CHADEMA yazidi kubomoka, katibu mwenezi atimkia CCM

Tanzania Daima hawezi kuandika hiyo habari wewe utakuwa umetumwa!
 
Tanzania Daima hawezi kuandika hiyo habari wewe utakuwa umetumwa!

Ha ha ha ha haaaaaaaa! Mwanzo nilisoma post bila kucheki ID ya mtumaji nikataka kukushukia! Kumbe ni wewe mkuu? Wenyewe wanaponda bila hata kusoma chanzo cha habari.
 
hivi yeye alipokwenda Cdm alimwambia nani? hvi hizo njaa zako unadhani zitamalizwa na CCM? wamakupata wamekutumia sasa subiri uone kama watakuwa na wewe tena!
 
Na bado mpaka watakwisha wooote. Mbowe badilika ubaguzi na ukabila na ubabe utakimaliza chama. weka wazi mambo watu wanakitegea sana chama hicho
 
Acheni ubishi GT's ni kweli huyo katibu uenezi wa CDM na mjumbe mmoja wamehamia CCM na walikabidhi katiba na kadi ya CDM na walipokewa kwa vifijo na nderemo, mimi nilikua kwenye huo mkutano jimbo la Gairo. Ni ukweli uliowazi CDM wanazidi kubomoka na CCM inazidi kuimarika.
 
[Katibu mwenezi wa CDM Wilaya ya Kilosa Bw. Raymond Mlama pamoja na mjumbe mmoja wameamua kuhamia ccm kwa kile walichoeleza kuwa wameona ina sera zinazoridhisha na kuwalenga wengi].

UKWELI WA HILI NI KUWA CHADEMA INAIMARIKA ZAIDI. Hawa wanadai wanarudi CCM ni wanafiki waganga njaa na hawakuwa na jambo wanataka kufanya kwa ajili ya nchi hii, wengi wanataka wafanyiwe. Wacha pakacha livuje.
 
Katibu mwenezi wa CDM Wilaya ya Kilosa Bw. Raymond Mlama pamoja na mjumbe mmoja wameamua kuhamia ccm kwa kile walichoeleza kuwa wameona ina sera zinazoridhisha na kuwalenga wengi.

Source: Tanzania Daima


CCM watakoma hadi mtaripoti balozi wa CDm kuhama, huu mwaka noma..
 
duh,hii sasa noma!!!!!!!!!
ilianza sengerema,ikaenda geita na Ilemela akahamia Nachingwea,sasa tena Kilosa..............mbona kazi??????????????
kibaha nako naskia kimenuka.
 
Issue ni ndogo sana katika siasa pana, ngazi hiyo sidhani kama inawezi kukisitua chama chochote makini. la msingi achunguzwe kama amekifisadi chama ????? Hao wengine wanapiga debe kuwakatisha tamaa...stand firm bigup...
 
Inashangaza kuona kwamba CCM imeshindwa kutekeleza ilani waliyoinadi kwa wananchi 2010 na sasa mafanikio yao ni kupata wanachama kutoka CHADEMA halafu eti tunashangaa kwa nini nchi haiendelei mpaka leo. Only in Tanzania...... Yaani CCM mpaka leo 2012 bado inacheza na siasa za Mrema 1995
 
Kuna watu wengi wanaona kati yao ni asilimia kumi tu hukitambua wakionacho, kati ya hao ni asilimia kumi tu hufanya uamuzi muafaka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom