanza ulaghai tena upya.

CHADEMA kimewalaghai wananchi kwa muda mrefu na kwa sasa kimefikia kikomo cha ulaghai ambapo kwa wananchi wameanza kuufahamu ukweli wa sababu ya CHADEMA kuwepo kwenye uwanja wa siasa.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

These people are just political profiteers.

Waacheni wafu wa siasa wazikane.
Mwenezi,siku nyingine jaribu kuleta bandiko lako la kiuchunguzi na kiuchambuzi.Haya mambo ya copy and paste yamepitwa na wakati. Ni hayo tu Katibu

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

 
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Messages
5,536
Likes
15
Points
135
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2013
5,536 15 135
Mwenezi,siku nyingine jaribu kuleta bandiko lako la kiuchunguzi na kiuchambuzi.Haya mambo ya copy and paste yamepitwa na wakati. Ni hayo tu Katibu

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mwenezi ndiyo nini?.

Ushauri wako upeleke kwenye ofisi za BAVICHA ambako hawajitambui kisiasa.

Mpe Mselewa habari za CCM pwani kwa kile kilichofanyika on 27th Nov 2013

Endelea kuwalaghai watu kama wewe unafanya kazi ofisi ndogo Makao Makuu kama ilivyo jadi ya CHADEMA.

Ulaghai wa CHADEMA uko ukingoni kukiporomosha.
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
527
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 527 280
Vijijini Chadema inaonekana kama UKOMA...
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
527
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 527 280
Mwenezi,siku nyingine jaribu kuleta bandiko lako la kiuchunguzi na kiuchambuzi.Haya mambo ya copy and paste yamepitwa na wakati. Ni hayo tu Katibu

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Tupa Tupa Mzee wa Lumumba, vipi zile siku 14 mmeshaanza kuzihesabu?
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,902
Likes
10,122
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,902 10,122 280
Mgongano wa kimaslahi kati ya chadema asili na chadema family,mapambano kati ya wahafidhina na wapenda democrasia!!
 
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,654
Likes
35
Points
145
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,654 35 145
Magamba naona wanajitekenya na kujichekesha wenyewe!
 
L

lupe

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
5,659
Likes
5
Points
0
L

lupe

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
5,659 5 0
Mwenezi,siku nyingine jaribu kuleta bandiko lako la kiuchunguzi na kiuchambuzi.Haya mambo ya copy and paste yamepitwa na wakati. Ni hayo tu Katibu

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Asanteee
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,936
Likes
1,600
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,936 1,600 280
Chama cha majungu lazima kife tu.
 
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Messages
12,485
Likes
2,581
Points
280
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2012
12,485 2,581 280
Haya mmeshayaliza ndio uanze ya wenzako?
1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,181
Likes
121,794
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,181 121,794 280
Thank you Amina mohamed, BAK anakupendaje weye!!!!!!
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,181
Likes
121,794
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,181 121,794 280
Ulikuwa unaheshimika hapa jamvini lakini umeamua kujivisha uhayawani kama wale wa uwanja wa fisi na kuandika pumba za hali juu. Endelea na utaahira wako maana ulikuwa unahama chumba kimoja cha darasa na kuhamia chumba kingine kila mwaka lakini kumbe hukuelimika hata kidogo.

Vijijini Chadema inaonekana kama UKOMA...
 
ifweero

ifweero

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Messages
7,962
Likes
46
Points
145
Age
39
ifweero

ifweero

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2013
7,962 46 145
Mwenezi,siku nyingine jaribu kuleta bandiko lako la kiuchunguzi na kiuchambuzi.Haya mambo ya copy and paste yamepitwa na wakati. Ni hayo tu Katibu

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

bado kidogo utaanza kuokota makopo
 

Forum statistics

Threads 1,252,180
Members 482,015
Posts 29,799,241